ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Swali:
Je ni lazima kuendelea kununua mandege ya kampuni ya Boeng?
---
LICHA ya mafanikio yanayopatikana kwenye Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Kamati ya Bunge ya Miundombinu imesema matatizo ya kiusanifu ya injini za Airbus A220-300 ambazo zimekuwa zinapata hitilafu mara kwa mara, yanasababisha kukosa mapato wastani wa Sh. bilioni 127.3 kwa mwaka.
Akiwasilisha bungeni jana taarifa ya mwaka ya kamati hiyo kwa kipindi cha Februari 2024 hadi Januari 2025, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Moshi Kakoso, alishauri serikali iharakishe upatikanaji injini mbadala za ndege aina ya A220-300 na pia itafute namna bora ya kuhakikisha ndege hizo zinaleta faida kwa nchi.
Mwenyekiti huyo alitaja changamoto nyingine ni upatikanaji vipuri kutokana na kushuka kwa uzalishaji vipuri hivyo duniani kutokana na athari za UVIKO-19.
Alisema ATCL pia inakabiliwa na uhaba wa marubani, hususan marubani viongozi, na wahandisi wenye leseni ya kuruhusu ndege kuruka baada ya matengenezo kukamilika.
View: https://x.com/Nipashetz/status/1886716612599845078?t=9cBWcQjvVHCqeKHZFAar-Q&s=19
Swali:
Kwa hasara hizi ,Kuna haja gani Sasa ya kuwa na Shirika la ndege?
Si Bora kulibinafsisha Kwa ubia Serikali iwe na hisa chache Ili kuokoa haya mabilioni ya walipakodo yanayopotea?
View: https://www.instagram.com/p/DF7NLhPCg0A/?igsh=Y2dwNDR2czdsZ2dv