Kamati ya Bunge Utawala, Katiba na Sheria yapokea maelezo ya Waziri wa Katiba na Sheria kuhusu muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria ya shule

Kamati ya Bunge Utawala, Katiba na Sheria yapokea maelezo ya Waziri wa Katiba na Sheria kuhusu muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria ya shule

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Florent Kyombo ameongoza kikao cha kamati hiyo kilichopokea Maelezo ya Waziri wa Katiba na Sheria kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Shule ya Sheria Tanzania (The Law School of Tanzania (Amendment) Act, 2024) na Maelezo ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2024 (The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Act, 2024);

Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.2) wa mwaka 2024 (The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No.2) Bill, 2024); na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (The Prevention and Combating of Corruption (Amendments) Bill, 2024) tarehe 14 Agosti, 2024 Bungeni Jijini Dodoma.

Kamati hiyo inategemea kupokea na kusikiliza Maoni ya Wadau kuhusu Miswada hiyo tarehe 15 na 16 Agosti, 2024.

mini_magick20240814-11513-zqak0q.jpg
mini_magick20240814-11513-metfdj.jpg
mini_magick20240814-11513-be581s.jpg
mini_magick20240814-11513-62mk9n.jpg
mini_magick20240814-11513-zsmwst.jpg
mini_magick20240814-11513-xn04j5.jpg
mini_magick20240814-11513-vlan57.jpg
mini_magick20240814-11513-6fs5qo.jpg
mini_magick20240814-11513-w1h110.jpg
mini_magick20240814-11513-3du3iy.jpg
 
Back
Top Bottom