Mtumishiwetu
Senior Member
- Jul 13, 2022
- 196
- 346
Naomba kwa heshima na unyenyekevu mkubwa niwasilishe maoni yangu ikiwa Kamati za Bunge zinakutana Dodoma kujadili masuala mbalimbali yanayohusu nchi yetu.
Naomba Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson aivunje Kamati ya Bunge ya Bajeti kutokana na Kamati hiyo kushindwa kusimamia masilahi mapana ya taifa letu na kusababisha maumivu makubwa kwa wananchi.
Leo kila kitu kimepanda bei, tozo na mambo lukuki ambayo yalipaswa kusimamiwa na kukataliwa na kamati hiyo ili yasilete madhara kwa wananchi na uchumi wa nchi.
Naomba watanzania wenzangu tuungane kumuomba Spika aivunje Kamati hii na kuiunda upya kama walivyofanya maspika wenzake waliopita pale inapothibitika Kamati imeshindwa kusimamia kikamilifu majukumu yake.