Kamati ya bunge ya huduma za jamii yaonesha upofu shule ya sekondari dunda bagamoyo

Kamati ya bunge ya huduma za jamii yaonesha upofu shule ya sekondari dunda bagamoyo

Joined
Feb 8, 2012
Posts
92
Reaction score
9
Leo 19/03/2013 Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii imefanya ziara ya kutembelea shule mbalimbali Wilaya ya Bagamoyo na kukagua miradi mbalimbali ya TASAF kama vile ujenzi wa madarasa,maabara, nyumba za walimu pamoja na hosteli.

Katika ziara yake hiyo imetembelea shule ya sekondari Dunda na kukagua ujenzi wa ofisi ya utawala pamoja na madarasa. Wameridhika na hali mbaya na matatizo lukuki yanayoikabili shule hiyo iliyopo katika jimbo la Waziri wa Elimu Dk. Shukuru Kawambwa. Vile vile shule hii ipo eneo muhimu sana lenye makazi ya mheshimiwa rais Jakaya Kikwete.

Shule hii ipo takriban kilometa 3 kutoka mjini Bagamoyo. Matatizo yanayoikabili shule hii ni uvamizi wa ardhi ya shule kwani sehemu ya mbele ya shule karibu na barabara imeshamegwa na kuuzwa kwa tajiri mmoja aliyeahidi kutoa rushwa ya gari kwa kigogo mmoja wa Idara ya Ardhi ngazi ya wilaya. Hata sehemu ya nyuma ya shule ilikwishauzwa kwa tajiri mmoja, juhudi ya mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa shule ziliokoa ardhi hii kwa kumtumia Mkuu wa Wilaya. Mkuu wa Wilaya aliingilia kati na kuirudisha ardhi hii kwa shule.

Kamati hiyo pofu ikishirikiana na watu wa TASAF waliowapa baadhi ya watendaji wa mtaa na walimu fulana na kofia, wamejifanya vipofu kwa kutoona ukosefu wa umeme katika shule hiyo inayoleta taswira mbaya kwa Waziri wa Elimu mpaka kwa rais. Walichokifanya ni kuhoji matokeo ya kidato cha nne huku wakiridhika na hali mbaya ya shule iliyo na madarasa yasiyokuwa na sakafu bali vumbi.

Kamati kama hii ni mzigo kwa Taifa letu kwani inafanya kazi kwa ubabaishaji wa hali ya juu. Nilifikiri walivyoitembelea hiyo shule vile vile wangeangalia mambo mengine ya msingi kama ujenzi wa nyumba ya mwalimu uliosimama, mazingira bora ya ufundishaji, ujenzi wa hosteli za wanafunzi, umeme,pamoja na mipaka ya shule inayomegwa.
 
Back
Top Bottom