JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini imeridhishwa na uhakika wa upatikanaji wa umeme wa gesi katika kituo cha kufua umeme cha Kinyerezi II ambacho kinazalisha megawati 240 ambazo zinaingizwa kwenye gridi ya taifa.
Kamati hiyo imefanya ziara katika Kituo cha Kinyerezi II kujionea uendeshaji wake, kabla ya kutembelea kituo hicho, kamati ilitembelea mitambo ya uzalishaji wa gesi mkoani Mtwara.
Akizungumza Alhamisi Oktoba 13, 2022 baada ya kukagua shughuli zinazofanyika, mwenyekiti wa kamati hiyo, Dunstan Kitandula amesema wameona jinsi kituo hicho kinavyoweza kuzalisha megawati 240 na upatikanaji wake ni stahimilivu.
"Tanesco wametuhakikishia wana mipango madhubuti ya kuhakikisha wana uwezo wa kupata vifaa kipindi chote cha mwaka bila kuwa na matatizo yoyote," amesema Kitandula.
=================
KAMATI YA KUDUMU YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YATEMBELEA MRADI WA KINYEREZI II NA KURIDHISHWA NA HALI YA UZALISHAJI UMEME
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dastan Kitandula amesifu jitihada zinazofanywa na TANESCO katika kuhakikisha kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi II kinazalisha umeme kwa mujibu wa uwezo wake na hivyo kusaidia upatikanaji wa nishati ya umeme kuwa ya kuridhisha na kuchangia uchumi wa nchi.
Kitandula ameyasema hayo wakati alipokuwa akizugumza kwenye ziara ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyotembelea kituo hicho kujionea hali halisi ya uzalishaji kwenye kituo hicho.
Ameisifu TANESCO kwa kuweka mikakati mizuri ya matengenezo ya miundo mbinu ya kituo hicho kwa kuingia mikataba ya muda mrefu na makampuni yaliyotengeneza mashine hizo ili kuleta unafuu na urahisi wa upatikanaji wa vipuri wakati inapotokea hitilafu.
Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa usambazaji umeme, Mhandisi Athanasius Nangali, ameahidi kuendelea kuboresha miundo mbinu ya umeme kwa kuhakikisha wateja wanapata huduma kwa wakati na bora kwa ajili ya kuinua uchumi wa nchi.
Kituo cha Kinyerezo II kina uwezo wa kuzalisha MW 240 za umeme kikiwa kina jumla ya mitambo nane (8), ambapo mitambo sita (6) ikiwa ni ya gesi asilia na mitambo miwili (2) inatumia teknolojia ya mvuke kuzalisha umeme.