Duh si mchezo manake haya ndiyo yale yaliyoongelewa kule http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=8939 na sasa wameanza kukwangua hivyo nadhani hii kamati ikiwa makini itaweza angalia madudu yote yakiwamo ya mizigo kuchelewa kutolewa bandarini...... Nadhani sasa waheshimiwa kule Bungeni wameanza kuamka na "my take" ni kwamba moto lazima utawaka katika kikao kijacho cha bunge pale mjini Dom (nadhani kuanzia wiki ijayo kama sijakosea)!!!
Hatujaambiwa ni makontena laki sita kwa mwezi au vipi. TICTS itahakikisha uwezo wa kupitisha hiyo idadi ya makontena haufikiwi. Wamejiwekea kipengele kitakachowaruhusu wawe na huo mkataba mpaka watakapopenda wenyewe. Na naamini watakuwa wameweka kipengele kingine kisemacho mahakama za Tanzania hazina ubavu wa kuamua lolote la kuhusu mkataba wao.
Iweje kontena lilipiwe $80 na sisi tuambulie $15 tu? Kuna mtu kasema wajinga ndio waliwao. Serikali ya CCM imetufanya tuwe wajinga waliwao na kila mgeni?
Mwalimu,
Kwanza naomba uelewe kwamba hiyo si Kampuni ya Kigeni ni hao hao walio serikalini na kwenye NEC ndiyo wenye hiyo Kampuni.TICTS wamegoma kufanya kazi masaa 24 kwa kuwa wakifanya hivyo idadi ya makontena itazidi laki sita na hivyo wataingia kwenye biashara ya ushindani na wao hawataki ushindani.
Mkataba ni wa miaka 10 na sasa miaka 25, kwanini wasinunue malori ya kubeba makontena kutoka bandarini kupeleka Ubungo ambapo pia wamepewa kwa ajili ya shughuli hiyo? Hao ndio wawekezaji ambao utendaji wao umeonekana ni mzuri sana kiasi cha kuongezewa miaka 15 hata kabla miaka 5 ya mwanzo haijaisha? Hiyo review ya utendaji wa TICTS ilifanyika lini na walitumia vigezo gani???
Si waseme tu ukweli kwamba TICTS walichangia kampeni ya mgombea urais wa CCM na wakapewa nyongeza ya mkataba na kuwapa monopoly zaidi ili waendelee kuvuna hela za bure!
.Kuna wakati najuiliza kama Spika na hata baadhi ya wabunge wanasoma katiba au wanaizungumzia tu hivi hivi.
Nina sababu za kudhani hata Waziri wa Sheria na Katiba hajawahi kusoma katiba yetu
Kuna wakati najuiliza kama Spika na hata baadhi ya wabunge wanasoma katiba au wanaizungumzia tu hivi hivi.
Nina sababu za kudhani hata Waziri wa Sheria na Katiba hajawahi kusoma katiba yetu.
Kuna wakati najuiliza kama Spika na hata baadhi ya wabunge wanasoma katiba au wanaizungumzia tu hivi hivi.
Nina sababu za kudhani hata Waziri wa Sheria na Katiba hajawahi kusoma katiba yetu.