Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Kamati ya Kudumu ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imeipongeza Serikali kwa kukamilisha vipande viwili vya vya mradi wa Reli ya Kisasa ya SGR na kuanza kutoa huduma.
Akizungumza jijini Dar es Salaam tarehe 14 Novemba 2024 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Mhe. Augustine Vuma (Mb), amesema kuanza kutoa huduma kwa sehemu hizo zilizokamilishwa ni kiashiria kuwa Serikali imejipanga kutoa huduma za viwango kupitia reli na hivyo kuchochea uchukuzi.
Mhe. Augustine Vuma amelitaka Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuweka mikakati ya kuhudumia mizigo ili kupitia huduma hiyo waweze kujiendesha bila kutegema fedha kutoka Serikali Kuu.
Naye, Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Mhe. David Kihenzile ameihakikishia Kamati hiyo kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha huduma za SGR zinaendelea kuboreshwa kufikia viwango vya Kimataifa lengo likiwa kupata thamani ya fedha kupitia Uwekezaji mkubwa uliofanywa kwa Ujenzi wa reli hiyo.
Mhe. David Kihenzile amesema Kamati imeridhishwa na kazi kubwa sambamba na mikakati iliyowekwa ya kujenga Reli ya Kisasa toka Dar es salaam, Mwanza hadi Kigoma yenye urefu wa zaidi ya KM 2,000 ambapo takribani Dolla Bilioni 10 sawa na shilingi Trilioni 27 zimewekezwa.
Mhe. David Kihenzile ameelezea jinsi Serikali ya awamu ya sita inayoongonzwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassaan inavyoendelea kuboresha Sekta zingine zenye uhusiano wa moja kwa moja na maboresho ya Reli ya Kisasa Nchini ikiwemo kutumia takribani Trilion Moja kwa ajili ya kujenga na kukarabati Meli na Kiwanda cha Kujengea Meli kwenye Maziwa Makuu, zaidi ya Trilion 5 zimeendelea kutumika kujenga miundombinu ya Bandari Nchini.