Kamati ya bunge ya mambo ya nje,ulinzi na usalama umeitaka serekali kukataa muundo wowote wa ushirikiano wa Afrika mashariki utakaoruhusu ardhi ya Tanzania kutumika kwa manufaa ya shirikisho.
Kamati ya bunge imeitaka serekali kuwa makini na suala la ardhi kwani ni rasilimali adimu na urithi pekeewa wananchi wa Tanzania.
Kamati ya bunge iliwasilisha rasmi mapendekezo yake kwa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa mheshimiwa B Membe.
Hakuna mtanzania halisi atakayepingana na kamati ya bunge ya mambo nje,ulinzi na usalama.Tatizo langu mpaka sasa watanzania bado tumeshikilia ardhi tu bila kuangalia mambo mengine muhimu kama free movement nadhani nalo ni hatari sana hasa katika sector ya utalii na usalama wetu.Miaka ya nyuma wakenya waliidanganya dunia kuwa mlima Kilimanjaro uko Kenya sasa kama free movememnt nayo isipoangaliwa vizuri tutarudi kulekule tulikotoka.
Sector ya utalii inatoa mchango mkubwa katika kukuza pato la taifa hakuna asiyejua wenzetu wamepiga hatua kubwa katika sector ya utalii tusipo angalia makampuni makubwa yaliyopo Tanzania yanaweza kutoweka kabisa.
Kichwa cha mada ni kibovu. Kamati ya Bunge haiwezi kukataa "ardhi ya Tanzania kutumika kwa manufaa ya EAC". Mbona tayari ardhi ya Tanzania inatumika vizuri tu kwa manufaa ya EAC? Makao makuu ya EAC yapo kwenye ardhi ya Tanzania, na tungependa watumie ardhi yetu kuweka taasisi za EAC zaidi.
There must be give and take. We must win some and lose some. Ni ajabu kuona nchi yenye makao makuu ya EAC inakuwa mstari wa mbele kupinga mipango ya EAC.
Ukitaka cha mvunguni sharti uiname. Tukitaka umoja sharti tukubali kuuchangia kwa hali na mali.