Kamati ya Bunge Yaridhishwa na Kasi ya Ujenzi wa Uwanja wa Arusha

Kamati ya Bunge Yaridhishwa na Kasi ya Ujenzi wa Uwanja wa Arusha

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA KASI YA UJENZI WA UWANJA WA ARUSHA

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo chini ya mwenyekiti wake Mhe. Husna Sekiboko imeridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu wa Jijini Arusha kufuatia muda na kiasi cha pesa ambacho Serikali imeshatoa kwa ajili ya ujenzi huo.

Amesema hayo Septemba 7, 2024 Jijini Arusha mara baada ya Kamati hiyo, kutembelea maendeleo ya Ujenzi wa uwanja huo.

“Sisi kama kamati tumeridhishwa sana na maendeleo ya ujenzi wa uwanja huu katika hatua ya mwanzo kabisa ambapo hadi sasa Serikali imeshatoa kiasi cha Shilingi Bilioni 50, tunauona utayari wa Serikali kukamilisha mradi huu na sisi kama Bunge hatutakuwa kikwazo katika kuunga mkono jitihada nzuri ambazo zinaendelea kuwekwa na Serikali yetu” amesema Mhe. Sekiboko

Ametoa rai kwa Serikali na mkandarasi juu ya kukamilisha mradi huo kwa wakati na kuzingatia ubora unaotakiwa huku akigusia kuanza kwa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu wa Dodoma.

Kwa upande wake Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema kuwa Serikali imepokea maelekezo na ushauri wa kamati na kuwahakikishia kuwa itasimamia utekelezaji wa mradi huo kwa ufanisi zaidi.

Ujenzi wa uwanja huo utakaotumika kwa mashindano ya AFCON 2027 tayari shughuli zilizofanyika ni pamoja na kuchimba eneo la uwanja kuondoa udongo usiofaa, ujenzi wa majengo ya muda kwa ajili ya ofisi na makazi ya mkandarasi.

GW4VIrdXQAAvauk.jpg
GW4VJBdXIAAGiac.jpg
GW4VJBeWgAA-zkx.jpg
GW4VJnbWQAAs4fZ.jpg
Screenshot 2024-09-08 at 15-33-15 Wizara ya Sanaa(MCAS) (@wizara_sanaatz) • Instagram photos a...png
Screenshot 2024-09-08 at 15-33-15 Wizara ya Sanaa(MCAS) (@wizara_sanaatz) • Instagram photos a...png
Screenshot 2024-09-08 at 15-43-14 Wizara ya Sanaa(MCAS) (@wizara_sanaatz) • Instagram photos a...png

Soma Pia: Bilioni 286 kujenga uwanja Mpya wa 'Samia Suluhu Hassan Arusha Stadium' Kwa ajili ya AFCON 2027
 
Back
Top Bottom