#COVID19 Kamati ya Corona: Serikali itoe taarifa uwepo wa Ugonjwa wa COVID-19 na kuruhusu matumizi huru ya chanjo

Lazima ripoti inenepe kujustfy mkwanja mnene waliovuta. Naamini mapendekezo haya ya tume yangeweza kutolewa NA Rais au Waziri wa Afya bila hata Kaunda tume. Upigaji uendelee
 
Hiiii misimamo ndo imemgharimu!
Haya ..ila.kikubwa ujue kuwa maisha hapa Tanzania yalikuwa Kama kawaida..watu tulikusanyika na kujumuika Kama Ilivyo ada yetu..tuliamua kuishi na ugonjwa huunkama.magonjwa mengine na maisha yakaendelea tu...sasa Hawa wakuna vitambi wanataka kiturudisha kwenye masharti ya kiganga
 
Ningeshangaa kama kamati ingekuja na mambo mapya kabisa yote tofauti na nchi zingine, labda kama ingeamua kuendeleza ubishi wa zamani ambao haukuwa na maana yoyote.
Dunia imeshafanya uchunguzi , wao kirahisi kabisa walitakiwa kupitia tafifiti za wenzao duniani ,kuzichanganua na kisha kuja na majibu ,,na naamini ndivyo walivyofanya.

Lakini wapiga nyungu hawajakatazwa.
Na chanjo ni hiari.
Hatua kama za kuvaa barakoa kwenye mikusanyiko na kunawa mikono hizo ni za kawaida.

Labda nikuulize: Lipi kati ya hayo limekukwaza ndugu yangu?
 
Uko lndia ambao ni watengenezaji wakubwa wa chanjo, unaona wamepotea wangapi kwa siku? Wewe ni njinga kama wajinga wengine haujui dunia inavyoenda.Ngoja takwimu kuhusu corona zianze kutoka,ili mfungiwe ndani kama kuku ndio utajua, maana Samia ndicho anachokitafuta
 
Imepoteza hela kama zile Trilion 1.5 za Mayanga Construction kujenga airport vichakani Chattle?
 
Kwa hiyo unataka chanjo kama wazungu. Tatizo lako unakopi na kutuletea unayaona mitandaoni na kuyasikia kupitia king'amuzi. Unavyoona kwa miaka miwili na zaidi ya kuishi na COVID-19 hali ni ngumua kiasi cha kuhitaji na kukubali madhara hayo ya chanjo? Madhara ya chanjo baada ya miaka 3, 5, 10 n.k. umeshayaelewa? Ni kweli hutambui chanjo zote zimepitishwa kwa mpango dharula kuokoa wanavyoteketea? Je sisi tunateketea? Kenya waliteketea? Burundi Uganda, Rwanda, majirani ...... wanateketea.

Tumieni akili bhana!
 
Huyo ndio kiongozi wa Kweli, maana ya kiongozi ni kujitoa kwa ajili ya watu wako,hata kama itakugalimu maisha yako,sio huyu takataka kazi ni kujipamba na kupaka lipstick tu, unafikiri anatafuta umiss Tanzania
 
Mama yenu amezungukwa na madalali ,dalali yupo radhi kusema uongo mkubwa hili apate kodi ya mwezi mmoja tu na kukuacha ww ukiangaika miezi 6 au mwaka mzima
Tangu alipoanza teuzi za kurudisha watu waliokwisha kaa kijiweni kwa ufisadi wao, hapo ndo nimeona njia yetu ilivyo na utelezi. Hatutapiga hatua na sijui ni kweli anafuta ushauri wa wastaafu? Yaani unahitaji kamati ya kukwambia vaa barakoa?
 
Nina uhakika huyu waziri sasa hivi angekuwa kichaa kama siyo Magufuli kufariki. Yale aliyokuwa anafanya ili kumridisha ni maluweluwe ya hali ya juu.
Eti kachumbari ni dawa ya covid19..tokea lini?..kwa clinacal trials gani?

Ama kwa hakika angekuwa amedata sasa hivi mkuu kama ulivyosema.
 
Potelea mbali, ukweli ni kwamba tunachangamana vizuri sana, tabiri zao hazitimii, matakwa yao yanaenda kutimizwa kwa lazima.

Kijiji ninachoishi, hakuna mwenye habari na yanayoendelea mjini, vilabuni tunatembeza kombe, mpirani kama kawa, ibadani hatuachiani nafasi na hasa kipindi cha mvua, bati linavuja vuja, tunamshukuru Mungu, katika miezi 8, tumeondokewa na wapendwa wetu wawili ingawa kwa niliyoyasikia ilibidi tuwe tumetoweka.
 
Kama ingekuwa hivo basi wasingebadili mawazo ya kwamba watu chini ya miaka 50 wasitumia hiyo chanjo ya astra... na kuagiza chanjo nyingine ya moderna ambapo kwa nchi zetu za kiafrika ni ngumu kuinunua kwa sabb ya gharama kubwa. Kwa sasa huwezi elewa kwa sababu ya ushabiki lakini kuna wakati utafika utajua kwann kuna mapingamizi mengi sana juu ya hizi chanjo.

Yamkini watengenezaji wana nia nzuri ila suala likiwa na maslahi mbele, lazima kuna vitu havitaenda sawa. Mshika mawili siku zote moja humponyoka for th3 seek of us not being kisiwa. Aibu kubwa
 
Chanjo ni hiyari.Kama hutaki hakuna atakayekulazimisha.Ni udikteta kitu ambacho wewe hukitaki basi ulazimishe kwa hoja dhaifu wengine wakikatae.Hakuna ambaye ana power of attorney ya kuamulia wengine.Kila mmoja wetu atafanya uamuzi wake kwa mahitaji yake na familia yake.
 
Simpendi Magufuli na nimeona bora kafa
Ila kwenye ishu ya Corona alicheza kama Pele
Kwa nn haya mafua yanapigiwa chapuo namna hii tofauti na TB Ukimwi n.k
Kipo kitu nyuma ya pazia
Hata yeye alisema, "Mtanikumbuka kwa mazuri, sio kwa mabaya"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…