Huwakilishi watanganyika chief,halafu kiongozi sio lazima atuongoze kwa kufoka foka.Kwanza huyu ni Rais wa Katiba tu,Kama sio kubebwa na Magufuri Nani angelikubari Samia awe rais wetu,rais gani nyoronyoro hivi,aende kwao zanzibar sie Watanganyika tulisha choka,kwanza ni mvivu.anawaza misaada tu.
Matumizi mabaya ya kodi za wananchi tu taarifa gani watazitoa zaidi ya porojo tu hv watanzania wanaitaji tume kuja kuambiwa wavae barakoa,wanawe mikono na maji tiririka ,wakae social distance kweli? Maana hakuna jipya watakalokuja nalo zaidi ya porojo hizo
Dunia nzima inajua covid ipo. Tanzania tulisema Covid hakuna kwetu na mazingira tunavyoishi mtaani kama ingekuwepo kweli kila siku tungekuwa tunazika watu .
Waje na porojo zao but swala la lockdown na chanjo hatutaki ..maana chanjo imekuwa ni biashara kubwa na inampaka madalali na nina imani hata watu wa tume madalali wameshawafata
Naona kuna mtu anataka kufungua duka saa 2 usk wakat wenzie wanakaribia kufunga biashara .
Mechi ya Corona inakaribia kuisha mtu ndo anataka kuingiza timu uwanjani kucheza mchezo ambao wenzie wanakaribia kuumaliza
Hivi hii tume inaweza kuwa I etumia sh ngapi hadi kukamilisha kazi yakeMatumizi mabaya ya kodi za wananchi tu taarifa gani watazitoa zaidi ya porojo tu hv watanzania wanaitaji tume kuja kuambiwa wavae barakoa,wanawe mikono na maji tiririka ,wakae social distance kweli? Maana hakuna jipya watakalokuja nalo zaidi ya porojo hizo
Dunia nzima inajua covid ipo. Tanzania tulisema Covid hakuna kwetu na mazingira tunavyoishi mtaani kama ingekuwepo kweli kila siku tungekuwa tunazika watu .
Waje na porojo zao but swala la lockdown na chanjo hatutaki ..maana chanjo imekuwa ni biashara kubwa na inampaka madalali na nina imani hata watu wa tume madalali wameshawafata
Naona kuna mtu anataka kufungua duka saa 2 usk wakat wenzie wanakaribia kufunga biashara .
Mechi ya Corona inakaribia kuisha mtu ndo anataka kuingiza timu uwanjani kucheza mchezo ambao wenzie wanakaribia kuumaliza.
Mzee ukisikia tume tena ya Rais jua kila kinachofanyika kinakuwa na status ya mwenye tume mwenyeweHivi hii tume inaweza kuwa I etumia sh ngapi hadi kukamilisha kazi yake
Kamati ya Corona imeishauri Serikali ya Tanzania;
1) Itangaze uwepo wa Corona
2) Iruhusu matumizi huru ya Chanjo sahihi za Corona
3) Ikubali maadhimio ya Kikanda na Kimataifa
4) Ipanue maktaba za kupima
5) Itoe takwimu sahihi za Corona
6) Tiba asili zitathiminiwe Kisayansi
View attachment 1788449
Rais Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Kamati Maalum aliyoiunda kwa ajili ya kufanya tathmini ya Ugonjwa wa Corona -COVID -19 nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Said Aboud
---
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU YATOKANAYO NA RIPOTI YA
KAMATI MAALUMU YA MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YAMUUNGANO WA TANZANIA YA KUFANYA TATHMINI YA UGONJWA
DAR ES SALAAM 17 MEI, 2021
WA COVID-19 NCHINI
Ndugu wanahabari, mtakumbuka kwamba kupitia hotuba ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
aliyoitoa tarehe 6 Aprili, 2021 wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam kuhusu kuunda Kamati ya kitaalamu ya kufanya tathimini ya ugonjwa wa COVID-19 na baadaye msisitizo alioutoa tarehe 22 Aprili,
2021 wakati akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma, naomba kuwajulisha kuwa Kamati hiyo imewasilisha rasmi ripoti yake kwa Mheshimiwa Rais leo tarehe 17 Mei, 2021.
Ndugu Wanahabari, Kamati ilifanyia kazi hadidu za rejea 12 zilizohusu maeneo mbalimbali ya tathmini ya mwenendo wa ugonjwa pamoja na afua za udhibiti wa COVID-19 ikiwemo chanjo hapa nchini, kikanda na kimataifa.
Ndugu Wanahabari, Tangu kuingia kwa ugonjwa wa COVID-19 nchini mwezi Machi 2020, Tanzania imekumbwa na mawimbi mawili makubwa na hivi sasa kutokana na mwenendo wa ugonjwa huo katika mataifa mengine duniani na kuna tishio la kutokea kwa wimbi la tatu hapa nchini.
Ndugu Wanahabari, Baada ya uchambuzi wa kina Kamati imependekeza yafuatayo:
1. Serikali ihuishe mipango ya dharura (Contigency and Response Plans) katika ngazi zote kwa ajili ya kukabiliana na majanga likiwemo janga la ugonjwa wa COVID-19.
2. Serikali itoe taarifa juu ya uwepo wa ugonjwa wa COVID-19 na ichukue hatua madhubuti kuimarisha hatua zote za afua za kinga
(interventions) katika ngazi zote ili kuepusha wimbi la tatu la ugonjwa huo.
3. Wataalamu wa afya watimize wajibu wao kitaalamu, kwa kuzingatia weledi, miiko na maadili katika kuelimisha, kukinga na kutibu ugonjwa wa COVID-19 nchini.
4. Tanzania ishiriki ipasavyo katika maamuzi na itekeleze maazimio ya kikanda na kimataifa iliyoridhia katika jumuiya za EAC, SADC, AU na WHO.
5. Kuhusu chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19:
a. Kamati inashauri Serikali kwa kutumia vyombo vyake iendelee na hatua kuelekea kuruhusu matumizi huru ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 kwa kutumia chanjo zilizoorodheshwa na Shirika la Afya Duniani ili kuwapa fursa ya kinga wananchi wake kwa kuwa kupitia uchambuzi wa Kamati, chanjo hizo zina ufanisi na usalama unaokubalika kisayansi;
b. Pamoja na mapendekezo haya, Kamati Huru ya Kitaifa ya Ushauri wa Chanjo (NITAG) na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) ziendelee kushirikishwa katika kutoa ushauri na kudhibiti chanjo hizo;
c. Kipaumbele cha utoaji wa chanjo dhidi ya COVID-19 nchini kwa kuanzia kiwe katika makundi yafuatayo kwa umuhimu:
i. Wahudumu katika vituo vya kutolea huduma za afya na watumishi walio katika mstari wa mbele wa utoaji wa huduma (frontline workers) mathalani watumishi sekta ya utalii, hoteli, mipakani, viongozi wa dini na mahujaji;ii. Wazee na watu wazima kuanzia umri wa miaka zaidi ya 50;iii. Watu wazima wenye maradhi sugu mengine (comorbidities) mathalani kisukari, shinikizo la damu, maradhi ya mfumo wa upumuaji, magonjwa ya figo n.k.;iv. Watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama; nav. Wasafiri wanaokwenda nje ya nchi.d. Kufanya uhamasishaji na maandalizi ya upokeaji, utunzaji, usafirishaji na utoaji wa chanjo na wananchi wawe huru kuamua kuchanja au la.
e. Serikali iratibu upatikanaji wa chanjo kwa watumishi wa taasisi za kimataifa walioko nchini.
6. Serikali ya Tanzania ijiunge na COVAX Facility kwa kuwasilisha andiko la kupatiwa chanjo, kwa kutumia fursa inayotolewa na GAVI.
7. Serikali itumie fursa zilizopo wakati huu wa janga la COVID-19 kuanza mchakato wa uanzishaji wa viwanda vya kutengeneza chanjo.
8. Serikali iimarishe huduma za uchunguzi kwa kuijengea uwezo Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii na maabara nyingine nchini ili kupanua wigo wa upimaji wa ugonjwa wa COVID-19.
9. Serikali ijenge uwezo wa ndani wa utambuzi wa virusi anuai vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 na magonjwa mengine ya kuambukiza.
10. Serikali itoe takwimu sahihi za ugonjwa wa COVID-19 kwa umma na Shirika la Afya Duniani ili wananchi wapate taarifa sahihi toka Mamlaka za Serikali na kuheshimu makubaliano na kanuni ambazo nchi iliridhia.
11. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ikamilishe mwongozo mpya wa matibabu ya ugonjwa wa COVID-19.
12. Serikali iendelee kuhakikisha kuwa matumizi ya tiba asili na tiba mbadala katika mfumo rasmi wa tiba za kisasa yanazingatia misingi ya kisayansi.
13. Serikali iendelee kutoa fursa na kuwawezesha wanasayansi kufanya tafiti kwa kufuata miiko, maadili na taratibu zilizowekwa ili kuimarisha kinga, tiba, uchunguzi wa ugonjwa wa COVID-19 na athari zake katika jamii nchini.
14. Serikali iendelee kuzingatia mazingira ya kitanzania katika udhibiti wa ugonjwa wa COVID-19 katika kuamua kuweka au kutokuweka shuruti ya kujifungia (lockdown) na kuwa na ubunifu ili kuruhusu ukuaji wa uchumi na kuimarisha sekta zinazochangia katika uchumi.
15. Wizara yenye dhamana ya fedha na uchumi ifanye tathmini ya kina ya athari za janga la COVID-19 na kuweka mpango madhubuti wa haraka wa sasa, wa muda wa kati na wa muda mrefu unaotekelezeka ili kukuza uchumi wa nchi.
16. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ziendelee kushirikiana ipasavyo katika hatua zote za kukabiliana na janga la COVID-19 pamoja na majanga mengineyo ikiwemo utoaji wa nyaraka za kimataifa kama vile Travel Advisory Note.
17. Idara ya Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu iendelee kutekeleza ipasavyo jukumu la uratibu na kutoa rasilimali husika wakati wa majanga ya kitaifa na kimataifa kama ugonjwa wa COVID-19 kwa kushirikisha ngazi na sekta zote.
18. Serikali ikamilishe malipo ya madeni ya watoa huduma na watumishi waliokuwa mstari wa mbele katika kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19 ili kuongeza ari na tija ya udhibiti wa ugonjwa huo.
19. Serikali iendelee kushirikisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, wadau wa maendeleo, sekta binafsi na vyombo vya habari katika mapambano dhidi ya janga la ugonjwa wa COVID-19.
Ndugu Wanahabari, Asanteni kwa kunisikiliza.
Nchi liendeshwa kienyeji sasa inarudi kwenye mstari mnyoofu.Kamati ya Corona imeishauri Serikali ya Tanzania;

Unaliwa ? Mwenda zake Yuko wap nguruwe weweNi upumbavu kupoteza Muda na hela Sababu ya vijimafua visivyoweza kuua hata kifaranga cha kuku.
Asante kwa hiyo ufafanuzi zaidiHofu ya nini? Sijaona jipya kwenye hiyo ripoti sana na mapya ni kutoa takwimu na kukubaliana kikanda na kimataifa. Suala la chanjo limewekwa huru , matumizi ta nyungu yafuate ushauri wa kisayansi. Sasa mbona kama hamsomi hayo mapendekezo mnaanza tu kulalamika? Watanzania nimewashindwa.
Mkuu nnachanjo nying kidg na kwa kuwa si mzawa wa 80s m niwa 70s Kama Ni mdogo hutajua... Bt chanjo zote kulikuwa na utafiti wa mda mrefu more than 5_15yrs...We umepigwa chanjo ngapi toka uko mdogo na uko hai mpaka leo? USA karibia nchi nzima wamepata chanjo,same hata UK na Mataifa yote ya ulaya. China, Russia na other big nations za Asia wame fanikiwa kutoa chanjo ya kutosha kwa watu wao. Huko kote wako kwenye mkakati wa kupunguza watu wao miaka michache ijayo kwa kutumia covid19 vaccine?
Mbowe ameshachanjwa fastaAfazali nitachomwa chanjo asante mama Samia Kwa kuniletea chanjo ya covid make mwenda zake aliiweka kiburi korona ikamuondoa fasta tu
Yeye na JPM ni kitu hichi... (1)Kamati ya Corona imeishauri Serikali ya Tanzania;
1) Itangaze uwepo wa Corona
2) Iruhusu matumizi huru ya Chanjo sahihi za Corona....
Nothing wrong actually, since chanjo zitakuwa huru atachoma aliye na mahitaji nayo ambaye hana mahitajio utatulia nyumbani kwake., na hivi ndivyo wenzetu wanavyoishi sisi tulikuwa tumelala usingizi wa ponooMkuu nnachanjo nying kidg na kwa kuwa si mzawa wa 80s m niwa 70s Kama Ni mdogo hutajua... Bt chanjo zote kulikuwa na utafiti wa mda mrefu more than 5_15yrs...