#COVID19 Kamati ya Kuchunguza Covid-19 iwe makini sana na hadidu rejea

Habari ya lock down hiyo hakuna, hayo mastory ya lock down ilikua ni kichaka cha mzee pombe kujificha tu ila hakuna mtu atakayeshauri eti nchi iwekekwe lock down.

Hatua za kisayansi ambazo lazima mfate bila kujali umataga wenu ni zile za kawaida kabisa na ikiwepo kupata chanjo ya korona na sio zile hatua za kienyeji mlizokua mnadanganyana na mzee pombe mpaka akaenda na maji kiutani-utani.
 
Nakusahihisha hapo. Ukiwapa foreigners report ya dawa zinavosaidia. Watakachofanya ni kuiga formula na ku apply kwao. Hivi kwa nn chochote anachotengeneza muafrika huwa ni bure kwa yeyote kukijua. Lakini mataifa mrngime yanaficha sana technology zao. Na yanazitumia kama advantage ya kibiashara. Ni lini na sisi tutajifunza kua wachoyo na wabinafsi ili kujinufaisha.
 
Afu Tatizo sio kufanya analysis kuhusu dawa. Tatizo ni kwamba je mna imani tena na wanaowapa dawa baada ya kudikia mambo yote ya agenda za kidunia na kadhalika. Je imani ipo?
 
Sio kwamba NIMR walikuwa hawafanyi tafiti za Covid-19, ishu ni kwamba haikuwa ikijulikana kama ambavyo mama kaona bora iwe wazi ili walimwengu watusome.

Na pia matokeo ya tafiti zao yawe wazi.
Matokeo ya tafiti ni siri. Ulisha ona mzungu anakupa tafiti yake ovyo. Hivi kwann tunapenda kugawa effort yetu bure bure. Why tusiwe wachoyo kama the rest of the world
 
Wanasayansi gani tulionao Tanzania wa kuwaamini hata ushauri wao uwe haupingiki tena.Angalia wanasayansi wakubwa huko magonjwa yalikoshika kasi hawana kauli moja na kila siku watu wanaandamana kupinga baadhi ya adha za corona.
 
Elewa kuwa mambo ya lockdown na visa vya corona sasa iko karibu kupindua nchi nyingi za Kiarabu. Uchumi wao umeporomoka sana kiasi kwamba raia wameanza kutokota kwa hasira.

Mfano mzuri ni kule Jordan yule mpuuzi ndugu yake mfalme Abdallah hana jipya na anatumiwa na maadui wa nje lakini amepata wafuasi kutokana na hali ya uchumi wa Jordan kuporomoka sana kutokana na kufungiwa ndani wasifanye kazi ilhali nchi yenyewe haina uwezo wa kuwalisha raia wake bure.
 
Hatuhitaji lockdown Tz bali tunahitaji hatua zingine za kisayansi ikiwepo chanjo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…