Pre GE2025 Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo lapendekeza Kuvunjwa kwa Mkataba wa Mkandarasi wa Mradi wa Umwagiliaji Mgongola

Pre GE2025 Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo lapendekeza Kuvunjwa kwa Mkataba wa Mkandarasi wa Mradi wa Umwagiliaji Mgongola

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo imependekeza Wizara ya Kilimo kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ivunje mkataba na Mkandarasi Badr East Africa Enterpries Limited ambaye anatakeleza ujenzi wa mradi wa Skimu ya Umwagiliaji Mgongola Wilayani Mvomero mkoani Morogoro.

Maamuzi ya Kamati hiyo inakuja baada ya taarifa ya Mhandisi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Mkoa wa Morogoro Matanga Juma kudai kuwa mkandarasi ameacha kuendelea na ujenzi akitaka kuongezewa fedha kutoka Bil 5.2 hadi Bil 12 nje na makubaliano ya mkataba ikiwa ni ongezeko la Bil.7.7

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa:
Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025


Anasema mradi ulianza mwaka September 2022 na ulitakiwa kukamilika Januari 2024 lakini hadi sasa umefikia asilimia 40 tu huku akigoma kuendelea na mradi huo kwa Madai fedha ni chache kwa sababu kifusi kinapatikana umbali wa kilometa 4 badala ya mita 200 ilivyopangwa awali.

 
Back
Top Bottom