Kamati ya Maadili ya Mawakili wa Tanganyika imekuwa jehanamu kwa mawakili

Kamati ya Maadili ya Mawakili wa Tanganyika imekuwa jehanamu kwa mawakili

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
15,835
Reaction score
23,776
Kamati ya maadili ya mawakili wa Tanganyika[Zanzibar hawahusiki] imekuwa sumu, mwiba, jehanamu kwa mawakili. Kamati badala ya kulinda, kutetea na kurekebisha mawakili yenyewe imekuwa kichaka cha kufuta, kufukuza na kusimamisha mawakili.

Mwabukusi ameipeleka mahakamani, Rutagatina aliwahi kuipeleka mahakamani.
Inaundwa na

(a) Jaji wa Mahakama Kuu atakayeteuliwa na Jaji Mkuu
(b) Mwanasheria Mkuu, Naibu Mwanasheria Mkuu au anayemwakiliasha
(c) Wakili anayeteuliwa na Counsel for Legal Education

Sakata la Fatma Karume kufungiwa, mara sijui kila mwaka wanafungiwa, wanashindwa kujifunza kwa mapolisi wanavyo lindana, nenda karipoti issue ya polii ama afisa ardhi uone.

Kamati ya Maadili ya mawakili imempa onyo, Wakili Boniface Mwabukusi kutokana na malalamiko yaliyotolewa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Eliezer Feleshi kwamba kuwa alitoa kauli za kichochezi, zisizo na staha na zisizozingatia taaluma ya uwakili.

Julai mwaka jana, Dk. Feleshi alipeleka shauri lake katika kamati hiyo akilalamika juu ya kauli alizozitoa Mwabukusi wakati akizungumza na vyombo vya habari.

Moja ya kauli iliyotajwa katika malalamiko hayo ni maneno ya Mwabukusi kwamba, “Spika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hawajui walichopitisha Bungeni kwamba hata Chifu Mangungo anasingiziwa maana yeye alijua ni Mkataba.
 
Waige hapo Kenya waache ujinga! Wanakuwa machawa TU!
Kenya ipi? Kenya ambayo IGP anapiga marufuku maandamano na Mahakama inaruhusu maana Katiba imeruhusu? Mbingu na kuzimu.
 
Mambo yenu tunawaachia wenyewe.
Nyie ndiyo kundi pekee mnalojiita wasomi lakini mmeshindwa kutatua kero zinazowahusu kwa kutumia usomi wenu.
Siku ukipotezwa, ukaokotwa pori la Muyowosi ndio utakumbuka hii kauli, Mawakili wanamteta Sativa bure, kwa fedha walizochanga wananchi walau wapate nauli, weka kiburi kama ndio unaanza kuota nywele za sehemu za siri.
 
Back
Top Bottom