Pre GE2025 Kamati ya miundombinu yaitaka Serikali kumsimamia mkandarasi ujenzi barabara ya Tanga-Pangani ili ikamilike wakati

Pre GE2025 Kamati ya miundombinu yaitaka Serikali kumsimamia mkandarasi ujenzi barabara ya Tanga-Pangani ili ikamilike wakati

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Serikali imehimizwa kumsimamia mkandarasi wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Tanga-Pangani ili kuhakikisha anamaliza kwa wakati. Katika mradi huo hatua ya kwanza (lot one) ya ujenzi wa barabara ya Afrika Mashariki, kipande cha kilomita 34 kilichosalia cha Tanga-Pangani, ambacho kwa mujibu wa mkataba kinapaswa kukamilika ifikapo Juni 16, mwaka huu.

Aidha, imeelezwa kuwa mkandarasi atakaposhindwa kumaliza mradi huo kwa wakati, atalazimika kuilipa Serikali fidia ya asilimia 0.01 kwa kila siku ya ucheleweshaji hadi mradi utakapo kamilika.

Pia soma Pre GE2025 Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze

Hayo yamebainishwa leo Ijumaa, Machi 14, 2025, wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ilipokagua mradi huu.

Katika ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati, Moshi Selemani Kakoso, ametaka kujua jinsi mkandarasi atakavyolipa fidia ikiwa atashindwa kumaliza mradi huo kwa wakati.

Mhandisi wa mradi wa Tanga-Pangani, Gladson Yohana, amethibitisha kuwa mkandarasi atakayeshindwa kumaliza mradi kwa wakati atalazimika kulipa penalti ya asilimia 0.01 kwa kila siku ya ucheleweshaji hadi mradi utakapo kamilika.
 
Back
Top Bottom