Kamati ya nidhamu ya TFF imempiga faini ya milion 5, Afisa habari wa Klabu ya Yanga Jerry Muro

mpira wa miguu hapa nchini ni majungu fitina kwenda mbele.
hivi tff ni kosa muro kupiga kelele kanuni ilivyokiukwa si mngempongeza muro kwa kufichua hujuma anazofanyiwa rais wa tff ama kweli ndio maana mnaitwa TANZANIA FITINA FEDARATION((TFF)
 
Rais mwenyewe majungu hata akipigwa majungu Sawa tu
 
Wanayanga nliwaulza kati ya Muro na Manara nani mropokaji hawajanjibu hadi leo. Jibu limetolewa na tff basi inatosha
Hata wenyewe tifutifu waropokaji pia, na tena wakurupukaji. Kanuni ya kumuombea kucheza mchezaji wenye kadi 3 za njano imeishia wapi!!!
Ama kwel nyani haoni kundule, kabla ya kupukutisha manoti kutoka kwa muro pia walipaswa watuambie aliyetia sahihi ya kuhalalisha kanuni ya mchezaji mwenye kadi 3 za njano kuchagua mechi ya kucheza yeye amepigwa faini ya sh. ngapi!!!!

Sijaliona la maana lililofanywa na tff ya malinzi zaidi tu ya kuvipiga vilabu faini za kufa mtu.
 
ivi kwani kuwa afisa habari wa timu lazima uwe mlopokaji maana naona kama wengi wao wako hivyo mfano wao huyu muro, haji manara na masau bwire yaani hao wote hapo naona kama akili zao sawa
 
Huyo angefungiwa tu maisha kutojishughulisha na soka, sehemu yoyote dunia hii.
 
Tatizo la huyu Dogo ni moja tu...ni namna anavyowasilishaga hoja zake,lkn ni mtu msema fact sana....kawapa FACT TFF ndo maana wamem'mind.
 
hivi jamani adhabu ya TFF Kwa msemaji wa Young Africans sports club ni sahihi? naomba kujua!
 
Makosa yapo na yataendelea kuwepo. Kwa nini wanaendekeza zaidi faini kubwa kubwa badala ya kumfungia mhusika kwa muda fulani kujihusisha na mpira? Inaelekea lengo lao kubwa si kurekebisha bali kukusanya fedha tu.

Kiasi hicho ni kikubwa mno. Kuna vilabu vinafanya mambo ya ajabu wanapigwa faini ya laki tatu.
 
Sasa tanzania fitina federation wanahamu ya kuunbulia mambo yao kama mimi muro silipi kwani wao nani
 
Habari iko kikanjanja sana.

Muro ndio nani? Kapewa adhabu gani? Lini? Ilikuwaje? Je wengine waliofanya kosa kama hilo walipewa adhabu gani?
By the way Muro ni jina la mabasi ya Mwanza
 
hivi jamani adhabu ya TFF Kwa msemaji wa Young Africans sports club ni sahihi? naomba kujua!

winmulu mbona unakurupuka kuandika vitu vya ajabu halafu unataka tujadili. Jerry Muro kafanya kosa gani? Lini? Kapewa adhabu gani? Lini?
 
Last edited by a moderator:

kweli kabisa mkuu lengo la tff sio kurekebisha bali kukusanya pesa, hebu rejea kadi 3 za ajibu.. lingekuwa ni kosa la kukusanya pesa tu na kesi kwisha wangefanya hivyo, lakini kwasababu kosa liliambatana na kupokonywa poiti 3 ndiyo maana kimya hadi leo.......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…