Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) kikaangoni

Joined
Jul 21, 2021
Posts
15
Reaction score
20
Mwishoni mwa 2021 wanaharakati wa A-Town walianzisha WhatsApp group iitwayo "MAPINDUZI YA RIADHA TANZANIA" group hilo limejaa vichwa vikali vyenye ujasiri mkubwa wa kuhoji na kuchalenji.

Pamoja na comments nyingi za hatari, nimeipenda hii hapa chini, nimeichomoa mle mle.

1) Viongozi wa TOC walishika hatamu tokea January 2002, that's 20 years

2) Kumekuwa na Olympics tano (5) kwa kipindi chao cha miaka 20

3) Mtoto aliyezaliwa January 2002 leo ana miaka 20 (ni mtu mzima)

4) Mtoto huyo atakuwa ni form six graduate anatafuta University sasa

5) Mtoto huyo ameshuhudia Tanzania ikiongozwa na Maraisi wanne (4) ambao ni Mkapa, Kikwete, Magufuli na Rais Samia Suluhu Hassan - TOC bado ni walewale

Nikisema viongozi wa TOC ni madikteta mtanipeleka mahakamani? (Jamaa huyo kahoji hivyo).

Pia inasemekana tangu 2001 hadi 2020 Kamati ya Olimpiki ya Dunia (IOC) imeigawia TOC ruzuku zaidi ya Tsh: bilioni 5.4 na kwamba Tanzania hatujaambulia medali hata moja.

Katika group hilo wanaharakati wamempongeza Waziri Mchengerwa kwa kuanza vizuri, ila wakaweka tahadhari kwamba isije kuwa ni nguvu ya Pepsi-Cola.
 
W
Mnampongeza au wanajipendekeza, WAZIRI ameingia Juzi tu, wameanza kumsifia?
 
Dollari
 
Toka wameingia madarakani wameleta medali ngapi za mashindano ya olimpiki?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…