Kamati ya PIC: Tunaelekeza Wanaohujumu Mradi wa SGR wachukuliwe hatua kali za kisheria

Kamati ya PIC: Tunaelekeza Wanaohujumu Mradi wa SGR wachukuliwe hatua kali za kisheria

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imeelekeza Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuendelea kuweka teknolojia za ulinzi ili kuthibiti uhalifu kwenye mradi wa Reli ya SGR huku ikisisitiza hatua kali za kisheria kuchukuliwa kwa wanaobainika kuhusika na vitendo vya kuhujumu mradi huo.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kamati ya PIC, Vuma Augustino wakati akizungumza baada ya Kamati kupokea Ripoti ya Utendaji Kazi wa Shirika hilo hususani mradi huo wa SGR, Novemba 14, 2024 Jijini Dar es Salaam, ambapo amesema tayari wamewaelekeza TRC kuongeza teknolojia za ulinzi ili kuthibiti matukio ya uharifu kwenye miundombinu ya SGR.

Aidha, amesema kuwa wamepokea taarifa kwamba kufikia Februari 2025 mabehewa ya SGR ya mizigo yataanza rasmi kusafirisha mizigo, ambapo amesema kwamba hatua hiyo itasaidia kuongeza mapato zaidi.

"Serikali kupitia TRC tunategemea itaendelea kukusanya kiasi kingine kikubwa cha mapato kupitia mradi huo, hasa baada ya kuanza kwa huduma ya Usafirishaji mizigo mapema mwakani," amesema Vuma.

Itakumbukwa hivi karibuni Mkurugenzi Mtendaji wa TRC, Masanja Kadogosa alidai kuwa kuna watu ambao wanahujumu SGR.

Kauli hiyo iliibua mjadala mseto hususani kwenye mitandao ya kijamii na kwenye vyombo vya habari.

Pia soma:
~
Ukitaka kukata tiketi SGR unaambiwa treni imejaa, muda wa kuondoka treni inakuwa wazi
~ Hujuma Kubwa SGR: Inagoma kukata tiketi
~ Picha: Hujuma nzito katika miundombinu ya reli ya SGR
 
Back
Top Bottom