Pre GE2025 Kamati ya Siasa Mkoa wa Kilimanjaro imeridhishwa na utekelezaji wa mradi wa maji unaosimamiwa na MUWSA

Pre GE2025 Kamati ya Siasa Mkoa wa Kilimanjaro imeridhishwa na utekelezaji wa mradi wa maji unaosimamiwa na MUWSA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
Kamati ya Siasa Mkoa wa Kilimanjaro imeridhishwa na utekelezaji wa mradi wa maji unaosimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Moshi MUWSA

Mradi huo unaogharimu Tshs; Milioni 787 unalenga kuhudumia wananchi zaidi ya 10,500 walioko kwenye Kata ya Marangu Mashariki.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Mhandisi Innocent Lugodisha ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji maji na Usafi wa mazingira ameihakikishia Serikali mradi huo kukamilika mapema ili wananchi waweze kupata huduma hiyo ya majisafi na salama.

Pia soma: Pre GE2025 - Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mkuu wa Wilaya ya Moshi Ndugu Geofrey Mnzava amepongeza na kuishukuru namna Mamlaka hiyo ilivyoweza kutekeleza mradi huo kupitia mapato ya ndani

Ndugu Selemani Mfinanga ambaye ni Mwenezi Mkoa wa Kilimanjaro amefurahishwa na namna Usimamizi mzuri wa Fedha za Serikali unavyotatua changamoto za wananchi.

Ziara hiyo iliambatana na viongozi mbalimbali akiwemo Mhe. Dkt. Charles Kimei Mbunge wa Jimbo na viongozi mbalimbali wa Chama, Serikali na Dini.
 
Back
Top Bottom