‘Kamati ya ufundi’ ilizuia Simba kuvaa jezi Nyeupe Shinyanga

PROSPER 05

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2013
Posts
226
Reaction score
217
Baada ya Stand United na Simba kuvaa jezi zinazolalamikiwa kufanana wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa jana Jumapili, October 1, 2017 kwenye uwanja wa Kambarage, ShaffihDauda.co.tz imefanya utafiti kwa nini timu hizo ziliruhusiwa kucheza huku jezi zao zikiwa zinafanana kwa rangi.

Taarifa ambazo ShaffihDauda.co.tz imezipata kutoka vyanzo tofauti ni kwamba, Simba hawakuwa tayari kuvaa jezi zao za ugenini (nyeupe) kutokana na maagizo ya ‘kamati ya ufundi’. Ikabidi kamishna wa mchezo akubali Simba watumie jezi nyekundu kwa sababu jezi za Stand United ni rangi ya machungwa wakiamini zisingewasumbua waamuzi.
 
Walihalibu sana muonekano wa uwanjani. Sisi ambao macho yetu yamefifia kwa sababu ya uhenga tulipata taabu sana kutofautisha kati ya wachezaji wa Simba na wa Stendi.
Wachezaji wote walionekana kama wamevaa jezi moja ya pinki. Kumjua mchezaji mpaka umwone anapenda na mpira upande wa timu pinzani, ni vigumu kujua nani beki na nani ni mshambuliaji.
Sisi wahenga hatukuufurahia mpira kabisa.
Hizi imani nyingine hizi hazina tija kwa maendeleo ya soka.
 
Acheni upuuzi mbona mwaka jana walivaa hivyo hivyo Uwanja wa Taifa?
 
Simba wanaamini sana ushirikina! Kuna wakati tuliambiwa kuna mafuvu yamefukuliwa uwanja wa taifa, sasa naamini simba ndio waliyafukia! Chezeni mpira si mmesajili kwa hela ndefu
 
Simba wanaamini sana ushirikina! Kuna wakati tuliambiwa kuna mafuvu yamefukuliwa uwanja wa taifa, sasa naamini simba ndio waliyafukia! Chezeni mpira si mmesajili kwa hela ndefu
POROJO
 
Je si kosa kuvaa jezi za nyumbani katika mechi za ugenini
 
Shafii Dauda nibLimbukeni na Mshamba
 
Simba wangevaa jezi zao nyeupe za ugenini wachezaji wangeonekana vizuri sana.
Naomba siku nyingine wafanye hivyo wanapoona jezi zao zinafanana na timu pinzani.
 
Chama la washirikina wakubwa Tanzania ni matopeni. Shafii ni Simba damu lakini imebidi aseme ukweli wake.
Timu inatii zaidi maagizo ya masangoma kuliko Kocha
 
Inasikitisha sana kwa Timu kubwa sana kama Simba kugoma kuvaa jezi Nyeupe za ugenini na kukomaa na hizo nyekundu zao...Kwa hali hii mpira wa TZ kusonga mbele bado sana..

Kamati ya ufundi wa kijinga hiyo
 
Simba wanaamini sana ushirikina! Kuna wakati tuliambiwa kuna mafuvu yamefukuliwa uwanja wa taifa, sasa naamini simba ndio waliyafukia! Chezeni mpira si mmesajili kwa hela ndefu
Kayafukue utuonyeshe, kwani shida ipo wapi?
 
Uyu shafih anawashwa washwa sana akiambiwa atoe ushaidi anaweza? Ambane na Boss wake anayelilia mbunye aache Simba ifanye yake
 
Tff ndo wenye uamuz wa jezi gani zitumike wakati wa pre match meeting na sio simba fc
 
Nakumubuka mechi ya simba vs stand msimu uliopita uwanja wa taifa stand alivaa rangi ya machungwa na simba nyekundu mbona hakukuwa na zengwe?Au Shaffi uliingia na matokeo yako mfukoni kwa upande wa simba?
 
Na wakikosa kombe tena msimu huu wasianze kwenda FIFA/Kamati ya masaa 72 kumtafuta aliewaroga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…