Pre GE2025 Kamati yapitisha shauri la Jimbo la Missenyi kubadilishwa jina na kuwa Jimbo la Nkenge ili kuleta "muunganiko" wa kiutawala

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Kamati ya Ushauri ya Wilaya Missenyi mkoani Kagera (DCC), imepitisha azimio la kubadili jina la Jimbo la Uchaguzi la Nkenge na kuitwa Jimbo la Missenyi, ili kuleta muunganiko wa kiutawala.

Kikao cha kamati hiyo kilichofanyika jana, Jumanne, Machi 11, 2025 kilichoongozwa na Mkuu wa Wilaya Missenyi, Kanali mstaafu Hamis Maiga, kwa kauli moja ya wajumbe kiliazimia mabadiliko hayo ya jina.

Akisoma mapendekezo ya kubadili jina hilo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Missenyi Ofisa Utawala Catherine Peter alitaja sababu mbalimbali za kubadili jina kuwa ni kutokuwepo na mfanano wa jina la Wilaya na Jimbo la Uchaguzi.

Alisema sababu hiyo imekuwa ikifanya jina hilo la Nkenge kutokufahamika na kutokutumika sana katika nyaraka mbalimbali za kiserikali na za kimaamuzi tofauti na bungeni.

jimbo la .png

Kadhalika alisema jina la Nkenge, linatumika kwenye Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) na uwakilishi wa Mbunge Bungeni hivyo kutumika kwa Mhimili mmoja wa Dola wa Bunge pekee na kuacha mihimili mingine ya miwili ya Mahakama na serikali ikitumia jina la Missenyi.

Aidha alisema uamuzi huo unakuja kufuatia taarifa rasmi ya INEC kwa umma pamoja na barua ya maelekezo katika Halmashauri hiyo Februari 26, 2025, iliyoelekeza kupitiwa upya kwa majimbo na kuyagawa au kubadili majina ya majimbo ya uchaguzi ya Tanzania Bara.

Source: Nipashe
 
Kichwa na kiwiliwili cha post yako havina ushirikiano!
 
Pumbavu, is this what Wahaya need as a priority?
 
Back
Top Bottom