Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mjumbe Wa Mkutano Mkuu Wa Wazazi CCM Taifa Ndugu Mrisho Kamba amesema Chama Cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA ) kinajaribu kueneza na kupandikiza chuki kati ya vijana na wazee kwa maslahi yao binafsi. “CCM ni chama kinachoamini katika mshikamano wa vizazi vyote”- Mrisho Kamba amesema maneno hayo Leo Januari 29 2025
“Nimeyasikia maneno yaliyotolewa na viongozi wakuu wa CHADEMA wakimkosoa Makamu Mwenyekiti wetu, Mzee Stephen Wasira, kwa madai kwamba ni mzee na hana mawazo mapya kwa jamii ya sasa. Kauli hii si tu kwamba ni ya dharau, bali pia inaonesha namna gani CHADEMA wamefilisika kisiasa na hawana hoja za msingi za kuzungumza na Watanzania”
“Kwanza, nataka kuwaambia Watanzania kuwa Mzee Wasira ni mmoja wa viongozi waliotoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi yetu. Uzoefu wake, hekima yake na mchango wake ndani ya chama na serikali vimeleta mabadiliko makubwa katika sekta mbalimbali. Leo hii tunapozungumza kuhusu maendeleo ya Tanzania, hatuwezi kupuuza mchango wa viongozi waliotangulia, akiwemo Mzee Wasira”
“CHADEMA wanadhani siasa ni umri. Hapana! Siasa ni uwezo wa kuongoza, ni maarifa, ni uzoefu, na ni mchango wa mtu kwa jamii. Kama wao wanabeza wazee, basi wanapaswa kwanza waangalie ndani ya chama chao—Mbowe si kijana, Lissu naye ana umri wa wastani. Kama umri ni tatizo, basi na wao waanze kwa kuwaondoa viongozi wao wakongwe”
“Huu ni uthibitisho mwingine kuwa CHADEMA wanajaribu kupandikiza chuki kati ya vijana na wazee kwa maslahi yao binafsi. CCM ni chama kinachoamini katika mshikamano wa vizazi vyote. Tunathamini hekima za wazee na tunathamini nguvu za vijana. Huu ndio msingi wa maendeleo ya kweli.” Alisema Mrisho Hassan Kamba
Nawaambia Watanzania, hasa vijana, kuwa msidanganywe na siasa za kubeza watu kwa misingi ya umri. Leo wanamshambulia Mzee Wasira, kesho watamshambulia nani? Taifa linajengwa kwa maarifa na uzoefu wa waliotutangulia pamoja na ubunifu wa kizazi cha sasa. CCM itaendelea kuheshimu na kuthamini viongozi wake wote, bila kujali umri wao, kwa sababu tunajua thamani yao kwa taifa letu