Kambaya wa ITV na Radio One anautamani ukuu wa Wilaya?

Kambaya wa ITV na Radio One anautamani ukuu wa Wilaya?

MUTUYAMUNGU

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2014
Posts
1,825
Reaction score
4,374
Nimemsikia bila aibu asubuhi hii akiwa Radio One akitetea mabasi yote yaanzie Mbezi/ Magufuli bus terminal bila kujali mateso wanayopata abiria wa mbali.

Hivi Kambaya basi likianzia Kigamboni na abiria 10 likapitia Mbezi stendi likajaza abiria na kulipa ushuru wa stendi kisha likaendelea na safari kuna ubaya?

Hivi Kambaya basi limetoka Mbeya ila wana yard Tandika likishusha abiria Mbezi stendi kisha wanaobaki wakaenda kushukia Tandika kuna ubaya?

Kambaya umewahi kusafiri na mizigo pamoja na watoto wadogo?

Kambaya vipi kuhusu abiria wa Bunju na mabasi yanayopita Bagamoyo Road?

Tukutane baadaye ITV kwenye kipima joto na ole wako unikatishe kuongea au uninyang'anye mic!
 
Naunga mkono ushauri wa Kambaya. Kila mtu akitaka ajashushiwe kwao itakuwa ni vurugu.

Serikali hebu simamieni mnachokiamini acheni kushikwa masharubu na Hawa wavunja sheria na utaratibu.

Serikali inagomewa na watu!!! Serikali?!!!
 
Ugumu wa hili unatokana na nini? Nini kiko nyumba ya kuwalazimisha abiria kushukia magufuli stendi? Kwanini iwe lazima wabiria wote kushushiwa hapo wakati kwa mlengo wa kibiashara wenye mabasi waliona ni vyema kuwatengenezea abiria wao urahisi wa kusafiri kwa kuwawekea vituo vidogo vya mabasi huko karibu na city center au pembezoni mwa miji, uharamu wa vituo binafsi vya mabasi ni upi hasa ikiwa kila basi ni lazima lipite stendi kuu zote za mikoa na lazima zilipie ada?

Ugumu wa hiki ninini? Ninyi viongozi wetu ni masadist? ni lazima mtese wananchi ili msikie furaha? Ni wazi shuleni mlienda kusomea ujinga kama hamuwezi kusolve matatizo madogo kama haya.

Kama stendi ya Magufuli inagenerate income ndogo, kuwalazimisha aibiria wote washushwe hapo hakutaweza kuongeza mapato kwa namna mnavyofikiri.
 
Umenena vyema ndugu yangu. Mfano ile stendi ya Shekilango kama shida ni ushuru si wakusanye tu kuliko kutesa abiria?

RC Makala amedhalilisha sana watu waliosoma IFM. Yeye ni msomi wa IFM hivi hata akili za kujua tu jiografia ya jiji LA Dar hana?
 
Litoke tamko moja watu watulie kila kitu kinawezekana
 
Lengo la daladala Ni kutatua kero za Safari ndogondogo mjini,
Lengo la daladala si kuleta kero za Safari ili zitatue!
safari ndogo ndogo ni bajaji na bodaboda. Daladal kazi yake ni kuwatoa watu pembezoni mwa mji na kuwapeleka katikati ya jijii.
 
Back
Top Bottom