(Kambi Ya Kimataifa kwa Vijana) Tanzania International Youth Camp

(Kambi Ya Kimataifa kwa Vijana) Tanzania International Youth Camp

Mvumbagu

Member
Joined
Nov 30, 2013
Posts
38
Reaction score
9

Kwa vijana wa chuo, wapenda maendeleo Umri kati ya miaka 18-40, Kambi maalum ya kimataifa kwa vijana inatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 3-17, Agosti, 2014 na nyingine 31,Agosti- 13,September,2014. (Kwa muda wa wiki Mbili Kila moja.)
MAHALI: ILONGA YOUTH CENTRE, KILOSA-Morogoro,Tanzania

Jifunze, Shiriki, Jumuika, na Badili Fikra.

INTERNATIONAL YOUTH WORK CAMPS AND EXCHANGE PROGRAM
CONDUCTED BY WATOTO WETU TANZANIA IN COLLABORATION WITH
MINISTRY OF INFORMATION, YOUTH, CULTURE AND SPORTS

PROGRAMS;

ENVIRONMENTAL ISSUES
BUSINESS PLAN WRITING
RESEARCH AND REPORT WRITING SKILLS
HUMAN RIGHTS ADVOCACY
GOOD GOVERNANCE & LEADERSHIP SKILLS.
ENTREPRENEURSHIP SKILLS
HEALTH CARE AND LIFE SKILLS
VOLUNTEERISM PROGRAM
INTERVIEW SKILLS

+ TOUR DURING THE WORK CAMP TO (E.g MIKUMI NATIONAL PARK, ULUGURU MOUNTAINS, WATER FALLS AND OTHER TOURISTS AREAS to Promote National Tourism Sector).

Unaweza kutuma maombi yako sasa, Kwa Maulizo na Taarifa zaidi
Wasiliana nasi moja kwa moja.

Barua pepe: wwtyouthexchange@gmail.com
Simu/ Whatsapp: 0716 979 939/ +255 712 439 124/ 0756 438 070
Landline: 023 262 3036
Twitter: @IycepTanzania
 
Imani inakuwa ndogo sana, juzi kati tuliitwa kwenye kongamano la vijana diamond jubilee, kufika tunakuta ni kongamano la umoja wa vijana wa ccm,baadaye ilibidi lirudiwe ili kufukia aibu.
 
Imani inakuwa ndogo sana, juzi kati tuliitwa kwenye kongamano la vijana diamond jubilee, kufika tunakuta ni kongamano la umoja wa vijana wa ccm,baadaye ilibidi lirudiwe ili kufukia aibu.

Capt Tamar..Kambi hii haipo kisiasa na wala haifungamani na masuala ya kisiasa ya upande wowote kiujumla. Hii imeandaliwa maalum kwa ajili ya kuwawezesha vijana kupata elimu na ujuzi zaidi (Capacity Building) wanayoweza kuitumia kwa masuala yao ya maendeleo baada ya chuo, kazini, ama kipindi akijipanga anapokuwa mtaani. Mbali na yote kukutana na wadau mbalimbali na vijana wenzake ili kubadilishana fikra na kujiendeleza zaidi katika uthubutu.
 
Habari,

Karibu Iycep Tanzania.

Ufuatao ni utaratibu wa maombi na vigezo vya washiriki.

Program hii ni kwa vijana wa jinsia zote (wasichana & Wavulana) kati ya umri wa miaka 18-40 kuanzia wahitimu wa kidato cha nne hadi elimu ya juu.

Ada ya program: 50,000/- Tshs. ( Chakula, malazi, mafunzo, cheti + Tour)

Number of participant per camp: 50 Participants

Utaratibu wa kutuma maombi:

- Lipia Ada ya program katika Benki ya NBC Account Number 011103025145 Branch: Corporate Branch,

- Scan bank payment slip ( Risiti ya malipo)kisha uitume kwa. Email: wwtyouthexchange@gmail.com au Whatsapp: 0716979939

- Utapokea namba ya ushiriki wa kambi pamoja na fomu ya maelezo ya kambi na maelezo ya ziada kukusaidia kufika kambini ( Ilonga Youth Centre)

-Mshiriki atatakiwa kujigharamia nauli ya kwenda na kurudi Kambini( Kutoka mkoa atokao)Mshiriki anaweza kuuliza Taarifa za gharama za nauli mapema kutoka kwa Iycep Tanzania, kulingana na mkoa anaotoka.

-Wakati wa kuripoti kambini, Mshiriki anaombwa kuleta risiti ya malipo ya benki (pay slip) kwa ajili ya kupewa risiti na kuthibitisha uhalali wa ushiriki wake.

Mwisho wa kutuma maombi wa ushiriki kwa camp I ni tar. 31st, July,2014.
Na kwa Camp II ni tar. 25th, August, 2014

Shukran.
Mohammed A. Mvumbagu
Coordinator
Iycep Tanzania.
View attachment 170367
 
Me nina uzoefu na haya Matamasha,haki ya Mungu Mikono ya wanasiasa hapa Upo,na Wanasiasa ndo influencial mkubwa hapa,Mwisho wa tamasha hili viongozi walioandaa wanatafuta fursa kwa wanasiasa,Lengo lenu ni zuri ila tatizo mnatumiwa nyie hamjitambui ila mnawafanya wenzenu kama greda au mgongo wa kufikia malengo yenu,Kijana anaejitambua hawezi kuja hapo
 
Ndugu Marangu,
Pole kwa Experience uliyopitia ambayo mara zote ilikuwa ikikutumbukiza huko kwa bahati mbaya ama Makusudi maalum.

Promising you, Kama Cordinator wa Iycep Tanzania. Hakuna Political Influence yoyote katika Program hii, nia na malengo makuu ni Kuzidi ku empower vijana kutoka katika Opportunity rasmi zinazojulikana, kuwapatia vijana experience, kushare skills, kuconnect na stake holders na kutengeneza fursa za kiuchumi na maendeleo ya jamii kwa vijana na maendeleo ya jamii kama Community Development Partners na si Politicians.
Please angalia kama katika Program zinazoainishwa kuendeshwa katika program hii kama kuna Theme au Topic yoyote inayoweza kuwa na tija ya kisiasa from your view then please Point it out.
 
Nimejiandaa kuchangia ila kutokana na michango ya baadhi ya wadau hapa hasa mkuu Marangu itanifanya nisite kidogo!!
 
we unahisi ni kwa nini vijana tukutane. kwa nini usitumie jamii forum kufikisha hayo unayotaka kuwaeleza vijana . unanifanya nipate mashaka sana na hizi kambi zenu maana nahisi zimekaa kibiashara zaidi. kama kweli una nia ya dhati na vijana wa kitanzania omba nafasi hapa then waelezee yale unayoi
taka kuwaeleza. na kuna mwenzio anaandaa pale mliman city nadhan ni mchina ,sasaq sijui china hakuna vijana hadi waje tanzania
 
@ Nyanyado, Una uhuru wa kutoa maoni na tunayaheshimu mawazo yako, ni ya msingi.
Jamii Forum ni sehemu tu ya Publicity na kujuzana kuhusu event, Kama pia tulivyo chapisha Vipeperushi, na soon Matangazo kwenye TV stations na Radio.

unadhani ni vijana wangapi hawana access na mtandao au Matumizi na Computer na wangependa pia kushiriki?,
Utawezaje kufanyia kazi ( Group work) wakati wa mafunzo, Utafanya vipi active presentations, Field work (Volunteering -katika jamii.) sambamba na mengine yanayohitaji active participation (Practically) kama tukiamua kutumia Mtandao kuendeshea Mafunzo, Utawezaje kujifunza physically kutoka kwa wengine nk.

Tafadhali Re-think about it, nadhani utaelewa kuwa this is not business but service kutimiza Mpango wa kimataifa wa kuwawezesha vijana kujitambua, kujiendeleza, kujiongoza na kujitegemea bila kutetereka katika maisha. It's all about Capacity building, experience, Inspiration and Life lesson.
Karibu kuuliza zaidi ili kuondoa Doubts ulizonazo.
13.png 1011932_10200697536414121_659062733_n.jpg 292801_10151026333040044_2117819136_n.jpg 16.png
Caption: Picha zinazo onyesha baadhi ya matukio wakati wa Kambi ya Kimataifa ya Vijana IYCEP Tanzania 2013
 
View attachment 171303 View attachment 171304 View attachment 171305 View attachment 171306
Caption: Picha zinazo onyesha baadhi ya matukio wakati wa Kambi ya Kimataifa ya Vijana IYCEP Tanzania 2013

nashukuru kwa kujitahidi kujaribu kunishawishi,
kuhusu suala la uhakika wa media ,nadhani hata wewe kuna kundi flani la watu umelikusudia .

Kambi ya Kimataifa ya Vijana IYCEP Tanzania 2013 nini yalikuwa matokeo yake? ambayo hadi sasa mnajivunia.

kuhusu suala la ushoga mna mtazamo gani?
 
hivi hii wizara ya information youth culture and sports inaongozwa na nani?
 
Waziri Dk. Fenella Mukangara na naibu wake ni Juma nkamia,upo hapo?utakuwepo kwenye kambi?
 
IYCEP Tanzania 2013 ilikuwa ikisimamiwa na Watoto Wetu Tanzania Organization kwa kushirkiana na Washirika mbalimbali wa kimataifa kabla ya Kuishirikisha serikali ambayo imeingia kupitia kituo cha vijana Ilonga 2014.

Baadhi ya Ambavyo ICYEP Inaweza kujivunia kutokana na matunda ya program hii ni kuwezesha vijana na jamii katika:

-Kuinua Ushiriki wa wasichana katika Uongozi from the grassroots, Created Oportunities kwa vijana katika kujitambua na kimaendeleo kupitia ujasiriamali.
-Kufanikiwa kuweza kutumia michezo kama nyenzo ya Kufundishia Uongozi, na Elimu ya Afya kwa vijana.
-Kupeleka vijana kushirki katika harakati za kimaendeleo za kujitolea na kwenye program mbalimbali ndani na nje ya nchi.
-Kushirkiana na Baadhi ya vituo vya Afya ya Uzazi na vijana katika kuendeleza elimu ya Afya kwa kijana.
-Kuwawezesha vijana wenyewe kuwa wawezeshaji wakuu wa masuala ya afya ya uzazi, Usafirishwaji haramu wa binadamu, Uongozi, Haki za Mtoto na Binadamu na Elimu ya Ujasiriamali Nk.

Kuhusu Suala la Ushoga hatuna support nalo, Tunafanya kazi kwa kuheshimu misingi yote ya kiimani, Tamaduni na Desturi ya kitanzania bila kuathiriwa na upepo kutoka utamaduni wa nje.

Haya yote na mengine zaidi yatazungumzwa kwa kina katika Taarifa ya Camp na Washirika kwenye vipindi maalum kuhusu kambi na way forward. I think It's enough for now, Stay tuned!
 
IYCEP Tanzania 2014 Camp Updates:

Tunatangaza kufunga rasmi awamu ya kwanza Usahili wa washiriki wa kambi ya kwanza kutokana na kujaa kwa nafasi zilizotolewa hadi Tarehe 13,August,2014 Tutakapofungua tena kupokea maombi kwa ajili ya Camp II.

( Kambi ya pili itafanyika Tarehe, 31,August- 13,September,2014)

Tunashukuru na kutoa pongezi kwa Vijana na Wadau wote waliojiandikisha kwa IYCEP Tanzania Camp I August, 3- 17, 2014.

Kaa tayari kupokea International Youth Day 2014 Challenge Pack ( Theme: ‪#‎Mental‬ Health Matters) kwa ajili ya Shule,Kikundi au Jamii yako.

Taarifa za ziadakwa washiriki wa kambi ya kwanza zitatolewa kwa mawasiliano ya washiriki, (Barua Pepe, na Simu).
**Tafadhali tujulishe endapo kuna mabadiliko yoyote ya mawasiliano utakayoyafanya kabla ya Tarehe 25, July,2014.12.png
https://www.facebook.com/IycepTanzania
 
Hapa hamna kitu,nani asiyejua kwamba mnatumwa na wanasiasa kukusanya mtaji wa watu hasa vijana?acheni hayo kuwa vibaraka vya wanasiasa ili waweze kutumia mtaji huo 2015,nyie si ndo mliokuwa na sumaye juzi mpaka kwenye gazeti ya Mwananchi picha yenu ipo,hizi issue me nazifaham sana au Unataka niweke majina ya vigogo waliowatuma kufanya kazi hii?
 
Kwa hesabu ya haraka sh. 50,000/= kwa wiki 2 ni wastani wa sh. 3571.4 kwa siku itakayogharamia malazi, chakula, tours na kuna vyeti na nimecheki hapo programmes ni nyingi kwa kweli. Naomba kama nitasaidiwa maelezo ya kutosha kama kuna wadhamini wengine wanaosapoti hii kitu kwa sababu ni moja ya vitu napenda lakini naona kama sielewi hv. Naomba mchanganuo namna wiki 2 zitakavoisha kwa mafanikio kwa gharama hiyo. Nawasilisha.
 
Mie ni mfuatiliaji sana wa hii kitu, ngoja nisubiri kwanza mrejesho kwa wale watakaohudhuria camp I, then nami nitaamua au kutoamua kuhudhuria hiyo camp II.
 
Back
Top Bottom