Kambi ya madaktari bingwa bobezi yaanza hospitali ya Wilaya ya Bukoba iliyopo tarafani Katerero

Kambi ya madaktari bingwa bobezi yaanza hospitali ya Wilaya ya Bukoba iliyopo tarafani Katerero

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
📌 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bukoba Vijijini Ndugu Fatina Hussein Laay awakaribisha wananchi wote. Kambi ya Siku 5 mfululizo yaanza leo Jumatatu Hospitali ya Wilaya- Bujunangoma kutoa huduma mbalimbali za Kibingwa Bobezi, Wananchi waitikia wito na wote mnakaribishwa.

Huduma za Kibingwa ambazo zamani zilikua zinapatikana kwenye Hospitali za Rufaa, za Mikoa na Taifani pale Muhimbili, sasa miaka mitatu ya Rais Samia Suluhu Hassan huduma hizi amezisogeza zaidi kwa wananchi kwenye maeneo yao ili kupata huduma hiyo ambayo zamani walikua wanasafiri umbali mrefu kwenda mkoani au Taifa.

Sasa kuanzia leo Jumatatu Juni 17 hadi Juni 21, 2024 Kambi ya Siku 5 ya Huduma za Kibingwa Bobezi zinazotolewa kwenye Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba iliyopo Bujunangoma kwenye Tarafa ya Katerero na wananchi mbalimbali wameanza kuitikia wito kwa siku ya kwanza ya leo Jumatatu.

Madaktari Bingwa watakaokuwepo ni Waliobobea Watoto na Watoto wachanga, Madaktari Bingwa wa Wanawake na Ukunga, wa Upasuaji wa Mfumo wa Mkojo, wa Magonjwa ya ndani na wa usingizi na ganzi, ENT (matatizo ya nasal polyps, n.k, uvimbe wa tumboni, hernia na screening ya cancer ya matiti kwa wanawake na wanaume.

Wananchi wote mnakaribishwa kuja kufaidi fursa hii adhimu iliyotolewa na Rais Samia kwa kuwajali wananchi wake na kuwasogezea huduma hizi za Kibingwa karibu yao.

IMG-20240614-WA0057.jpg
 

Attachments

  • IMG-20240617-WA0016.jpg
    IMG-20240617-WA0016.jpg
    483.6 KB · Views: 4
Back
Top Bottom