Kambi ya siku 8 Misri kwa Taifa stars ni ufujaji wa pesa

ubuntuX

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2014
Posts
1,977
Reaction score
2,200
wakuu

hapo jana timu ya taifa, Taifa stars ilikwea pipa na kuelekea nchini Misri kwaajili ya maandalizi dhidi ya Letheto
mechi itakayochezwa Jijin Dar es salaam kuwania kufuzu AFCON 2019

kiukweli kwa jinsi timu yetu ilivyo kichwa cha mwendawazimu, kuipeleka Egypt kwa pesa za watanzania ni ufujaji wa pesa na matumizi yasiyolazima!

kwani tanzania yote hii ilivyokubwa haina sehemu tulivu kwaajili ya kambi waweze kutulia na kujiandaa vema?

nipende kuwaambia TFF kuwa uwendawazimu wa Taifa stars hauwezi ondokana na kuweka kambi ya gharama kubwa nje ya nchi, zaidi timu inahitaji hali kimchezo

wakae hapa hapa Tanzania kuna maeneo murua kabisa kama vile Zanzibar nk
huko mmewapeleka gharama za hotel, chakula na usafiri nje ya nchi kwa kikosi cha zaidi ya watu 20 sio matumiz sahihi

then badae mtaanza kupitisha bakuli

au mnajitanua na chenji zilizobakizwa na Serengeti boys?
Kwa sasa nguvu yetu watanzania tuwekeze katika soka la vijana, hii taifa stars haitufikushi popote zaidi ya kutuongezea pressure tu
 
Kwanza TIMU kama lesotho ILIVYOKUWA YA HOVYO.......ni timu ya kuiendea MISRI? wote huo ni upigaji pesa tu...wakirudi watatwambiya wametumia dola 300000... UPUUZI MTUPU..mambo haya ya kipuuzi yapo AFRICA PEKEE...
 
Hata tukicheza na vibonde wa aina gani,Bado hatuwezi kwenda AFCON kwa inch yetu inelaniwa chini ya utawala ccm.hivyo huwa ni ufisadi wa ubadhirifu wa pesa zetu.
 
Hata tukicheza na vibonde wa aina gani,Bado hatuwezi kwenda AFCON kwa inch yetu inelaniwa chini ya utawala ccm.hivyo huwa ni ufisadi wa ubadhirifu wa pesa zetu.

wanasema egypt kuna hali ya hewa kama ya Dar. Sijawahi kusikia hicho kitu.
 
Reactions: PNC
hii timu ivunjwe tu, tusubiri serengeti boys wakue!

huu ni ufujaji wa mali ya umma kabisa kugharamia timu hii
 
hata timu za ndondo cup hawachezi hivii daaah hii ni zaidi ya Makinikia
 
Kwakweli ni upuuz mtupu wanacheza kiboya sana
 
Hata tukicheza na vibonde wa aina gani,Bado hatuwezi kwenda AFCON kwa inch yetu inelaniwa chini ya utawala ccm.hivyo huwa ni ufisadi wa ubadhirifu wa pesa zetu.
mameno yako ni sahihi kabisa
 
Cjawah kuona Thomas ulimwengu cha maana anachocheza upuuz mtupu
Mkuu huyu sio Thomas ni tomato,kijana kwanza kuzeeka akili aisee,kocha nae sub anafanya zimebaki dk 10 wakati anajua kabisa jamaa ni majembe
 
Haki ya nani hayo mazoezi bora wangeenda kigamboni kwanza tumekosa hata ubingwa wa sport pesa kisa hili litimu sjui malinzi utakumbukwa kwa lipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…