Kambi ya TAIFA ya Jumuiya ya Madola ya Riadha Yasambaratika, Serikali Yashindwa kulipa

Kambi ya TAIFA ya Jumuiya ya Madola ya Riadha Yasambaratika, Serikali Yashindwa kulipa

Melubo Letema

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2020
Posts
416
Reaction score
414
Kwa mara ya kwanza kambi ya Riadha iliwekwa West Kilimanjaro, ilipomaliza Mafunzo ya huko, ikaamishiwa Olmotonyi Arusha, baada ya Serikali kushindwa kulipa pango , timu ikahamia Chuo Cha Habari Maalum Jijini Arusha, huku Nako wakatimuliwa baada ya kushindwa kulipa bili Mbalimbali, ikiwemo vyumba na Chakula.

Ndipo Wanariadha wakafukuzwa kwenye Chuo hicho, Kila mtu akaondoka na kwenda kwake wakati Wengine wamepewa hifadhi Kwa wasamaria Wema.

Mjumbe wa kamati ya riadha akaandika hivi:

"Lakini kuna changamoto zimejitokeza zinazosababishwa na utaratibu wa Malipo ya serikali na hivyo tumelazimika kuwapa wachezaji mapumziko ya siku mbili.

Viongozi wa Wizara, BMT na RT wanazishughulikia. Baada ya hizo siku mbili wachezaji watarudi kambini.

Si jambo la kufurahisha kwa wanariadha wetu na shirikisho kwa ujumla, lakini ndio hali halisi." Aliandika hivyo.

Waziri wa wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Anahitajika Ajitafakari , Kwa kuwa Juzi akizindua Marathon Moja alisikika akisema Kambi zote zipo na zimejitosheleza na Pesa zimetolewa.
 
Riadha imetengeneza tittle kwa jirani yetu Kenya,Ethiopia kukusanya medali za kutosha kwenye mashindano sijui kwanini Tanzania kama taifa atuweki mkazo kwenye mchezo huu wa kufukuza upepo.
 
Wapi Gidabudai, ye kazi yake ni kuwalaumu tu wenzake...kamu harass Bayo mpaka Bayo kaachia ngazi na bado hakuna kubwa linalofanyika huko riadha.
 
Back
Top Bottom