informer 06
Member
- May 11, 2024
- 66
- 49
Watoto 30 kati 50 waliofanyiwa uchunguzi katika kambi ya siku 10 iliyofanyika katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) wamefanyiwa upasuaji wa moyo.
Akizungumza wakati wa kufunga kambi hiyo kwenye makao ya taasisi hiyo, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI,Dk Tatizo Waane amesema kambi hiyo imefanywa na madaktari kutoka Kituo cha King Salman Humanitarian Aid kwa kushirikiana na wataalamu wa JKCI.
Ameeleza kuwa matibabu hayo ni muhimu kwa kuwa yanaokoa maisha ya Watoto pamoja na kuokoa gharama.
Amebainisha wazi kuwa timu hiyo wataalamu kwa kushirikiana na wataalamu wa JKCI tokea waanze utaratibu huo wameweza kuchangi Sh bilioni 4.5 ambapo kwa kambi iliyohitimishwa takribani milioni 700 zinadaiwa kutolewa.
Pia Balozi wa Saudi Arabia Nchini Tanzania Yahya Okeish aliwashukuru madkatari na timu yote kutoka kituo cha King Salman na madkatari wa JKCI kwa kufanikisha matibabu ya watoto hao.
“Ninaona heshima kushiriki nanyi kuhitimisha kambi hii ya matibabu ya moyo huu ni ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia na tunapata faida hasa kwa watu tunafurahi naamini kuwaona tena wakitembelea Tanzania tena.
Aidha mmoja wa Wazazi ambaye Mtoto wake amenufaika na suala hilo, Ester Shauri kutoka Mkoa wa Mbeya amesema haikuwa rahisi mtoto wake kupata matibabu kwasababu shida ilikuwa kubwa.
“Mwanzo mtoto alikuwa anachoka mapema ila sikuweza kugundua kwasababu alikuwa haumwi mara kwa mara sikujua ni shida lubwa nimekuja kugundua mwezi wa sita mwaka huu.
Soma Pia: JKCI yashirikiana na wataalamu kutoka Muntada Aid kuwafanyia upasuaji watoto 40 wenyewe matatizo ya moyo
Ameongeza “Nilivyompeleka hospitali walisema anashida kwenye moyo kwa hospitali ndogo hawakuona tatizo ndo wakasema nimpeleke hospitali kubwa.