Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Moja kwa moja kwenye mada na leo nazungumzia umuhimu wa kamera za CCTV.
CCTV (closed- circuit television) ambayo pia yajulikana kama video ya uchunguzi au Video Surveillance ni kifaa muhimu sana cha ulinzi kwenye dunia ya leo.
CCTV hutumika katika maeneo ya umma kwa minajili ya kubaini na kuzuia uhalifu (detection and prevention of crime) na huongozwa na sheria na kanuni za matumizi yake.
Kutokana na matukio mengi ya uhalifu katika sehemu mbalimbali duniani kupita bila kupata ushahidi wa kutoka kiasi cha kuweza kumtia hatiani mtuhumiwa wa uhalifu, sehemu nyingi zimewekwa kamera za CCTV.
Ukiwa Marekani na Ulaya na sasa sehemu nyingi duniani huwezi kukosa kuona kamera za CCTV katika majumba, nyumba za makazi, maofisi, mabarabarani, katika vyombo vya usafiri kama reli mabasi magari ya kukodi (taxis) na ndege vyote hivi vimefungwa kamera za CCTV.
Ukija kwa maeneo kama jeshi la polisi na idara kama za zimamoto wao nao hutumia kamera za kurekodi shughuli zao popote wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao. Polisi (wa doria na wale wabeba silaha au armed police) na hata walinzi wa maduka (security guard) nao pia huvaa BodyCam ambazo ni kwa ajili ya kurekodi matuko yoyote na pia kwa ajili ya usalama wa mhusika.
Polisi wa nchi hizi ziloendelea wakienda kutekeleza kazi yao iwe ni kukamata muuza madawa ya kulevya, au mhalifu yoyote ni lazima wavae kamera za kurekodi matukio. Ni lazima waiwashe kamera hiyo ili kurekodi tukio wanolifanya na baadae kuzima.
Baadae kinofanyika ni kuinywila kamera hiyo/hizo na kufanya analysis na utambuzi wa tukio/matukio na baadae kuchukua hatua kulingana na maamuzi ya mwendesha mashtaka au jaji.
Lakini pamoja na hayo yote wananchi wa nchi hizi nao siku hizi wamekuwa makini na shughuli zozote na mapolisi na uhalifu kwa ujumla. Mtu huweza kuchukua tukio lolote kwa kutumia simu ya mkononi au kamera ya kwenye gari (dashcam) ambazo baadae polis huweza kuweka laini maalum ambayo wananchi wataweza kujaza video hizo.
Pia polisi wakianza uchunguzi ni lazima watataka kuona video zinozunguka eneo tukio lilipotokea na pia kuuliza raia kuhusu kamera zao za majumbani au milango mbele ya nyumba zao.
Kutokana na utendaji kazi zao polisi wa nchi hizi kupata ushirikiano mzuri kutoka kwa wananchi na endapo tukio limetokea, kitu cha kwanza polisi watakifanya ni kuitisha "press conference" ili kueleza tatizo na kisha kuomba wananchi watoe ushirikiano.
Sasa tukiangalia tukio na kutekwa kwa mzee Mohamed Ally Kibao, kitu cha kwanza kabisa ni kulichukua basi alokuwa akisafiria na kulihifadhi kwa uchunguzi wa forensic na pia kuwasiliana na abiria wote walokuwamo kwenye basi.
Abiria hao wataweza kutoa ushirikiano wa kueleza namna tukio lilivyotokea na namna mzee huyo alivyofuatwa kwenye basi na kisha kuteremshwa. Litakuwa ni jambo la kushangaza endapo hakutakuwa na raia yoyote ambae amerekodi tukio hilo isipokuwa kama raia hao walitishiwa maisha yao na kuambiwa wasifanye kitu chochote.
Nini kifanyike.
1. Wananchi watanzania wenzangu wajifunze kutumia simu zao kurekodi matukio yoyote ambayo yaweza kutumiwa kama ushahidi. Hilo liende sambamba na kuanza kununua DashCams za kufunga katika magari ili kujilinda na matukio kama wizi, kutekwa na ajali za barabarani.
2. Vyombo za usafiri kama mabasi ya abiria umefika wakati sasa wa kuhakikisha mabasi ya kisasa yote kamera zake zafanya kazi. Ni lazima mabasi yote ya kisasa kwa sasa yamefungwa kamera toka kiwandani tayari kwa kazi ya kurekodi hivyo kinohitajika ni kuhakikisha kamera hizo zafanya kazi na matukio hayo yamekodiwa na kuhifadhiwa kwenye Kanzidata ya Cloud ambayo ni vigumu kuiingilia.
Cloud storage si ghali na wenye mabasi waweza kuilipia kwa dola chache sana kila mwezi kulingana na ujazo wa data.
3. Wananchi kuwa macho na makini na maisha yao kwani hakuna imani kuwa usalama wao walindwa masaa yote na jeshi la polisi.
Mwisho, matukio ya kutekwa, kuteswa na kuuawa kwa watanzania ni jambo baya na linotia doa serikali na jeshi la polisi. Serikali iamke na ijitokeze kwa kuunda tume huru itayochunguza madhila haya yanotendwa na kundi la watu makatili.
Yawezekana lengo ni kuwatia hofu raia lakini bado misingi ya katiba ya JMT yatoa haki ya uhuru wa kujieleza na kutoa maoni, hayo yote yakiwa ni sehemu ya demokrasia tunoipigia debe kila mara. Je, kwanini raia watiwe hofu kwa kuua au kuteka na kutesa?
Ubalozi wa Marekani umetoa tamko na pengine balozi zingine zitatoa tamko kulingana na kasi ya uwajibikaji wa tukio lolotokea hivi majuzi.