Kamisaa wa sensa: Bajeti ya sensa kutumia bil. 629, NBS: Bajeti ya sensa bil. 400!

Kamisaa wa sensa: Bajeti ya sensa kutumia bil. 629, NBS: Bajeti ya sensa bil. 400!

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
590
Reaction score
1,648
Katika kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na chanel ya ITV tarehe 16 May, 2022, Kamisaa wa Sensa Anna Makinda alihojiwa kuhusu zoezi la sensa, na moja ya kitu alichoelezea ni bajeti ya Sensa, ambapo alisema bajeti ya Sensa kwa mwaka 2022 ni Tsh bilioni 629.

Cha kushangaza jana tarehe 1 September, 2022 Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari kuhusu maendeleo ya Sensa ya Watu na Makazi, Sensa ya Majengo na Sensa ya Anwani za Makazi hadi kufikia August 31, 2022, alisema kuwa bajeti ya Sensa ya Watu na Makazi na Sensa ya Majengo ambayo iliidhinishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ni kiasi cha Tsh. billion 400.

Kwa mkanganyiko huu kati ya Kamisaa wa Sensa na Mtakwimu Mkuu wa Serikali unaleta picha gani, kwamba hakuna mawasiliano kati yao au kuna harufu ya upigaji kwenye zoezi hili?

Hii imekaaje wadau?

bajeti sensa.jpg


NBS.jpg
 
kuna upigaji hapo wahuni washaongeza namba.wanatukamua kwenye tozo alafu wanagawana mchana kweupee.
 
Utasikia Laptop moja wamenunua 20 million ili watupige tuu...
 
629-400 = 229

Wahuni wametia mfukoni Billion 229 km utani, afu maelezo utakayopewa unaweza ukadata
 
Tanzania bado tupo nyuma sana.. sasa tumuini nani hapo na source ipi ni ya ukwel. Watanzania tutakimbilia kwenye kidogo
 
Back
Top Bottom