Kamishina Mkuu TRA haya maagizo mafundi wa ujenzi wa madarasa kukatwa kodi kwenye malipo yao ni yako au mnataka mkwamisha Rais?

REJESHO HURU

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2014
Posts
4,664
Reaction score
9,929
Niende moja kwa moja kwenye mada nikiwa kama mzazi na mwana jamii nilifurahi sana kuona Serikali inatoa pesa za kwenda kujenga madarasa nchi nzima ili mwakani watoto wote watakaochaguliwa wapate nafasi ya kwenda kuanza kidato cha kwanza

Pia nilifurahi kuona ujenzi wa madarasa haya wanatumika mafundi wa mtaani ambao si makandarasi lengo kuu kupunguza gharama za ujenzi kwani hawa mafundi gharama zao kuwa ndogo kwa sababu hawana Kodi na nimafundi ambao wanazunguka maeneo husika kwaiyo hata bei zao huwa chini

Kilichonishangaza tangu majuzi mafundi wamekimbia ujenzi kwa kile wanachodai wao wakati wanafunga mikataba hawakuambiwa watakatwa Kodi asilimia mbili katika malipo yao hivyo kutokana na kupatanisha kazi kwa bei ndogo kumeathiri ulipaji wa vibarua wao kwa hiyo bora waende wakajenge kwa mzee Msiriri ambako jioni ikifika anaondoka na chake siyo hizi kazi ambapo awali walikuwa hawakatwi hii Kodi

Nikastuka nikafutilia nimeambiwa ni agizo kutoka TRA, Sasa unawaza hawa TRA wameibukia wapi muda huu kama wanataka Kodi Serikali ingeruhusu makandarasi wachukue hizi kazi siyo hawa mafundi wa mtaani sababu tayari wameipiga hesabu kazi atafanya kwa muda gani na atapata faida gani leo hii ukimkata hata elfu hamsini tayalri umemuingiza kwenye mgororo na wasaidizi wake wa kazi matokeo yake ndio kesi mnaanza ziona kwa Mkuu wa Wilaya vijana wanalalanika hawajalipwa na fundi sababu fundi anaona hesabu haimlipi anaamua kukimbia

MY TAKE
Kama Serikali inataka kazi ya ujenzi wa haya madarasa iishe kwa wakati waondoke hii Kodi kwa hawa mafundi watazidi kukimbia kazi Serikali itaingia hasara sababu washafunga mikataba, mngewambia mapema kutakuwa na kodi wangejua wanajipangaje.

UPDATE
Hongera serikali kwa kuona ujumbe huu na Jana usiku kuagiza halmashauri zote zisitishe hili zoezi la ukataji Kodi kwa hawa mafundi mpaka mtakapotoa maelekezo mapya.

Ushauri wetu hakuna haja ya hawa mafundi wakatwe Kodi walipwe pesa zao Kodi wataenda kutana nazo kwenye mihamala ya sm na bidhaa uko.
 
Nchi imepoteza mwelekeo hii. Mwananchi hasikilizwi wala hathaminiwi na serikali hii
 
Tutaona mengi sana

Mbuzi wa bwana Kheri amekula mazao kwenye shamba la bwana Kheri , na huko mahakamani hakimu Ni bwana Kheri kwa maana hiyo yote Ni kheri tu...
 
Hizi hela zitakuja kuwafunga watu mark my words
 
Pesa iliyokatwa kodi kwenye miamala inakomaliwa ikatwe kodi tena, daah, hii ni sawa na nyoka taahira kujimeza mkia hakyanani

Mwanamke siku zote anawaza vikoba. Hayo ndiyo matokeo ya mwanamke kuwa kichwa cha familia
 
Hizi hela zitakuja kuwafunga watu mark my words
Inasikitisha sana mafundi wanajenga kwa gharama ndogo hapo hapo linaibuka kundi na agenda zao mbona kipindi cha amagufuri huu ujinga haikuwepo kuna rais aliyekuwa anapenda Kodi kama magufuri
 
Fundi alipwa kupitia bank akienda ATM anakatwa uko tayali TRA wamefanya yao, ndio maana Kuna mafundi na wazabuni hawataki kusikia kazi za serikali kwani Kuna urasimu sana uku chini kundi furani likiona Kuna pesa sehemu furani tu shida inaanza
Pesa iliyokatwa kodi kwenye miamala inakomaliwa ikatwe kodi tena, daah, hii ni sawa na nyoka taahira kujimeza mkia hakyanani

Serikali makanjanja sana, mwaka huu wameweka Hadi kodi kwenye kilimo cha tumbaku (mkulima kakaktwa 2% ya mauzo yake )

Yaani majamaa yamekuwa mezi kichizi, wakati huo yananufaika na ushuru tokana na zao la tumbaku

Hakuwa almashauri inayorudisha lolote kwenye jamii inayo lima tumbaku bado wanaweka Makato ya 2%

Wameona wawakamue na mafundi pia
 
Niende moja kwa moja kwenye mada nikiwa kama mzazi na mwana jamii nilifurahi sana kuona Serikali inatoa pesa za kwenda kujenga madarasa nchi nzima ili mwakani watoto wote watakaochaguliwa wapate nafasi ya kwenda kuanza kidato cha kwanza

Pia nilifurahi kuona ujenzi wa madarasa haya wanatumika mafundi wa mtaani ambao si makandarasi lengo kuu kupunguza gharama za ujenzi kwani hawa mafundi gharama zao kuwa ndogo kwa sababu hawana Kodi na nimafundi ambao wanazunguka maeneo husika kwaiyo hata bei zao huwa chini

Kilichonishangaza tangu majuzi mafundi wamekimbia ujenzi kwa kile wanachodai wao wakati wanafunga mikataba hawakuambiwa watakatwa Kodi asilimia mbili katika malipo yao hivyo kutokana na kupatanisha kazi kwa bei ndogo kumeathiri ulipaji wa vibarua wao kwa hiyo bora waende wakajenge kwa mzee Msiriri ambako jioni ikifika anaondoka na chake siyo hizi kazi ambapo awali walikuwa hawakatwi hii Kodi

Nikastuka nikafutilia nimeambiwa ni agizo kutoka TRA, Sasa unawaza hawa TRA wameibukia wapi muda huu kama wanataka Kodi Serikali ingeruhusu makandarasi wachukue hizi kazi siyo hawa mafundi wa mtaani sababu tayari wameipiga hesabu kazi atafanya kwa muda gani na atapata faida gani leo hii ukimkata hata elfu hamsini tayalri umemuingiza kwenye mgororo na wasaidizi wake wa kazi matokeo yake ndio kesi mnaanza ziona kwa Mkuu wa Wilaya vijana wanalalanika hawajalipwa na fundi sababu fundi anaona hesabu haimlipi anaamua kukimbia

MY TAKE
Kama Serikali inataka kazi ya ujenzi wa haya madarasa iishe kwa wakati waondoke hii Kodi kwa hawa mafundi watazidi kukimbia kazi Serikali itaingia hasara sababu washafunga mikataba, mngewambia mapema kutakuwa na kodi wangejua wanajipangaje.

UPDATE
Hongera serikali kwa kuona ujumbe huu na Jana usiku kuagiza halmashauri zote zisitishe hili zoezi la ukataji Kodi kwa hawa mafundi mpaka mtakapotoa maelekezo mapya.

Ushauri wetu hakuna haja ya hawa mafundi wakatwe Kodi walipwe pesa zao Kodi wataenda kutana nazo kwenye mihamala ya sm na bidhaa uko.
Naomba tukumbuke kuwa sheria ya kodi ya mapato haijamsamehe mtu yeyote anayepata mapato yatokanayo biashara,ajira au uwekezaji

Kadhalika zipo shughuli nyingi za kiuchumi inazofanywa na watu mbalimbali bila kuingizwa katika wigo wa kodi kutokana na changamoto mbalimbali ikiwamo ukosefu wa utayari wa walipakodi kurasimisha na kulipa kodi zao kwa hiari.

Mfumo wa utozaji wa kodi za zuio ndio mfumo pekee ulioonekana kuleta suluhu katika kuingiza kwenye uwigo wa kodi shughuli zote rasmi na zisizo rasmi zenye sifa kukatwa kodi ila wahusika hawakufika kwa hiari yao kusajiliwa kwa kupatiwa TIN na kukadiriwa kodi hasa wafanyabiashara za msimu (kama Kilimo, uchimbaji n.k ) na wale wanaofanya kazi na taasisi za serikali.

Swali
Ni mafundi wangapi waliofika TRA kujisajili wa hiari?

Ni mafundi wangapi wenye vipato vinavyopaswa kulipa kodi wanachangia kodi kwenye mapato yao?

Kumbe basi tunajifunza ya kwanza jukumu la kulipa kodi sio la watanzania Fulani wenye vipato Fulani pekee ndio wanapaswa kulipa kodi, kila mmoja kwa kipato anachokipata anaowajibu wa kisheria wa kuhakikisha anachangia sehemu ya mapato yake kama kodi, haya nimepata toka kwa mshauri wa maswala ya kodi
 
Serikali makanjanja sana, mwaka huu wameweka Hadi kodi kwenye kilimo cha tumbaku (mkulima kakaktwa 2% ya mauzo yake )

Yaani majamaa yamekuwa mezi kichizi, wakati huo yananufaika na ushuru tokana na zao la tumbaku

Hakuwa almashauri inayorudisha lolote kwenye jamii inayo lima tumbaku bado wanaweka Makato ya 2%

Wameona wawakamue na mafundi pia
Hao mafundi Kama kipato Chao kinazidi tsh.270,000 kwa mwezi sheria inawataka wakatwe(withholding tax kwny PAYE) na aliyewapa kazi ndie atawakata,Kama kipato Chao Ni chini ya tsh.270,000 wako exempted.

Suala Ni sheria inasemaje na sio mambo ya kuoneana huruma/kukandamizana.
 
Ni jambo la aibu kuna Watanzania wa nadhani kulipa kodi sio jukumu lao. Hao mafundi wanastahili kukatwa asilimia hiyo pesa kwa sababu ni withholding tax on construction activities. Ni aibu kubwa zaidi kama kuna mtu amesitisha hilo ati kuna mwananchi amelalamika JF.

Kuna makundi ya wananchi yanalipa kodi hawalalamiki, hao mafundi wao wanauspecial upi hawataki kulipa kodi?
 
Back
Top Bottom