Kamishina wa uhamiaji Z'bar adaiwa 'mweupe'


Jee mmelifikisha wapi Taifa kwa hayo madarasa matupu? Elimu ingekuwa ya manufaa kama mwananchi angekuwa anagomboka lakini elimu ya kujitia kwenye siasa na NGO za kuomba misada. Tunahitaji elimu ya kweli lakini hadi saasa tusiwabeze waliotufikisha angalau hapa.
 
Mosi: Tuweke nafasi katika vichwa vyetu kuwa huyu kamishna anaweza kuwa na uhusiano wa namna fulani na 'Afro Shiraz Party' (nafikiri mnanielewa)
Pili: Idara nyeti kama hii, haina nafasi ya kuongozwa kwa uzoefu, ni hatari sana kwa usalama wa taifa letu, ni idara inayo kabiliwa na 'challenges' za mabadiliko ya kiteknolojia na unaongea na mabingwa na wajuvi wa mambo ya mataifa mbalimbali, ni lazima shule yako iwe ya kutosha. Tuache mambo ya kisiasa!!!!
 
Kulikuwa na tatizo gani kuweka habari yenyewe nzima badala ya kuchagua maoni uliyoyapenda wewe?
 
Kwa muda wa takribani wiki mbili sasa kumekuwa na tuhuma nzito za ufisadi na matumizi mabaya mbalimbali ya ofisi katika Idara ya Uhamiaji, moja ya Idara nyeti kabisa nchi, kiuchumi, kisiasa na kidiplomasia.

Shutuma hizi zimeelekezwa zaidi kwa KAMISHNA WA UHAMIAJI, ZANZIBAR, Ndugu, MWINCHOUM NASSOR SALUM.

Nimejaribu kufuatilia kwa undani na nimegundua kweli huyu jamaa ni FISADI MZURI, na kama Serikali haitachukua hatua za dharula djidi ya ke ataliingizia taifa hasara kubwa sana.

Ningependekeza, kwa vile Idara ya Uhamiaji ni ya Muungano, basi PCCB wamchunguze. Binafsi nina taarifa za kutosha kumhusu FISADI huyu anayeibuka kwa kasi kwenye medani hii ya IFISADI.
 
Kajipange upya uje na nyama nyama, habari imejaa mifupa mitupu!
 
Fisadi Hater, Habari za namna hii ni majungu, mifupa mitupu hapo, kama nyama unazo weka ili watu wapime.
 

Acheni kasumba, hivi kunatakiwa degree gani ili mtu aweze kuendesha shughuli za ukurugenzi wa uhamiaji? as long as anafahamu kazi na anauzoefu wa kiuongozi basi hata kama ni form IV basi si tatizo, kumbukeni John Major kaiongoza UK kwa miaka na alikuwa hana hiyo degree kamaliza high school tu (Form VI), kabla ya kuwa Prime Minister aliwahi kuchukua nafasi nyingi tu za uongozi. Mbali na hayo Bill Gates pia hana degree na muangalieni vitu alivyofanya - acheni kasumba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…