Kamishna David Kafulila na "TOLL ROADS". Fikra pevu ya ujenzi wa nchi chini ya Rais Samia Suluhu Hassan

Mkunazi Njiwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2023
Posts
8,538
Reaction score
7,559
Tukiachana na ya Simba asiyetulia wa kule Kizimkazi...

Tukiachana na "assist" 4 na goli 1 la mwamba Clatous Chota Chama,mh.David Kafulila amekuja na wazo kuntu haswa....

TOLL ROADS(barabara za kulipia).

Wenzetu wa Afrika kusini wameanza kuzitumia 1983 ,leo hii mh.Kafulila kamishna wa mipango na fedha (PPP) anayataka makampuni kuwekeza katika ujenzi wa barabara hizo. Tukianzia na ya kutoka Kibaha hadi Morogoro ,kongole kwake[emoji7]

TOLL ROADS huongeza uchumi kwa sababu hizi :-

1)Badala ya wananchi kuumia kwa kodi yao kukatwa kutengeneza barabara ,ujenzi huu wa barabara hizi za kulipia utatufanya tupate fedha ambayo itakwenda kutumika katika ujengaji na uboreshaji wa barabara zetu.

2)Matumizi yake hupunguza muda wa kukaa barabarani.

3)Matumizi yake hupunguza "running cost" ya magari yetu,vipuri na mafuta.

4)Matumizi yake hutuliza fikra na sonona barabarani kwa ule utulivu wake(smooth riding).

5)Matumizi yake yatatusaidia kuziachia barabara zetu kupumua na kutupunguzia mzigo wa maboresho ya hapa na pale.

Tumuunge mkono kamishna David Kafulila akitekeleza ilani ya chama dola chini ya mh.Rais Samia Suluhu Hassan.

Hakika hizi ni fikra tunduizi za maendeleo makubwa kwa ajili ya taifa letu pendwa na vizazi vyake.

#Mama Tanzania milele dumu[emoji7]

#Chifu Hangaya nahodha wa jahazi letu, amen[emoji7]

Pia soma:Kafulila: Tanzania kwa mara ya kwanza tunajenga barabara za kisiasa za kulipia 150km kutoka Kibaha Pwani-Morogoro bila Fedha ya Serikali
 
Wenzetu Kenya wana toll road ya juu yenye urefu wa 22km, sawa na kutoka Tegeta nyuki hadi posta mpya....rejea ni barabara ya juu
 
Tutaanza mbali yao....yetu kutoka Kibaha mpaka Morogoro...zaidi ya kilomita 22....

Ama kwa kuanzia hapo ni haba binamu ?!!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
..toll roads haziivui serikali jukumu la kujenga mabarabara.
 
Toll Road siyo wazo jipya serikalini, linaeleweka miaka nenda rudi. Kwanini hazijaweza kujengwa ni kwasababu nyingi tofauti lakini moja kubwa, Toll Road hazijengwi kwa pesa za kodi za wananchi, hawa ni private investor ndio hu-gharamia ujenzi huo, na baada ya kumaliza kuzijenga kwa gharama zao, ndio watumiaji(wananchi) huanza kulipia pindi wanapo zitumia kwa kulipia hiyo toll fee.

Wawekezaji wana akili pia, Tanzania kulipia Toll fee ni utamaduni mpya, wengi hawawezi kulipia, hilo tu linatosha kuwafanya wawekezaji wasiwekeze kwenye Toll roads.

Daraja la kigamboni kuna toll pale, wwapo wanaokwepa kwa kuzunguka mbagala huko sijui wapi ilimradi wasilipe toll fee. sasa huyo muwekezaji atarudisha pesa zake lini?

Hata wakitangaza tender sijui nani ata bid kujenga toll road Tanzania hii? Na Itajengwa wapi?

Labda Serikali igharamie ujenzi huo kisha idai pesa zake kutoka kwa watumiaji wa barabara kwa kuweka tolls, kitu ambacho sioni kikiwezekana. Hata hao PSPF sijui kama wanaweza kufanya hilo kwa mazingira yetu haya.
 
Mzikimuko kwenye fidia eneo barabara itapita

Na pia kibiashara sio feasible barabara kujenga ya kulipia Dar Moro hasa baada ya ujio wa treni ya mwendo kasi Dar -Moro -Dodoma

Matumizi ya private car yamepungua ambao ndio wangekuwa watumiaji wakuu wa hiyo barabara

Hiyo pesa kuja kurudi ni karne ijayo
 
Tukiachana na ya Simba asiyetulia wa kule Kizimkazi...

Tukiachana na "assist" 4 na goli 1 la mwamba Clatous Chota Chama,mh.David Kafulila amekuja na wazo kuntu haswa....

TOLL ROADS(barabara za kulipia).

Wenzetu wa Afrika kusini wameanza kuzitumia 1983 ,leo hii mh.Kafulila kamishna wa mipango na fedha (PPP) anayataka makampuni kuwekeza katika ujenzi wa barabara hizo. Tukianzia na ya kutoka Kibaha hadi Morogoro ,kongole kwake[emoji7]

TOLL ROADS huongeza uchumi kwa sababu hizi :-

1)Badala ya wananchi kuumia kwa kodi yao kukatwa kutengeneza barabara ,ujenzi huu wa barabara hizi za kulipia utatufanya tupate fedha ambayo itakwenda kutumika katika ujengaji na uboreshaji wa barabara zetu.

2)Matumizi yake hupunguza muda wa kukaa barabarani.

3)Matumizi yake hupunguza "running cost" ya magari yetu,vipuri na mafuta.

4)Matumizi yake hutuliza fikra na sonona barabarani kwa ule utulivu wake(smooth riding).

5)Matumizi yake yatatusaidia kuziachia barabara zetu kupumua na kutupunguzia mzigo wa maboresho ya hapa na pale.

Tumuunge mkono kamishna David Kafulila akitekeleza ilani ya chama dola chini ya mh.Rais Samia Suluhu Hassan.

Hakika hizi ni fikra tunduizi za maendeleo makubwa kwa ajili ya taifa letu pendwa na vizazi vyake.

#Mama Tanzania milele dumu[emoji7]

#Chifu Hangaya nahodha wa jahazi letu, amen[emoji7]

Pia soma:Kafulila: Tanzania kwa mara ya kwanza tunajenga barabara za kisiasa za kulipia 150km kutoka Kibaha Pwani-Morogoro bila Fedha ya Serikali
Promo, Kafulila apewe Uwaziri Mkuu!
 
Kafulila acha kuhangaika. Hata ngazi ya wajumbe wa chama tu hauwezi kutoboa. Yaani omba Mungu SSH aendelee kukukumbuka kwenye teuzi za Rais.
 
Back
Top Bottom