Kamishna Jenerali wa Magereza nchini asema msamaha wa Rais haukumuhusu Lulu

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Juma Malewa amesema katika msamaha uliotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli siku ya uhuru Desemba 9, 2017 haukumuhusu msaani wa filamu Elizabeth Michael maarufu kama Lulu.

Jenerali Malewa amefafanua kuwa mchakato wa kuanza kuangalia wafungwa wakupunguziwa vifungo na kusamehewa haukumuhusisha Elizabeth Michael kutokana na yeye kuingia gerezani wakati tayari mchakato wa kuangalia wafungwa wa kusamehewa na kupunguziwa vifungo ulikuwa umeshaisha

"Msamaha huu haukumuhusu yeye kwa sababu aliingia magereza wakati tayari zoezi hili lilikuwa limekamilika, kwahiyo labda misamaha ijayo kama itakuwepo lakini katika hii haikumuhusu",amesema Kamishna Malewa.

Kamishna Malewa pia ameeleza kuwa vipo vigezo vingi vinavyoweza kumfanya mfungwa asamehewe ama kupunguziwa kifungo kutokana na kosa na muda wa kifungo chake na kwamba misamaha inatofautiana kutokana na kosa kama endapo mfungwa atafata taratibu na kuonekana amerekebishika anaweza kupata msamaha na mengine mengi.

Desemba 9 mwaka huu siku ya uhuru kwa mujibu ya ibara ya 45 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais John Pombe Magufuli alitoa msamaha kwa wafungwa 61 waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa na wawili Nguza Viking (Babu Seya ) na Johnson Nguza (Papii Kocha ) waliohukumiwa kifungo cha maisha jela na wengine kupunguziwa vifungo vyao.

Chanzo: EATV
 
Ni kweli lulu alikua hana uwezo wa kutoka mda huu asubiri mwezi April tu.
 
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Juma Malewa amesema kuwa msamaha uliotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli siku ya Uhuru Desemba 9, 2017 haukumhusu msaani wa filamu Elizabeth Michael maarufu kama Lulu.

Amefafanua kuwa mchakato wa kuanza kuangalia wafungwa wakupunguziwa vifungo na kusamehewa haukumhusisha msanii huyo.

Amesema kuwa vipo vigezo vingi vinavyoweza kumfanya mfungwa asamehewe ama kupunguziwa kifungo kutokana na kosa na muda wa kifungo chake na kwamba misamaha inatofautiana kutokana na kosa.

“Msamaha huu haukumuhusu yeye kwa sababu aliingia magereza wakati tayari zoezi hili lilikuwa limekamilika,”amesema Malewa
 
Alafu angeongezea Mh Rais haongozwi na remote ya bashite na hiyo ndio msg kwao wote wanao fikiri bashite ndio mshauri wake... In addition ur dad is coming alikuwa anajikomba wala hakukuwa na ukweli wowote... End...
 
kaeleweka vizuri
 
Samehe samehe samehe wote baba tufunge na magereza yote maana wote wamefungwa kwa kusingiziwa. Samehe hata wabakaji na wakati samehe hata waliouwa samehesamehe
 
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Juma Malewa amesema katika msamaha uliotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli siku ya uhuru Desemba 9, 2017 haukumuhusu msaani wa filamu Elizabeth Michael maarufu kama Lulu.

Jenerali Malewa amefafanua kuwa mchakato wa kuanza kuangalia wafungwa wakupunguziwa vifungo na kusamehewa haukumuhusisha Elizabeth Michael kutokana na yeye kuingia gerezani wakati tayari mchakato wa kuangalia wafungwa wa kusamehewa na kupunguziwa vifungo ulikuwa umeshaisha

"Msamaha huu haukumuhusu yeye kwa sababu aliingia magereza wakati tayari zoezi hili lilikuwa limekamilika, kwahiyo labda misamaha ijayo kama itakuwepo lakini katika hii haikumuhusu",amesema Kamishna Malewa.

Kamishna Malewa pia ameeleza kuwa vipo vigezo vingi vinavyoweza kumfanya mfungwa asamehewe ama kupunguziwa kifungo kutokana na kosa na muda wa kifungo chake na kwamba misamaha inatofautiana kutokana na kosa kama endapo mfungwa atafata taratibu na kuonekana amerekebishika anaweza kupata msamaha na mengine mengi.

Desemba 9 mwaka huu siku ya uhuru kwa mujibu ya ibara ya 45 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais John Pombe Magufuli alitoa msamaha kwa wafungwa 61 waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa na wawili Nguza Viking (Babu Seya ) na Johnson Nguza (Papii Kocha ) waliohukumiwa kifungo cha maisha jela na wengine kupunguziwa vifungo vyao.

Mpekuzi
 
Kifungo miaka miwili tu na bado "wafurukutwa" wanataka msamaha wa Rais...
 
Kamishna kwa kuanza ku speculate "labda misamaha ijayo" kashaingia katika kampeni ya kumpa msamaha Lulu.

Just the facts please.
 
Hata ningekuwa mim nimefungwa nae gereza moja afu itokee mim nilikaa mda mrefu ma nikapata msamaha wa raisi afu ma yy apate msamaha wa raisi hiyohiyo siku kiukwel nisingekubali yaaan nasema hivi ningemsukumia ndan akaemo japo kwa miezi sita kama sio kuwaambia wafungwa wenzie wamvutie kwa ndan
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…