Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Juma Mwenda, amesema Siku ya Mlipakodi ni tukio maalum linalolenga kutambua na kuwashukuru walipakodi wa kada zote kwa mchango wao katika maendeleo ya taifa.
Akizungumza Januari 23, 2025, jijini Dar es Salaam, wakati wa maadhimisho hayo, Bw. Mwenda ameeleza kuwa utoaji wa tuzo unakusudia kutambua walipakodi waliotoa mchango mkubwa katika sekta mbalimbali, zikiwemo sekta ya madini, taasisi za umma, taasisi za fedha, uzalishaji na viwanda, pamoja na sekta ya utalii.
Bw. Mwenda amebainisha kuwa baadhi ya walipakodi walifanikisha makusanyo makubwa ya kodi katika nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/2025, ambapo TRA ilivuka malengo yake kwa kukusanya Shilingi Trilioni 16.528. Washindi hao pia wametunukiwa tuzo maalum kwa mchango wao.