JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamad amelani kitendo cha upotoshaji wa hali ya uhalifu na usalama visiwani Zanzibar.
Akizungumza na waandishi wa habari huko Makao Makuu ya Polisi Zanzibar amesema usambazaji wa taarifa za upotoshaji kupitia mitandao sio tu kukosa uwajibikaji bali pia huzusha hofu na taharuki kwa jamii.
=============
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KWA VYOMBO VYA HABAR
Hivi karibuni tumeshuhudia kuenea kwa taarifa za upotoshaji kwenye mitandao ya kijamii kuhusu hali ya uhalifu Visiwani Zanzibar. Taarifa hizo mara nyingi zimekuwa zikisambazwa na watumiaji wa mitandao ya kijamii wasio waadilifu ambao wamekosa uwajibikaji kwa jamii.
Lakini pia tumeshuhudia baadhi ya viongozi wa Chama cha ACT Wazalendo wakitumia nafasi zao na mitandao ya kijamii kusambaza taarifa za kupotosha kuhusu hali ya uhalifu na usalama kwa maslahi yanayoonyesha dhahiri yana malengo binafsi ya kisiasa. Mfano wa karibuni ni tukio la tarehe 28/03/2024 la mauaji ya Ngd. Ali Bakar Ali.
Kinyume na madai ya upotoshaji yanayotolewa na Chama Cha ACT Wazalendo ya “... uwepo wa vikundi vya kihalifu vinavyojiimarisha kila siku bila Jeshi la Polisi kuonesha uwezo wa kudhibiti kwa kukinga au kufanya upelelezi unaopelekea wahusika kutiwa hatiani”, napenda niwahakikishie wananchi kuwa madai haya lengo lake ni kuzusha hofu na taharuki. Ni uthibitisho wa utamaduni endelevu wa baadhi ya viongozi wa chama hicho kutothamini juhudi za serikali na taasisi zake katika kudumisha amani na utulivu.
Viongozi wa ACT Wazalendo wanapaswa kutambua uhalifu ni zao la jamii na udhibiti wa uhalifu ni jukumu la jamii. Wao kama sehemu ya jamii, wana wajibu wa kushirikiana na serikali pamoja na vyombo vinavyotekeleza sheria katika kubaini visababishi vikuu vya uhalifu kama vile ukosefu wa malezi, umasikini na mmomonyoko wa maadili na kushiriki katika kutengeneza sera na mikakati madhubuti ya kijamii na kiuchumi inayolenga kuvishuhulikia visababishi hivyo na kuunda hali zinazozuia tabia ya uhalifu na kukuza ustawi wa jamii, badala ya kujiweka pembeni kubuni mikakati ya kuwajengea hofu wananchi.
Sote tunatambua nguvu ya vyama vya siasa katika kuwezesha ubia na ushirikiano kati ya vyombo vinavyotekeleza sheria na jamii katika kuunga mkono programu mbalimbali za kubaini na kuzuia uhalifu kama vile polisi jamii, ambayo lengo lake ni kuwashirikisha wananchi katika kutambua viashiria vya uhalifu kwenye maeneo yao na kuvishuhulikia kabla uhalifu haujatokea. Aidha, kupitia majukwa yao wanasiasa wanaweza kuongeza ufahamu kwa umma juu ya umuhimu wa kuunga mkono juhudi za vyombo vinavyotekeleza sheria, za kubaini na kuzuia uhalifu na kudumisha usalama wao. Ni bahati mbaya kwamba kuna baadhi ya viongozi wa ACT Wazalendo hapa Visiwani wamekuwa wakishawishi wananchi wasijiunge na vikundi vya ulinzi shirikishi kwa madai kuwa ulinzi shirikishi ni sera ya chama kilicho madarakani.
Niwakumbushe wananchi wote kwamba usalama wa raia na mali, hali ya amani na utulivu katika nchi hunufaisha watu wote bila kujali tofauti za kiitikadi, uwezo au hali ya mtu.
Sote tunatambua athari kubwa za usambazaji taarifa potofu na za kutia chumvi kwenye jamii na kwa kutumia mitandao ya kijamii. Zinaweza kuanzisha hofu na wasiwasi hata kama hatari halisi ya kutendewa uhalifu ni ndogo/haipo, kuchochea ubaguzi na mgawanyiko, kudhoofisha juhudi za
kukuza ushirikishwaji wa jamii kwenye mambo mbalimbali yakijumuisha ulinzi na usalama, kudhoofisha imani ya wananchi kwa taasisi za serikali, kudhoofisha mshikamano wa kijamii, kuchangia hisia za kiwewe hasa miongoni mwa makundi ya watoto na wazee. Mmomonyoko huu wa kimaadili katika matumizi ya mitandao ya kijamii unaweza kuzuia juhudi za kushuhulikia masuala ya uhalifu halisi kwa ufanisi na kwa ushirikiano baina jamii na vyombo vinavyotekeleza sheria.
Nitumie nafasi hii kuwaasa viongozi wa ACT Wazalendo hususan wale wanaotumia nafasi zao kusambaza taarifa za upotoshaji zinazoweza kuleta hofu na taharuki kwa jamii waache tabia hiyo. Badala yake watumie fursa walizonazo na majukwaa ya kijamii kukuza mijadala yenye msingi wa ukweli na sera zenye ushahidi ambazo zitasaidia kubaini vyanzo vya uhalifu na kushauri mikakati ya kuvishuhulikia ili kuzuia uhalifu usitokee.
Aidha, natoa rai kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii na wananchi kwa jumla, kuwa waadilifu katika matumizi ya mitandao hiyo na katika mijadala ya umma ili kukuza utamaduni wa uwazi, uwajibikaji na kuheshimiana. Tuwe na mijadala inayolenga kuleta mabadiliko ya maana na mipango madhubuti ya kubaini na kuzuia uhalifu ili kujenga jamii salama na yenye ustahimilivu zaidi kwa watu wote.
Kwa kumalizia, niwahakikishie wananchi Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vya Ulinzi na Usalama, na wananchi kwa ujumla tunao uwezo mkubwa wa kudhibiti uhalifu wa aina yoyote. Niwaombe wananchi wayapuuze madai ya Chama cha ACT Wazalendo, hayana ushahidi wowote. Nawashukuru wananchi wote wema kwa ushirikiano wenu katika kutunza usalama, amani na utulivu ambayo ni misingi mikuu ya kukuza ustawi na mshikamano wetu uliodumu kwa miaka mingi.
ASANTENI KWA KUNISIKILIZA IMETOLEWA NA KAMISHNA WA POLISI ZANZIBAR
Pia soma - ACT: Tunalitaka Jeshi la Polisi Kuhakikisha linawakamata wote waliohusika na Kifo Cha Katibu wa ACT Jimbo la Chaani