Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kamishna wa Polisi Zanzibar CP KOMBO KHAMIS KOMBO amesema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vikosi vingine vya ulinzi limejipanga kuimarisha Ulinzi na usalama wakati wa uchaguzi na kwamba wananchi watatumia haki yao ya kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa katika mazingira ya utulivu.
Akizungumza katika kipindi cha MADA MEZANI kinachorushwa na Habari FM Redio leo Septemba 24, 2025 CP KOMBO amewahimiza wananchi kuheshimu sheria na wasikubali kuhamasishwa kufanya vurugu.