Kamishna wa sensa na mkurugenzi wa takwimu wakutana na masheikh

Kamishna wa sensa na mkurugenzi wa takwimu wakutana na masheikh

BabieWana

Senior Member
Joined
Nov 3, 2010
Posts
178
Reaction score
29
Kamishna mkuu wa sensa na mkurugenzi wa takwimu kutoka NBS wamekutana na masheikh kujadili suala la waislam kutoshiriki sensa ya mwaka huu
Wakiongea na masheikh hao waliwataka waislam washiriki sensa kwani suala la kipengele cha dini halipo kwa mujibu wa katiba kwa kifungu walichokitoa, pia waliwataka waelewe kua suala la sensa maandalizi yote yamekamilika hivyo kurudia kuchapa karatasi itakua ni gharama kubwa mno.

Kwa upande wao masheikh waliwaambia kua suala la katiba haikatazi kuwatambua watu kwa makundi yao, pia wakaongeza kua hata muongozo wa umoja wa mataifa unataka sensa ifanyike kwa kufuata makundi ya watu
pia wakasema kama karatasi zimechapwa tayari zinaweza kurudiwa ili kipengele kiwekwe maaana hakuna ugumu ila kama muda umekua mfupi wanaweza kusogeza sensa mbele kukamilisha maandalizi haya kwani hata uchaguzi mara nyngi tunaona unasogezwa mbele. pia waliwaomba kama kurudia karatasi zote kuchapa ni gharama basi wanaweza kuweka appendix ya kipengele hicho , hii itakua rahisi

Kamishna na mkurugenzi wakaahidi suala hili watalipeleka mbele kwenye mamlaka za juu

Masheikh wanasema bila kipengele hicho waislam hawatahesabiwa, hiyo ndio maoni yao

Jmabo hili litaumiza kichwa kwani kundi dogo hili la waislam lisipohesabiwa itakuwa lina impact kubwa kwa watu wanaojua maana halisi ya sensa ili jambo hili lisiharibike serikali ijitahidi kukubaliana na waislam ili wananchi wote wahesabiwe

Jmabo baya la kushangaza mikoa yote tanzania bara wameitisha kikao cha masheikh na viongozi wengine wa kidini lakini hapa kwetu arusha, mkuu wa mkoa amewatishia kuwafanyia dhambi kubwa masheikh hasa wanao hamasisha watu wasihesabiwe amesema "wapelekeeni salamu akina ...,... na .... kuwa mimi nina dhamabi nyingi sana hivyo wasitake kuniongezea dhambi zingine kwa kitendo chao cha kuhamsisha watu wasikubali kuhesabiwa". chakujiuliza hapa ni dhambi gani ambayo mkuu wa mkoa huyu anataka kuifanya kwa masheikh hawa?

Sote tuko kimya ila kwa sasa tunasema HATUHESABIWI KAMA KIPENGELE CHA DINI HAKIMO, hii ndo busara yetu kwa sasa

Ila waislam wengine hawana uchungu weneyewe kila kitu poa kama wale wa shinyanga, naona hawa hata kwa familia zao hawana uchungu hata wakiona mtu anabaka wanawake zao watafurahi
 
Ngoja nitafute kivuli nipate kinywaji. Huku nikisubiri movie ianze.
 
sijui serikali inaogopa nini kuweka hicho kipengele cha dini. Au kuna siri imejificha hapa?. Kwa nionavyo sensa ya mwaka huu inaelekea kuharibika.
 
jamani tatizo kama serikali imesema kipengele cha dini kisiwemo basi wote tutii amri tusipende kurumbana na serikali kila wakati
 
Sasa mimi nashindwa kukuelewa,unasema kamishina wa sensa kakutana na masheikh. Ina maana ni masheikh wote wa Tanzania au viongozi wa masheikh? Pili ninachofahamu ni kuwa waislamu wana wakilishwa na vyombo kama Bakwata.
Mimi naomba tuache siasa na uchonganishi. Serikali imeshasema kuwa lengo la sensa ni kwa ajili ya kujua idadi ya watu kwa kuangalia umri na jinsia. Sasa ninachokiona hapa ni kuwa kuna watu wanataka kuleta ushindani wa kidini kati ya wakristo na waislamu. Ilo halitawasaidia waislamu wala halitawasaidia wakristo. Tuwe objective na sio subjective.
 
Bakwata wanaiwakisha serikali dhidi ya waislamu.
 
Bakwata ipo ipo tuu ! Kama stamp, unagonga unapojisikia !
 
serikali ya ccm inawa handle hawa jamaa kama mayai yasije kuvunjika kwa sababu ni mtaji wao pekee uiobaki wa kubaki madarakani...kama ni kosa kisheria kugomea sensa, mimi sioni sababu ya serikali kuwabembeleza hawa mashehe...
 
Hivi miaka yote ambayo sensa ilifanyika kulikuwa na hicho kipengele? kwanini mwaka huu imekuwa nongwa kutokuwepo hicho kipengele cha udini. ? Unajua hata BOKO HARAM kule Nigeria walianza kwa kutafuta visababu hadi wakafanikiwa kufanya hayo wanayoyafanya mpaka sasa. Hivi ni kwanini waislamu kila wanapotaka kufanya jambo lihusulodini yao wanataka serikali ihusike? au kwasababu uongozi wote wa juu wa serikali yetu ni wa upande huo? Mh! tusubiri tuone.
 
tatizo nini kama serikali inahesabu idadi za nyumba za ibada kama msikiti na makanisa lengo lao nini? Baadae wanataka kutumbia kuwa makanisa ni
mengi kuliko miskiti wakati wakristo hawachangie makanisa kama waislam.
 
Mimi naona waweke wasiweke maisha yako pale pale, kama ni tight ni tight tuu!! Na kama mtu ni mzembe ni mzembe tu hakunaga unafuu wa jambo lolote!! Cha msingi ni kujua kuwa dini zilikuwepo, zitakuwepo na zitakuwepo. Tuungane kujenga nchi yetu kwa kujadili masuala ya msingi!! Na hivi vitu ndiyo wamalawi wanatuona tumegawanyika wanaanza kutulia timing za kutuibia hadi sehemu ya ziwa nyasa!!
 
tatizo nini kama serikali inahesabu idadi za nyumba za ibada kama msikiti na makanisa lengo lao nini? Baadae wanataka kutumbia kuwa makanisa ni
mengi kuliko miskiti wakati wakristo hawachangie makanisa kama waislam.
Nimeuliza sana hili lakini kila nikiuliza watu wanaingia mitini...wanahesabu nyumba za ibada tu au wanataka kujua exactly ni kanisa/misikiti etc ?? niletee hapa hicho kipengele cha dodoso kinachoonyesha hiyo kitu...
 
serikali ya ccm inawa handle hawa jamaa kama mayai yasije kuvunjika kwa sababu ni mtaji wao pekee uiobaki wa kubaki madarakani...kama ni kosa kisheria kugomea sensa, mimi sioni sababu ya serikali kuwabembeleza hawa mashehe...

Hao wengine ambao si Waislaam ni mtaji wa chama gani kinachotaka kuingia madarakani !?.....................mdomo ulimponza kichwa !
 
Aisee... nimeona ITV waislam wengi Shinyanga wameandamana na wamewalaani VIKALI hao mashehe wanaohamasisha kugomea sensa vilevile wamempongeza mufti mkuu kwa kumchagua Kadhi mkuu...ngoma inogile...
 
serikali niwatu nawatu ni waislam na wakristo kilakitu wewenikutii kwasababu niserikali sikuinasema mwanamume kwa mwanamume wawowane nalo utatiiamri ndomalengoo?
 
Hao wengine ambao si Waislaam ni mtaji wa chama gani kinachotaka kuingia madarakani !?.....................mdomo ulimponza kichwa !

Serikali pia itoe takwimu suni ni wangapi na shia ni wangapi kwasababu waislam halisi ni suni na hawapewi haki zao.
 
Hivi uchaguzi 1995 kurudi nyuma kulikuwa na kadi ya mpiga kura jibu ni hapana sawasawa na katika sensa kuanzia sensa ya mwaka 2002 kurudi nyuma hapakuwepo kipengele cha dini ila kwa sasa kinahitajika kiwepo kutokana na mabariko ya mazingira .mabadiliko ni hali ya kawaida katika maisha.FUNGUKA WEWE.
 
Back
Top Bottom