Kamishna wa Tume ya Uchaguzi ajiuzulu, asema tume imegawanyika na inafanya kazi bila kuzingatia utaratibu

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Roselyn Akombe ajiuzulu, asema tume imegawanyika na inafanya kazi bila kuzingatia utaratibu

Dr. Akombe alituma taarifa kutoka New York alipokuwa akifanya kazi Umoja wa Mataifa kabla ya kwenda kufanya kazi tume ya uchaguzi

Katika taarifa hiyo Dr. Akombe alisema uchaguzi uliopangwa kufanyika hauwezi kukidhi matakwa ya uchaguzi unaoaminika

'' Kwa jinsi tume ilivyo sasa ni hakika haiwezi kutuhakikishia uchaguzi utakaoaminika tarehe 26 Oktoba. Sitaki kuwa sehemu ya dhihaka hiyo kwa uchaguzi wa kiadilifu''

Akihojiwa na shirikala utangazaji la BBC Jumatano Asubuhi, amesema amekimbilia New York akihofia usalama wa maisha yake na pia na kuongezea Mwenyekiti wa Tume hiyo, Wafula Chebukati amezingirwa

Alikuwa ni sehemu ya timu iliyokuwa isafiri kwenda Dubai kusimamia kuchapishwa kwa karatasi za uchaguzi

=============================================
IEBC commissioner Roselyn Akombe has resigned from the poll agency.

Dr Akombe sent the statement from New York, where she was based, working for the UN, before she took the job at the electoral commission.

In the statement, Dr Akombe said the repeat election as planned cannot meet the basic expectations of a credible election.
ELECTORAL INTEGRITY

"The commission in its current state can surely not guarantee a credible election on October 26. I do no want to be party to such a mockery to electoral integrity," she said.

In an interview with the BBC Wednesday morning , Dr Akombe said she went to New York fearing for her life. She said IEBC chairman Wafula Chebukati is under siege.
In her statement she said it is unacceptable for any party to disrupt, attack IEBC staff; says acts must be condemned and action taken against perpetrators.

"It broke my heart in the last few days to listen to my staff in the field, majority of whom truly want to do the right thing, express to me their safety and security concerns. I shared detailed reports from staff in four of the Counties most hit by the ongoing protests - Nairobi, Siaya, Kisumu, and Homa Bay - with the hope that this will bring sobriety to our decision making.

"Instead this was met with more extremist responses from most Commissioners, who are keen to have an election even if it is at the cost of the lives of our staff and voters," she said.

She was supposed to be part of a team that is in Dubai to monitor the printing of ballot papers.

Dr Akombe toured Nyanza and the Western region last week as the commission worked to train officers to handle elections.

Source: Daily Nation
 

Attachments

  • AKOMBE.jpg
    32.3 KB · Views: 57
Kwani hujui sasa tunafuata katiba ya Rwanda?


$wissme
 
Aliyekuwa moja ya makamishna wakuu wa tume ya uchaguzi Kenya IEBC,ndugu Roselyn Akombe Kwamboka amejiuzulu kutoka nafasi yake hiyo kwa kile alichodai kuwa
"Tume hiyo haina uwezo wa kuongoza uchaguzi wa kuaminika".

Ndugu Rosslyn aliyazungumza hayo akiwa nchini Marekani ambako kwa sasa ndipo alipo na amesema hafikirii kurudi tena nyumbani,Kenya siku za hivi karibuni.

Wakati hayo yakiendelea mahakama ya juu ya Kenya hapo jana imetoa/imeondoa zuio la Serikali lilitaka wanachama Wa NASA kutoandamana katika miji mikubwa,hivyo basi kuruhusu wanachama hao kuendelea na maandamano yao kama ilivyopangwa.

Kitu gani atajibu Chabukati kutokana na alichokisema Roselyn na kujiuzulu kwake?tusubiri na tuone.
 
Watu wenye nia njema na wananchi wao, hawawezi kuuana kwa ajili ya kuingia ikulu, kuna kitu si bure.
 
Inasemekana jana zaidi ya Lorry 15 ikiwa na wanajeshi zimeelekea jijini Kisumu ame tweet Robert Alai na kuweka video ikionyesha malori hayo.
 
Hakuna kama Tanzania, panga pangua.
Tz ipi hii ambayo viongozi wake wako radhi kupiga selfie wakipatanisha nje, na kualika wapinzani wa nje kuwafanyia tafrija, lakini hawawezi kukaa na wapinzani wa ndani, kujadili mustakbali wa nchi yetu!!! Hii ambayo mwenyekiti wa A anateua makamishna wa uchaguzi na mwenyekiti wao?! Hii ambayo mwenyekiti huyo anateua wakuu wa wilaya, mkoa, vyombo vya dola???!!! Na hao wateule ni sehemu ya uchaguzi?!

Tz ni mbaya zaidi labda uwe mnufaika!!
 
 
Africa mashariki "EAC" ni laana ktk democracy ya kweli!!! Angalau west Africa chini ya ECOWAS

Tume hizi za uchaguzi pamoja na kuitwa TUME HURU si huru kabisa
Leo kwa sababu mnamatatizo inataja Afrika mashariki, juzi mlipokuwa mnasifia demokrasia Kenya, mlikua mnataja Kenya kama nchi, kama ni jambo zuri ni Kenya, jambo likiwa baya ni Afrika mashariki, tafadhali endelea kutaja Kenya katika hili, usiingize Afrika mashariki
 
Lakini bado wako mbele yetu kwa almost kila kitu wala usijidanganye!! Kila kitu!!
 
Hayo yote inayoyasema yamo kwenye katiba yetu ambayo tulikibaliana wenyewe, hakuna hata moja ambalo lipo nje ya katiba, sio wote watakaokubaliana na katiba iliyopo lakini hiyo haimaanishi kwambakatiba sio halali.
 
Lakini bado wako mbele yetu kwa almost kila kitu wala usijidanganye!! Kila kitu!!
Wewe ndiyo unasema hivyo, mimi ninasema kinyume chake, kwamba wapo nyuma yetu kwa almost kwa kila kitu, ni jukumu lako kutetea hoja yako kwa ushaidi, ili na mimi nikuletee ushaidi kutetea hoja zangu, tukubaliane maeneo ya kulinganisha ili tuone ni nchi gani ipo vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…