Kampala int un-serikali inatuangamiza......!!!????

Kampala int un-serikali inatuangamiza......!!!????

Joined
Oct 10, 2014
Posts
14
Reaction score
4
Ni wiki mbili sasa tangu kutulia kwa mgomo uliokuwa ukiendelea kati ya wanafunzi na chuo kufuatia kutokuwapo na usajili wa kozi za afya ktk bodi mbalimbali za wataalamu ikiwemo dodi ya wafamasia.Kutulia kwa mgomo huu ni baada ya wanafunzi hao kukutana na serikali yaani mkurugenzi bodi ya mikopo bw mgaya,waziri wa elimu,mkurugenzi wa mafunzo ya afya toka wizarani,afisa upelelezi kanda maalumu ya dar es salaam,OCD wilaya ya ilala na wawakilishi toka bodi ya wafamasia.Mkutano huu ulishuhudia serikali ikitoa wiki mbili yaani kuanzia tar 13.aprili 2015 hadi 28 aprili 2015 uliwapa imani wanafunzi na kuamini serikali itashirikiana nao bega kwa bega kutatua matatizo yao.kwa muda huu wa wiki 2 serikali iliagiza wanafunzi wachague kamati ya watu kumi ambayo itakuwa huru na iliakikishiwa usalama na kuibariki kuwa ni ya halali.Kazi kubwa ya kamati hii ilikuwa ni kujadili hoja za msingi kwa njia ya uwakilishi na kurudisha taarifa kwa wanafunzi kadri ilivyowezekana ikiwa pia ni kamati pekee ambayo ilipewa mamlaka ya kuhudhuria vikao vikuu vya mjadala huu vilivyofanyika tar 29-30 april 2015 na kuahidi kamati hii ndio itakayopewa majibu na kuyawakilisha kwa wanafunzi wenzao sambamba na msimamo wa serikali juu ya maamuzi hayo.

SINTOFAHAMU

-Tar 29-30 april 2015 siku ambayo kikao kilikaa na kufanya maamuzi hakuna hata mwakilishi mmoja kati ya wale kumi walichaguliwa aliitwa kuhudhuria kikao hicho kama walivyo ahidi.sababu hzijatajwa.

-Tar 30 april 2015 siku ambayo serikali iliahidi kamati tuliyoichagua itayafuatia majibu ya maamuzi ya kikao lilibandikwa tangazo kunako mbao za matangazo za chuo mapema asubuhi likiwataka watu wanafunzi 16 wakiwamo wale 10 wa kamati iliyoagizwa kuundwa na serikali na wengine 6 wakiwa ni wawakilishi wa madarasa toka mwaka wa kwanza hadi wa pili,toka ngazi zote za cheti mpaka shahada kukutana na utawala majira ya saaa 9 kamili alasili nayo ikafanya hivyo.

-Kikao hicho cha watu 16 na utawala wa juu wa chuo kilimalizika mishale ya saa 12 jioni ,wanafunzi takribani 13 kati ya 16 walipewa barua za kusimamishwa chuo hadi tar 11 august 2015 kamati ya nidhamu itakapokaa.walioachwa bila kupewa barua ni pamoja na waziri wa mikopo na waziri wa elimu wa serikali ya wanafunzi.

-Wanafunzi 10 wa ile kamati iliyoahidiwa kulindwa kati 16 walijaribu kuwasiliana na viongozi wa wizara wanalishughulikia suala hili kupitia mawasiliano ya simu lakini hakuna aliyepokea simu.kwann..sintofahamu!!!? Lakini moja ya wanafunzi ambao wanandugu na jamaa zao katika bodi ya wafamasia alifanikiwa kuongea na afisa mmoja toka bodi hiyo(jina kapuni),alikataa katukatu kueleza kilichoazimiwa tulipojaribu kumdodosa sana haya yalikuwa moja ya majibu aliyatoa "NDUGU ZANGU MAMBO YA KAMPALA NI MAZITO MNO KUENDELEA KUYAJADILI NA KUYAZUNGUMZIA BINAFSI YANAWEZA KUNIHATARISHIA MAISHA YANGU KWANI YANABEBA MASLAHI BINAFSI,MWENYE MAAMUZI PEKEE KWA SASA NI MSAJILI MKUU...BI ELIZABETH YEYE NDIO ATALIZUNGUMZIA".ni sehemu ya maongezi kwa njia ya simu.

Kwa sasa wanafunzi wamepunguzwa nguvu na hali kila mmoja amekuwa mnyonge,zaidi ni kwa watoto wa walala hoi ambao wanategemea serikali itasema nn ndio wjue hatima yao....baadhi ya wanafunzi tayar wamekwisha anza chukua hatua binafsi kwani mpaka sasa zaidi ya wanafunzi 100 wameachana na kampala ama kwa kuacha chuo au kuhama.

PIA:Tatizo la usajili wa kozi si tu kwa health science ni kwa kozi zote za chuo hiki kwa sababu ajili zilizotoka hivi karibuni hakuna mwanafunzi wa kampala aliyeajiriwa kigezo ni kwamba taaluma zao hazitambuliki tanzania,yaani chuo walichosoma{kampala} hakitambuliki kama kinatoa taaluma hizo.
TCU wamewezaje kudahiri wanafunzi chuo cha kampala hususa ni kozi za afya ilihali bodi za wataalamu wa kada hizo hazitambui uhalali wa chuo hicho.SerikAli kupitia HESLB wamewezaje kupoteza mabilioni ya shilingi kwa taasisi ambayo hawajui matunda ya yake yatakuwaje.

JAMANI TUNAOMBENI MSAADA WA KITAALAMU KWA TULIPOFIKA WAPI NA IPI NI NJIA SAHIHI YA KUPITA KUPATA HAKI YETU SISI WATOTO WENU,WATANZANIA WENZEUNU NA WADOGO ZENU.


INAUMA SANA.
 
sooo sad nimeumia sana.

cjui hata nitoe comment gan hebu ninywe maji kwanza poleni wadogo zetu
 
Nyiee mlifauluu marks chachee tangiaa linii mtuu akaacha chuo kinachoeleweka na kwenda chuo ambacho wanafunzi wengi tunakijua ni gharama na ubabaishaji mwingi usilazimishe kusoma kitu wakatii huwezo wako mdogo wengi mnadivision zetu zile za kawaida kwaninii msingeomba hata baadhi ya vyuo vya gov au vya private kama st francis bugando na vingine viingi vinavyojielewa kwaninii mnaaply vyuo alafuu hamfuatilii details za chuo husika auu mnapenda kusifiwa kwamba mnalipa ada ndefuu wakatii kuna ubabaishajii na wengi mnaosoma kampala mnamarks za ubabaishajii mnalazimisha mambo hahahahahhaha karibunii mbeya rufaa dental therapy walalahoi wenzangu ada laki sita kwa mwaka hahahahahhaha
 
we serotherapy acha kukatisha tamaa wenzangu kaka ivi nani kakuambia waliopale wote Wana low division mkuu,jiangalie kaka Ukimaliza hapo mbeya unaweza jikuta unaangukia kampala Aaaaaaaah msalimie gemba hapo.
 
labda nikuulize swali mshani,ivi kaka hapo mbona Kila mtoa mada kuhusu kampala anazungumzia pharmacy izo kozi zengine vipi hawana matatizo namaanisha madaktari sababu mkizungumzia mnajitaja nyinyi tu pharmacy au maabara na kama hawana matatizo wanawasaidia vipi kama wanafunzi wenzenu maana mpo nyumba moja.
 
kampala siasa zimejaa.... hizi kozi nyingine hawaeleweki, hakuna taarifa za uhakika mfano medice wao wanaambiwa wanao usajili wa muda lakini hakuna oficial documents kudhibitisha, naweza sema wanajifariji kwa hilo hivyo hawashiriki kabisa na sisi, kwa upande wa medical lab na wao hivyo hivyo kama medicine.
ni pharmacy pekee ndio tumepata oficial documents kuhusu usajili wetu,hivyo ushahidi huu unafanya tuwe na nguvu ya kuhoji lakini wenzetu hawana oficial information kutoka bodi zao husika.
 
Nchi iache ubaguzi wa elimu kwa kukalili kuwa daktari ni lazima asome muhimbili kama kuna fursa kama hii serikali itoe usajiri na iboreshe yale yanayo onekana kuwa ni mapungufu ili tupate madaktari au wafamasia wa kutosha ili wananchi wapate haki yao ya matibabu siyo kuishua kupanga foleni maospitalini.
 
hapo mgomo unaanza upya wasizingue hao jamaa kama vipi warud uganda kwao.
 
nyie mliomalza education njoon chuon na wale wa kutoka health science njoon 2endeleze harakati
 
we serotherapy acha kukatisha tamaa wenzangu kaka ivi nani kakuambia waliopale wote Wana low division mkuu,jiangalie kaka Ukimaliza hapo mbeya unaweza jikuta unaangukia kampala Aaaaaaaah msalimie gemba hapo.

Hii ndio tabia mbaya za baadhi ya Watanzania wenzetu,wanapenda penda sana kuwaponda wenzao.
 
Back
Top Bottom