Mshani de Orbital
Member
- Oct 10, 2014
- 14
- 4
Mambo yamekuwa mambo, kampala hapatoshi....!,baada ya ustaarabu na uvumilivu mwingi sasa kauli ya MH. Pinda ya kwamba "WAPIGWE TU" yatekelezwa,polisi watumia mabomu ya machozi na maji ya kuwasha kutawanya wanafunzi waliostaarabika na welevu ambao walikuwa wamejikusanya katika moja ya viunga vya chuo hiki wakisubiri kamati ya bunge ili waweze kutoa malalamiko yao na hoja zao juu ya uozo wa chuo hiki mbali na kusubiri kamati pia wanafunzi walitaka utawala watoe tamko rasmi kuhusu taarifa zilizoenea na kuchapishwa katika makaratasi yenye nembo na muhuli wa chuo hiki kwamba chuo kimefungwa kwa muda usiojulikana,
#Je ni nani katoa tamko la chuo kufungwa ghafla hivi ilihali kamati ya bunge iliagiza lazima ikutane na wanafunzi na kuwasikiliza,sasa basi kamati ikija itaongea na nani?
[URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=kwa]#kwa nn[/URL] polisi wanatumia nguvu kiasi hiki kuwatawanya watu ambao hawajafanya fujo yaani mabomu ya machozi na maji washa nani katoa amri hii,na ni kwann haya yanakuja baada ya kamati kuundwa.
#kwa kuwa chuo hiki kimepakana na shule za msingi za mwangaza na maarifa wanafunzi wa shule hizi wameathiriwa vibaya na mabomu na maji haya iliyopelekea shughuli za masomo kusitishwa na mwanafunzi mmoja kuzimia na amelazwa zahanati ya GONGOLAMBOTO kwa ujinga huu serikali itasema nn?
Baada ya vurugu hizo wanafunzi wa chuo walijibu mashambulizi kwa mawe,uharibifu watokea chuoni na mitaa jirani kwani polisi wameingia hadi mitaani na kukamata raia ambao siyo wanafunzi.
Haya ndio waliyataka,watasemaje wanafunga chuo leo wakati hata ua la chuo hiki halijavunjwa wakashindwa kufanya hivyo wakati wana funzi walipofunga barabara,eti leo sababu kuna kamati ya bunge inkuja kuchunguza umafia unaendelea chuoni kinafungwa.
"HAKUNA MAREFU YASIYO NA NCHA"