Kampala University na Vyuo vingine iwe fundisho kwetu vijana wa Tanzania

Lord Lofa

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2011
Posts
2,390
Reaction score
2,396
Wakuu kwa mfumo wa utendaji wa vyombo vya serikali ni complicated. mfano kesi ya hiki chuo.
hiki chuo hawatoi kozi za afya tu kuna kozi mbalimbali ambapo nina uhakika kwa kozi zisizo za afya
TCU itakuwa imeona hicho chuo kimekidhi vigezo shida ni hapo kwenye kozi za Afya ambazo kimsingi
ili chuo au taasisi iruhusiwe kutoa kozi hizo ni lazima wawe wamekidhi vigezo vilivyowekwa na hizi bodi
kwa maana nyengine kuna urasimu kati ya hizi bodi na vyuo vyenyewe sababu kwa kesi ya hiki chuo ni
wanafunzi wa kozi za afya tu ndo wanazungushwa wengine mambo yanaaendelea ni kweli kuna uhusika
wa TCU ila kwa hiki chuo ni mdogo tofauti na ile ya st.Joseph Arusha kule.

kilio changu mimi ni kwa wanafunzi inakuwaje mtu uchague chuo ambacho hakina usajili na wala kozi
zake hazisajiliwa na bodi husika ok lets say hukutegemea kupangwa hapo, TCU hawampeleki mtu
sehemu ambayo haipo katika machaguo yako ma 5 kama hukuiweka ya 1 kwanini uliiweka namba 5
hii haikupaswa kuwa sehemu ya machaguo yako kabisa.

Mwanafunzi Tena wa sayansi ulishindwaje kufanya kautafiti ili ujue background,rank na vitu vyote
muhimu kuhusu vyuo unavyovichagua au ilikuwa kufuata mkumbo? hivi vyuo vipo katika mitandao ya
hizi bodi vimeonyeshwa usajili wake kozi ambazo zinatolewa zipo kama zimesajiliwa au la
ok uliangalia ukakosa uliuliza ndugu na marafiki ambao ninaamini ni miongoni mwa waajiriwa wa hizi
Taasisi ok Huna ndugu huko ulishindwa hata kuuliza hapa jamiiforums ambayo ina watu wa kada zote
wanakusanyika hapa ni kweli ungekosa msaada au hata facebook?

Vijana wakitanzania tuache kuishi kwa mazoea na tuache kutafuta wachawi wa matatizoo yetu
wakati wachawi ni sisi wenyewe. Hakuna kijana wakitanzania aliyesoma na kuelimika asiejua
utendaji wa vyombo na taasisi za serikali yetu. ukitaka wawe wachawi hata kwenye sehemu ambayo
umakini na jitahada zako ungeweza kuzuia matatizo basi wao watakuroga na utarogeka kwelikweli
wao wanashida gani, wamesoma, wana kazi, wana pesa, na hata maisha ya kuishi duniani wengine
wanayo mafupi kuishi ukilinganisha na wewe they have got nothing to loose but but you have a lot
to loose kama kijana.

Hii iwe fundisho kwa wale wote wanaojipanga kujiunga na elimu ya juu kwa mwaka huu na ijayo
na hii iwe changamoto kwa ambao wapo shuleni wasome kwa bidii ili wafaulu vema wasije waka
chaguliwa kwenye vyuo na taasisi zisizokidhi mahitaji ya Mitaala na kozi wanazopenda kusomea
katika Elimu ya juu. Kijana mwenzangu mchawi wa mafanikio yako ni wewe mwenyewe.

Your fate is on your hand is up to make a right decision for your destiny
 
Hichi chuo kinawaibia watanzania wenzetu hela tena n chuo chenye Ada kubwa na kinachukua wanafunzi wengi xana
Bt serikali inatetea uovu huo cjui kuna watu wanafaidika kupitia hichi chuo kimsingi hakuna usajiri wowote na vijana wanaangaika xana kila cku wamegoma Sana lakin serikali haifanyi chochote
 
Yan bro hiki chuo cha Kampala mi nasoma pale TCU kuweni na huruma kwetu cc wanyonge wengne tulichagua pale pasipo kujua hiki chuo kikoje hasa upande wa koz za afya ila pale hakuna kitu serikali tuangalieni sisi wanyonge
 
Mkuu hoja yako kuwa ni uzembe wa wanafunzi kuchagua vyuo visivyo na vigezo imeeleweka lakini tambua yafuatayo; 1. TCU ni chombo cha Serikali chenye jukumu la kudhibiti,kukagua na kusajili vyuo vikuu hivyo chuo kama KIU Kipo ktk TCU-GUIDE BOOK na kozi hizo za afya mwanafunzi utamlaumu kwa lipi:what::what: 2. Si rahisi kwa mhitimu form 6 kufuatilia/kujua mambo ya vyuo vikuu hadi usajili wa kozi katika chuo kilicho ktk TCU GUIDE BOOK si inamaana hakina shida yoyote hadi kiwe ktk tcu list:what::what: ningekuona umeleta uzi wa maana kama UNGEHOJI MAJUKUMU YA TCU mpaka kuleta sintofahamu hii kwa wanafunzi😕
 
Kwa kweli mih naweza kusema kuwa serikali ya nchi yetu imekuwa ikifanya kazi kwa mazoea...haiwezekani wanafunzi wawe kwenye mgomo kwa takribani miezi 6 wakidai haki zao..na serikali ikawa inakumbatia tu chuo hiki...kwa tafiti nilizofanya chuo hiki hakistahihili hata kuitwa chuo kikuu kwa kuwa kinaonekana kikifanya mambo yake kimagumashi...Nashangaa kusikia kuwa TCU inatambua kuwa chuo hiki katika kozi za afya hakitambuliwi na mabaraza ya kitaaluma na bado haichukui hatua yoyote..ya hata kuwahamisha wanafunzi hao na kuwapeleka kwenye vyuo vyenye sifa. Hii ni kashfa kubwa sana na ni doa katika taifa. Naomba mamlaka husika zishughulikie hili suala maana vijana wanapoteza muda na pesa zao bila sababu zozote za msingi.
 
KIU ni kimeo sana. Hata kile cha kansanga kampala ni aibu tupu. watu wanakikimbia hakuna elimu pale. Cha kushangaza wabongo wamejaa humo balaa.
 
Kwa kweki imetosha...sisi watanzania hatuko tayari kuona watoto wetu wakipewa elimu iliyo chini ya kiwango na ilihali wanasoma kozi nyeti sana za afya...hii inaandaa taifa lenye wataalamu wasio kuwa na uwezo katika taaluma zao...na hii inaweza leta hasara kwa taifa huko mbeleni. WATAKUJA KUUA NDUGU ZETU HAWA HUKO MBELENI...Katika hili inabidi tuwe serious.
 
jamani sijakataa madhaifu ya TCU lakini mimi nachoshangaa ni kama watu hamjui utendaji wa hii serikali
Serikali inayoweza kucheza na afya za raia wake na usalama wao ni serikali isiyo aminika kabisa utegemee
nini hapo mara ngapi mikopo imechelewa the whole system is corrupt.
 

Kuwa serious unapojibu mada makini! Xana ndio nini! Unaniudhi mburula wewe!!!!
 
umeongea ujinga mwanzo kabisa ivi unadhani wanafunz wangechunguzaje kwamba chuo hakijasajiliwa au laa wakati mpka Tcu wamekiweka kwenye guide book yao hapo ni uzembe wa nani Tcu au wanafunzi..? hakika ni uzembe wa Tcu kutoshirikiana na body husika kujua kwamba chuo kimesajiliwa au hapana ili wakiweke au wakitoe nakushangaa unaandika msg ndefu alafu haina maana chamsingi wanafunzi hao waweze kuamishwa na kulipwa fidia zao pesa walizopoteza na mda waliopoteza hapo.serikali yetu inacheza na maisha ya watu ni zaidi ya wanafunzi mia mbili wapo nje hao hawajajua hatma ya serikali juu yao serikali inabidi ichukue hatua kali juu ya hili pamoja na kuadhibu wote waliohusika na kupeleka wanafunzi hao mahala pasipo
 
mkuu nashukuru kwa kuona ujinga nilioandika. Hicho chuo kinatoa takribani kozi 17 kati ya hizo kozi 14 ni za biashara, utawala, na sheria kozi 3 tu ndizo ambazo za Afya chuo hakiwezi nyimwa usajili kama kime kidhi vigezo vya kutoa kozi nyengine maake wanao andamana wote ni wanaochukua masomo ya Afya tu ni kweli madhaifu ya TCU yapo sijakataa
Lakini hivi pamoja na hayo madhaifu ni nani mwenye akili timamu asiyejua utendaji wa vyombo na taasisi za serikali yetu kwa sasa? ni nani asiyejua?
Wanakufa watu kwa kukosa madawa, polisi wanavamiwa, watu wanaofail wanaongezeka then leo unashangaa haya kwa TCU. afu unajiita unasoma kweli? siwatetei ila mtu lazima uwe makini unapo fanya mambo yako ukizingatia hali
halisi ya nchi yetu. Andamaneni keep on complaining kama taifa tunapata kweli hasara lakini hasara kubwa ni kwa
hao wanafunzi sababu wanaweza rudia mwaka na pesa ndo hivyo tena TCU hawana cha kupoteza pamoja na makosa
yao tusiishi kama Tanzania hatuijui na huo uwajibikaji mnaoulilia kuufikia sio leo ngoja wanafunzi wabweteke tu
wataandamana sana
 
Mkuu nakubaliana nawe madhaifu ya TCU na Bodi nimakubwa sana tu lakini ndo hvyo sasa ishatokea
madhaifu hayap kwao tu.Utendaji wa taasisi nyingi katika nchi yetu unafahamika watanzania shida
yamekuwa maisha yetu tatizo ni mfumo mzima sasa tufanye nini sasa ili kuzuia yasijetokea tena au
tuyapunguze vipi haya
Hili la mwanafunzi kushindwa kufatilia usajili ni uzembe tu mkuu. Internet hatuitumii kwa vitu vya
kujenga kabisa hivo vitu ni mtu anavitafuta hata online anavipata kabisa na hata unaweza kuuliza pia
Hebu fikiria kuna siku nimekuta muhitimu wa form six tena mjini kabisa hata kufanya Transaction ya
Mpesa anasaidiwa mtu anaenda kusajiliwa hana email hajui hata kuifungua ukweli ni kwamba bado tuna
mapungufu mengi tu dunia ya sasa imebadilika sana upashanaji wa habari wa sasa ni mkubwa sasa hivi
unaweza jua jambo linalotokea maili nyingi sana lazima tubadilike tena hasa wasomi
 
Kiu kweli pasua kichwa mara waziri wa elimu amefika na wataalam wake wa tcu na kukubali kukitambua mara waziri wa Afya amekubali kuzitambua kozi za afya na wale waliomaliza waende nacte au tcu wakafanyiwe evaluation ya vyeti vyao ili vitambulike sasa tunasikia mmeandama tena kweli mnatuchanganya vijana,mie nawashauri kwa hapo komaeni muone usajili kwa macho na komaeni ada ishuke,kozi azina usajili na ada juu sasa ndio nini?komaeni mpate usajili na ada ishuke,chuo kiwe local kama alivyosema waziri wa elimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…