Kampeni chafu zaanza UVCCM


Well, ingawa nachukia sana siasa hizi za kikaburu lakini ni muhimu wasomaji wakajua kuwa Hussein Bashe alikuwa na bado mpambe mzuri sana wa ROSTAM AZIZI ambaye alikuwa bosi wake wakati Hussein akifanya kazi katika kampuni ya Mwananchi Communications inayomiliki gazeti hili liloandika hii habari.

Hussein Bashe mwenye ufadhili mkubwa wa ROSTAM na anayetokea mkoa wa TABORA alihusika kwa namna fulani katika kufanikisha zile siasa chafu za kibaguzi dhidi ya Dr Salim Ahmed SALIM.

Wanasema...........

Tanzanianjema
 
Fedha ya wizi iliwapa nguvu CCM na kutwaa madaraka ya kuiongoza nchi sasa fedha hiyohiyo imegeuka kuanza kuwatafuna wenyewe.
Udhaifu siku zote huzaliwa pale penye uimara na palipo egemeo kuu, Fedha haramu.

Kile kiwatiacho nguvu CCM ndicho kitakachowaliza wabakie jivu la kumwagwa Bahari ya Hindi.
 


Tanzania Daima

Inaonyesha huna taarifa sahihi juu ya hili awali ni kuunge mkono kuchukia ubaguzi na kuuita ni ukaburu.

Juu ya ulicho ongea si kweli 2005 Bashe alikua mfanyakazi wa mwananchi bali kipindi hicho alikua mfanyakazi wa kampuni ya CELTEL.

Swala la uhusiano wao hatuwezi kuutazama kwa kuwa wametoka mkoa mmoja BASHE 2007 alihujumiwa na walokua wana mtandao na jina lake likapotea ktk mazingira ya kutatanisha ingawa wachunguzi wa Duru waligundua kua bwana huyu alishinda NEC na alipata kura ZAIDI ya 1000 lakini samweli sita chini ya maelekezo ya ROSTAM AZIZI jina likafichwa na kusababisha ukumbi kupiga kelele lakini jina likapotea.

Bashe 2005 alihujumiwa ktk uchaguzi wa jimbo nzega na Bwana Rostam akimsaidia bwana Seleli,pia 2007 Bashe alitofauutiana na Bwana Rostam katika uchaguzi wa Mkoa wa Tabora Bashe akimsaidia Mzee anaeitwa Nkumba walitofautiana

Naeleza haya ili usipotoshe watu si kweli kua huyu bwana ni mpambe wa Rostama AZIZI.
 


..conspiracy..
 
Ningepata nafasi ya kukaa nae na kumshauri( japo nahisi hashauriki), 'Ningemwomba' akae pembeni apumzike! Si vema kujishuhudia ukifa kwenye kifo kibaya kama cha moto au maji!
 
Na Simon Mhina

SOURCE: Nipashe

Hawa ndio viongozi wetu: Im out of words...
 
Like a son like a father. Hakuna cha ajabu hapo isipokuwa wameamua kusema ukweli tu kwani wamekuwa wakipokea fedha chafu kwa muda mrefu tu.
 
Like a son like a father. Hakuna cha ajabu hapo isipokuwa wameamua kusema ukweli tu kwani wamekuwa wakipokea fedha chafu kwa muda mrefu tu.

Tuko pamoja mkuu, kilichonishtua zaidi ni kuamua ku-legalize it... Kazi kweli kweli
 
Tutapokea fedha bila kujali zinakotoka-UVCCM

2008-11-24 09:59:56
Na Simon Mhina


Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umesema utaendelea kupokea fedha kutoka kwa wafadhili bila kujali zimetoka wapi au mfadhili amezipata kwa njia gani.

Akizungumza na Nipashe Makao Mkuu ya Umoja huo jijini Dar es Salaam, Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya Uhamasishaji Charles Charles alisema UVCCM haikuwa na sababu ya kuchunguza wala kusita kupokea fedha za kugharamia uchagizi toka kwa kada wao Tanil Somaiya, kwa vile hawana vyombo vya dola.

Charles ametoa kauli hiyo kujibu msimamo uliotolewa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Jerry Slaa ambaye alisema hatua ya Somaiya kuamua kugharamia uchaguzi huo kwa Sh. milioni 400 ilikuwa na walakini.

``Mtu yeyote ambaye anaamua kutusaidia, hatuna sababu ya kuanza kuchunguza vyanzo vya mapato yake ili mradi tu awe anafuata taratibu za kutoa mchango. Kazi ya kumchunguza mtu kuwa kapata wapi fedha hatuwezi kuifanya sisi,`` alisema.

Alisema si haki kuhoji ni vipi mfanyabiashara huyo anachangia UVCCM pekee na kuacha jumuiya nyingine, kwani mfadhili ndiye siku zote huamua fedha zake azipeleke wapi.

``Kumtuhumu Somaiya eti kwanini kama ana mapenzi na CCM asichangie jumuiya nyingine, ni upungufu mkubwa wa kuwaza na kupembua mambo na pia ni udhaifu wa fikra na upeo wa kisiasa,`` alisema.

Charles alisema Somaiya alikuwa mjumbe katika kamati ya kutafuta fedha za kugharamia uchaguzi huo na ni mmoja wa watu walioombwa kuchangia.

``Mbali na hivyo, siku zote mtoaji hachaguliwi wapi apeleke fedha zake, bali anaamua mwenyewe,`` alisema na kuongeza ``huenda Jumuiya nyingine hazikumuomba ndio maana hakuzichangia``.

Alisema ameshangazwa na kauli hiyo ya Slaa, ambao kwa kiasi kikubwa inafanana na ile ya Mkurugenzi wa Vijana (Chadema), John Mnyika.

Alisema kama kweli Slaa anaona Somaiya ni fisadi, basi amripoti kwenye vyombo vya dola.

Pia alisema Slaa akiwa mjumbe wa vikao vya CCM alipaswa kupeleka malalamiko yake huku badala ya kuzungumza na vyombo vya habari.

Akijibu `madongo` hayo, Slaa alisema Charles hajui kitu kwa vile licha ya kwamba amerukia jukwaa la CCM hivi karibuni akitokea upinzani, lakini pia majibu yake kwamba UVCCM inapokea fedha popote bila kuchunguza uhalali wake, yanaonyesha jinsi `shule` ilivyompiga chenga.

``Huwezi ukapokea fedha tu kwa chombo cha watu kama UVCCM, huyu haelewi kwamba kuna sheria ya kudhibiti fedha haramu, nadhani haya ni matatizo ya elimu, tunashukuru yupo CCM tutamfundisha kidogo kidogo ataelewa. Lakini wakati anajifunza, asiwe mpayukaji, anatutia aibu,`` alisema.

Slaa alisema anachopigia kelele sio hatua ya UVCCM kuchukua fedha haramu za Somaiya, lakini anahoji ni vipi umoja unashindwa kujigharamia hadi watokee wafadhili.

``UVCCM ndipo chimbuko la viongozi hivyo, ninahofu kwa mtindo huu tunazalisha viongozi ombaomba hata watakapokuwa serikalini,`` alisema.

Alisisitiza kwamba, Somaiya si mtu safi na hatua yake ya kumwaga fedha UVCCM inalenga kufunika tuhuma dhidi yake.

SOURCE: Nipashe
 

Kaka kazi ya propaganda humu huiwezi. Nakushauri kwanza uende ukamjibu Nape Nnauye kwenye ule uwongo wako mwengine katika thread inayodai kuwa yeye anamuunga mkono/anakuunga mkono (BASHE). Yaani huwezi hata kuangalia kama kuna mtu anaweza kuaamini kuwa NAPE NNAUYE kumuunga mkono mgombea wa MTANDAO MASLAHI.

Salam wote kambini...

Tanzanianjema
 
Watoto wa vigogo wapata ushindi kuongoza UVCCM
Na Waandishi Wetu

Habari hii imeandaliwa na Julieth Ngarabali, Kibaha, Lilian Lucas,Morogoro, Paulina David, Mwanza, Brandy Nelson, Mbeya, Joyce Joliga, Songea, Lilian Lugakingira Bukoba, Mwandishi Wetu, Sumbawanga na Ally Sonda,Moshi
 
Hii habari inanikumbusha kale kawimbo: "CCM ina wenyewe!"
 
Amosi Makalla hajui anachosema, ufisadi ungekuwa uzushi huyo Rajab Maranda mweka hazina wa CCM Kigoma na wenzie kumi na nane wanafanya nini mahakamani Kisutu? Tatizo la ccm ni kuokoteza watu barabarani na kuwabatiza majina eti "KADA WA CCM" ndio inakuwa qualification ya kuwa "TREASURER" wa ccm Taifa!! Makalla ana utaalam gani wa kuwa mweka hazina wa chama cha siasa kinachojiheshimu mtu ambaye wengi tunamjua utaalam wake ulikuwa kuhesabu vigae pale Mbezi Tiles; ndio maana anabwabwaja hovyo hovyo tu!!.
 
Chrisant Mzindakaya lazima amehonga sana akitumia fedha alizokwapua kwa mgongo wa BOT ili mwanae apate uenyekiti wa vijana CCM huko Rukwa. Matokeo haya yanaonyesha jinsi mafisadi wa ccm wanavyowatayalisha watoto wao kurithi chama chao ili hapo baadae waweze kuficha siri za maovu ya baba zao; unaona hata yule Mwang'onda wa Kagoda amehakikisha mwanae pia ameingia kwenye ulingo wa siasa.
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni,Amos Makala ni miongoni wa viongozi wa CCM wenye upeo wa kuona mbali
 
Bulesi
kwa taarifa zako Amos Makala ni msomi CPA holder,vile vile ana Advance Diploma ya Business Admnistration na Postgraduate degree ya procurement and supply kutoka chuo cha usimamizi wa fedha IFM
Maranda ni maimuna kaishia darasa la saba kuna kipindi alijaribi kujiunga na Elimu ya watu wazima Unfortunately akafeli akiwa form 2
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…