Kampeni ku'unfollow wasanii wanaonunulika na vyama vya siasa

Ngonepi

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2013
Posts
1,872
Reaction score
1,207
Wasalaam wana Jf,

Nikiwa kama raia ambaye ili nipunguze 'stress' za kila siku za kimaisha, nahitaji burudani mbalimbali! Mojawapo ya burudani ni muziki na maigizo. Nimesikitishwa na wengi wa wasanii wa muziki na maigizo kuonyesha misimamo yao ya kisiasa waziwazi kwenye kurasa zao za mitandao na hasa Instagram!

Nikiwa kama shabiki mwenye msimamo wangu katika siasa nimesikitishwa kwa kiasi kikubwa na jambo hili.Sio shida kwa kila mtu kushabikia chama akitakacho lakini kwa wingi huu wa wasanii ambao juzi tu tuliwaona Mlimani city walikotwambia kuwa wameandaa sherehe ya kumuaga Kikwete am ambapo ilitumika kisiasa, tunaamini kuwa WAMENUNULIKA!

Binafsi kwa kipindi hiki nimeamua kuwa "UNFOLOW" wasanii wote wanaoonyesha mihemko yao kipindi hiki cha kampeni mpaka uchaguzi utakapoisha na ningependa muungaane na mimi kukataa wasanii hawa kutumika kisiasa katika kipindi hiki kwa kuwa UNFOLOW Instagram na Facebook!
 
unadhani dunia nzima na watu wote tutakuwa na mawazo ya aina moja au ya kufanana... mfano mimi kiusanii namkubali afande sele na prof jay eti kwa sababu hawapo upande wangu wa kisiasa eti niseme hawajui kuimba au wameishiwa... nitakuwa mtumwa wa fikra.... tufanye siasa zisizo na chuki
 
Nao ni wananchi mkikaa mashuleni na makazini mnashabikia chama na wao why wasifanye hivyo.

Uhuru kwa kila mtu na maisha yake. Kazi huko siasa hukoooooo
 
Wasanii ni binadam kama binadam wengine wana haki ya kuonyesha Hisia zao, Usanii ni kazi yao na pia wana maamuzi katika Siasa n.k. hata kama kuna jamii inawaangalia bado ni binadamu na wana maamuzi yao binafsi, ni sawa na wewe boss wako akufukuze kazi ati tu kisa mmetofautiana vyama, diamon ni mwanamuziki wakati huo huo ni mfanyabiashara na ameshanunulia na ccm kwa ajili ya kampeni hatuna budi kukubaliana nalo, diamond ataendelea kuwa mwanamuziki na mtanzania ambae hajavunja sheria, ni kama baadhi ya wanaccm wanavyoendelea kumkubali professor j. hawa wasanii wakishangilia chadema ni sawa hakuna kuwaunfollow wakishangilia ccm ndo tatizo, tusiwe hivyo, TUONYESHE UKAKAMAVU KATIKA SIASA.
 
Hahahaha vipi wakina wolper,prof Jay, aunty ezekieli, juma nature.......nao umewa unfollow au kisa wao ni chadema

My take ; me naona wametumia haki yao kikatiba.......so siungi mkono hoja
 

Ww ni kiazi usiwe na akili mdebwedo na yakijinga....kila mtu anahaki ya kumchagua mtu anayempenda mbona wasaniii wengine wanaoshabikia ukawa hujaeleza ivooo...watu kama nyinyi nihasara kwa taifaaa
 

Mie nshamaliza kazi
 
Acha ujuha, mbona sisi huku professor J, na Sugu sio tu kwamba wametangaza msimamo wao ila na kugombea wamegombea?
 

Acha kupanik mkuu unaingilia mpaka uhuru wa mtu kisa msanii??
 

Akili zako fupi, kwanza ndo nawafollow hadi wale ambao nilikuwa sija-wafollow
 
we unasema kuwaunfollow tu?!funga kabisa na account zako huko instagram na twitter na facebook na kwingineko!watu hatuna habareeee nitampigia kura ninayemtaka mimi baaaasi!!
 

Mhxuuuuuuuuu !!😡😡😡
 
What I need is just good music basi.

Mambo yake binafsi hayanihusu.

Hivi kweli kama wasanii wa nchi hii wangekuwa na mashabiki diehards kama mnavyotaka ionekane leo,wangekuwa na maisha hayo waliyonayo?

Maanake hata nakala halisi za kazi zao hamnunui halafu mnataka muwapangie mpaka mambo yao binafsi.
 
Ni sawa kabisa kwasababu Lowassa ni muigizaji basi atatuburudisha katika kipindi hiki cha uchaguzi...umeeleweka
 
Tupa kule wasanii vilaza wote waongozwao na njaa badala ya akili!!

Ni huru kila mtu kuungamkono chama apendacho, ila kushabikia wale walioshindwa kusimamia haki za wasanii kwa miaka yote na kupelekea wawe na majina makubwa kuliko vipato vyao ni UMBURULAZZ!! Unfolow wote!!
 
TANGAZO KWA UMMA; Habari hii imekuja kufuati DIAMOND kuonyesha mapenzi yake kwa CCM, lakini wasanii kama Prof jay, Afande sele, na mh Sugu wao kuonyesha mapenzi yao CDM na A.C.T si tatizo. Hakika wewe kijana ni NEMBO YA TAIFA ULIFANYALO LOLOTE NI MJADALA WA TAIFA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…