Elections 2010 Kampeni Moshi mjini katika picha

Mgombea CCM aahidi kudhibiti karo

MGOMBEA ubunge wa Moshi Mjini kwa tiketi ya CCM, Justine Salakana, amewaomba wananchi wamchague ili ashirikiane na vyombo vilivyopo kudhibiti upandaji holela wa ada za shule za msingi na sekondari binafsi.

Akizungumza jana na wananchi katika mtaa wa Soweto kata ya Korongoni mjini Moshi Salakana aliwaomba wananchi wampe ridhaa ya kuwa Mbunge wao ili arahisishe mfumo wa maisha kuliko hali ilivyo sasa.

Alisema,asilimia kubwa ya wananchi wa manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro kwa jumla ni wa kipato cha chini, lakini wanapenda watoto wao wapate elimu bora ila tatizo ni viwango vya ada vinavyopanda kwa kisingizio cha soko huria.

“Jimbo la Moshi lina changamoto nyingi … hatuwezi kumaliza zote kwa wakati mmoja, lazima tuanze na vipaumbele, suala la elimu ni la kuangalia kwa mapana, nipeni nafasi nikashirikiane na vyombo husika tudhibiti viwango vya ada,” alisema.

Alisema,hata Serikali imeliona jambo hilo ambapo Rais Jakaya Kikwete alitangaza kuwa umefika wakati Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), kuunda chombo kitakachodhibiti ada kwa shule hizo na elimu ya juu.

Salakana alisema, Rais Kikwete alilazimika kutoa kauli hiyo, wakati wa kukabidhi hati idhini kwa vyuo 13 vya elimu ya juu inayotolewa na TCU, lakini akaeleza kutoridhishwa kwake na ada ambazo hupangwa bila kuwa na udhibiti.


Chanzo: Habari Leo
 
Babu M asante sana. Kazi inaoneka ni nzito!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…