Kampeni nyingi za utunzaji mazingira zimekosa uhalisia

Kampeni nyingi za utunzaji mazingira zimekosa uhalisia

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Kabla hujaenda mbali kusoma huu uzi tazama hiyo picha kisha utuambie kama kinachofanyika hapo kinahamasisha chochote.

Ndugu zangu katika mambo ambayo nimeshindwa kabisa kuyaelewa ni hizi kanpeni za kuhusu mazingira ninazoziona kwenye vyombo vya habari. Kwa upande wangu naona nyingi zinafanyika kisiasa na watu kuishia kupiga hela na kuendelea na mambo yao. Haiingii akilini kuhamasisha utunzaji mazingira kwa kwenda kudeki lami huku umevaa Tshirt zenye kaulimbiu. Na zile za kwenda kufanya usafi Beach kila inapotokea uhamasishaji. Hakuna uhalisia wowote zaidi ya upigaji hela. Mwananchi wa kawaida anaishia kuwaona wale mabalozi wa mazingira kama wapigaji tu wasio na faida.

Kuna maeneo mengi ya kufanyia kampeni na kweli ikaleta hamasa. Kwa mfano upandaji miti maeneo yenye uhaba wa miti kama Dodoma. Kutoa elimu kwa wananchi wanaokata miti na kuuza mkaa badala ya kukusanya vijana na wasichana warembo ukumbi flani wa kifahari na kuwapa semina ambayo hawataitumia kwa maslahi ya wengi. Badala ya kwenda beach mngeenda hata soko la Mabibo na Buguruni mkahamasisha pale ingevutia.

Sipingi kabisa hizo jitihada ila fanyeni vitu vyenye uhalisia ili kuleta matokeo chanya.
 

Attachments

  • FB_IMG_1670057708745.jpg
    FB_IMG_1670057708745.jpg
    35.2 KB · Views: 8
Back
Top Bottom