Kampeni ya "Dondosha mkono sweta" ndio suluhisho la kupunguza kasi ya maambukizi ya VVU?

Articulator

Senior Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
194
Reaction score
141
Kwa kipindi cha takribani miaka mitano au zaidi sasa,kumekuwa na uhamasishaji wa Voluntary male medical circumcision katika bara la Africa huku katika inchi yetu ya Tanzania kampeni ya Dondosha mkonosweta ikionekana kushika hatamu katika sehemu mbalimbali za inchi yetu lengo likiwa ni kuzuia maambukizo ya virusi vya ukimwi.

Kampeni hii pamoja na nyingine za mfano wake zinazoendeshwa na asasi za kimarekani kwa ushirikiano na wizara ya afya na ustawi wa jamii,zimekuwa zikitoa huduma ya tohara kwa wanaume na watoto wa kiume katika vijiji,tarafa na wilaya mbalimbali inchini.

Kampeni hizi zimekuwa zikifanyika katika maeneo yaliyo na kiwango kidogo cha uelewa wa elimu ya ugonjwa wa ukimwi,huku zikiwaacha wengi kati ya waliopokea huduma wakiamini kuwa kwa kufanyiwa tohara sasa wako salama na hawawezi kupata maambukizi ya ukimwi.

Tohara inahubiriwa kana kwamba ni condom ya asili na the likeliest outcome is that HIV infections would actually increase badala ya kupungua.
Circumcision must be combined with other techniques of HIV prevention, such as safe sex and voluntary testing. It is not sufficient to rely on circumcision alone to prevent HIV transmission.

Katika kipindi hiki cha ukimwi, nilitazamia wizara ya afya itafanya juhudi za makusudi kuhakikisha inakuwa na condoms za kutosha kwa ajili ya kusambaza katika maeneo mbalimbali inchini, lakini inasikitisha kuona nyumba za wageni zinakosa condoms,sio zile zinazopaswa kutolewa bure tu bali hata za kuuza inakuwa ni mtihani,hii ikiwaweka katika hali hatarishi wageni wa nyumba hizo waliokuwa na nia ya kushiriki mapenzi salama.

Jitihada za dhati zifanyike kuhakikisha condoms zinapatikana kwa urahisi katika maeneo yote yaliyo na viashiria vya kuzaliwa kwa mahusiano yasiyo rasmi.

 

Hujaeleweka ndugu, unatoa lawama kwa wizara ya afya kuhusu upatikanaji wa kondom au unapigia debe misaada ya marekani? Pia takwimu zako ni za uongo, kwamba huduma ya tohara inatolewa mikoa yenye watu wenye uelewa mdogo wa huduma hiyo.

Hivi Mashirika ya Marekani yanatekeleza kwa kushirikiana na serikali au serikali inatekeleza kwa kushirikiana na watu wa marekani?

Ni vizuri ukajipanga badala ya kukurupuka na kuandika habari kama hii inayopotosha.
 
Hivi viashiria vyakuzaliwa kwa mahusiano yasiyo rasmi ni vipi mkuu?nadhani ingekua vema zaidi kama ungeshauri elimu itiliwe mkazo zaidi kuhusu madhara ya ngono zembe na ukimwi.kondom zinawezakupatikana kwa wingi na zisitumike vilevile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…