Copro mtego
JF-Expert Member
- Aug 22, 2022
- 619
- 796
UTANGULIZI
Serikali imeanzisha kampeni ya kupambana na usugu wa madawa na tiba za kiholela kwa wananchi kupitia kampeni iitwayo HOLELA HOLELA ITAKUKOST. Hii kampeni ni nzuri kwa jamii na ina matunda mengi chanya kwa sababu itasaidia kupunguza na kuondoa magonjwa sugu ya kuambukizwa, kutibu ugonjwa sahihi na kupunguza madhara ya tiba holela kama vile vifo na kukua kwa maradhi ambayo yangetibika mapema. Hivyo hii kampeni itasaidia sana kuimarisha afya za watanzania na kurahisisha tiba kwa magonjwa mengi hasa ya kuambukiza.
Kampeni hii imejikita sana kwenye kuelimisha wananchi kuhusu kuacha kujitibia kiholela holela au kwa mazoea na kutofuata ushauri wa kitaalamu kama ambavyo baadhi huwa wanafanya katika jamii zetu. Wananchi wamekuwa wakielimishwa kupitia vyombo mbali mbali vya habari hasa kupitia vipindi mbali mbali vya redio.
Kampeni hii imeendelea kufanywa kwa wananchi kwa kutumia wanahabari,wataalam mbali mbali wa afya na pia kupitia shuhuda mbali mbali kutoka kwa watu walioathirika na mitindo ya kujitibia kiholela holela.
HOLELA HOLELA KWENYE SECTA ZA AFYA
Katika utoaji wa huduma za afya kumekuwepo na uholela wa utoaji tiba na ushauri kwa wagonjwa na kwa namna mbali mbali. Baadhi ya maeneo huduma za afya zinapotolewa kiholela ni kama ifuatavyo.
TIBA MBADALA/ ASILI
Kumekuwepo na ongezeko kubwa la tiba mbali mbali mbadala huku wauzaji wakidai ni tiba asili wakienda mbali na kudai kwamba hazina kemikali na ni salama ili kuvutia wateja na waweze kuuza bidhaa zao. Kiuhalisia dawa hizi zote hazijafanyiwa utafiti wa kutosha kujua ni namna gani dawa hizi zinachakatwa mwilini na kuondoshwa mwilini pia haijulikani ni kiasi gani cha dozi ya dawa ambayo ni salama kwa mtumiaji. Vile vile wauzaji hawana vipimo vya magonjwa hivyo hutibu watu kiholela holela. Mfano tafiti zinaonesha kwamba asilimia 35 ya ugonjwa wa figo (acute kidney injury) husababishwa na matumizi ya tiba mbadala/ asili katika nchi zenye uchumi wa chini huku ikichangia hadi asilimia 70 ya vifo vinavyotokana na tatizo la figo la ghafla (acute kidney injury).
Pia wauzaji wengi wa madawa asilia sio wataalamu wa afya kwa hiyo huwa wanatibu bila kujua nini wanachokitibu hivyo kufanya tiba hii mbadala/asili kuwa tiba ya kiholela holela. Binafsi nimejaribu mara kadhaa kuwauliza wauzaji wa madawa haya kutoka makampuni mbali mbali ya tiba mbadala hasa mitandaoni na wengine ana kwa ana lakini wamekosa majibu lakini pia wameshindwa hata kufahamu nn kimetumika kutengeneza hizo dawa na pia mchanganyiko na kiwango (concentration) havijulikani.
Nimeweza kuona baadhi ya wagonjwa waliopata matatizo kama ya kisukari, shinikizo la damu na figo ila baada ya kugundulika waliacha dawa za hospitali na kutumia dawa mbadala lakini matokeo yake wamerudishwa hospitalin wengi wao wakiwa wameshapata madhara makubwa kama figo kushindwa kufanya kazi kabisa kutokana na shinikizo la juu la damu na kisukari ambavyo havikutibiwa.
MADUKA BINAFSI YA DAWA ZA BINADAMU (PHARMACY)
Kuna ongezeko la maduka ya madawa (pharmacy) na kumekuwepo na wamiliki wasiokuwa na weledi wa kazi zao na wamekuwa wakitoa huduma tofauti na utaratibu ukiowekwa na wizara pamoja na miongozo ya utoaji dawa.
Kumekuwepo na maduka ya dawa muhimu lakini yanauza dawa ambazo kimsingi hazitakiwi kutumika katika tiba za awali (primary health care) zinatakiwa zitumike ngazi za juu lakini zinauzwa katika maduka madogoadogo ya dawa mitaani. Mfano dawa za maambukizi mbali mbali hasa ya mfumo wa mkojo (UTI) ambazo zilitakiwa zipatikane kuanzia kwenye hospitali za wilaya na rufaa zimekuwa zikiuzwa kiholela katika maduka ya dawa na watu wamekuwa wakiuziwa bila kufuata utaratibu.
Dawa ambazo zilitakiwa zitumike baada ya dawa za mwanzo kushindwa kufanya kazi vizuri zimekuwa zikiuzwa kama dawa za awali kwenye maduka ya dawa. Hii imepelekea usugu wa vimelea dhidi ya dawa hivyo kupelekea tiba kuwa ngumu kwa wagonjwa hata katika hospitali za rufaa. Madawa kwa mfano cefriaxone sulbactam, meropenem na amoxyclave yamekuwa yakiuzwa kiholela katika jamii kupitia maduka ya dawa.
Pia madawa ya maumivu yanayotakiwa yatumike kwa mpangilio maalumu yamekuwa yakiuzwa kiholela kwenye maduka ya dawa. Mfano nimeshuhudia mgonjwa mmoja aliyekuwa alitumia dawa ya maumivu aina ya morphine kwa muda kutoka duka la dawa hadi anakuja hospitali alikuwa na urahibu (addiction) lakini alikuwa hawezi kupata choo hivyo alilazimika kufanyiwa upasuaji mkubwa wa mfumo wa chakula.
WATUMISHI WA VITUO VYA SERIKALI VYA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA.
Kuna baadhi ya watumishi katika vituo vya serikali vya kutolea huduma za afya wasiokuwa na weledi wamekuwa mawakala wa makampuni ya tiba mbadala hivyo wanauza dawa ambazo sio za hospitalini (kutoka makampuni ya tiba mbadala) kwa wagonjwa. Niliwahi kushuhudia afisa tabibu msaidizi anamuuzia mgonjwa dawa kutoka kampuni la tiba mbadala na cha kusikitisha dawa haikuwa sahihi kwa tatizo la mgonjwa.
NINI KIFANYIKE
Ili kuondoa uholela kwenye sekta ya afya yafuatayo yafanyike.

- Wizara ya afya pamoja na mamlaka zirudie kupitia muongozo kuhusu tiba mbadala. Mamlaka zihakikishe dawa za tiba mbadala zimefanyiwa utafiti wa kutosha ili kuhakikisha usalama kwa watumiaji.
- Mamlaka zinazohusika na tiba mbadala zihakikishe mchanganyiko wa dawa (ingredients) unafahamika pamoja na kiwango cha mchanganyiko (concentration) vinawekwa wazi.
- Maduka ya dawa yadhibitiwe katika uuzaji wake wa dawa na dawa zisizotakiwa kuuzwa kwenye huduma za awali na sheria iwe kali kwa wamiliki na wauzaji pia ufuatiliaji uwe mkubwa na hatua zichukuliwe kwa wanaouza dawa zisizotakiwa kuuzwa bila maagizo ya daktari.
- Dawa zote ambazo zinaweza kuwa madhara au kuzalisha usugu endapo zitatumika kiholela holela zidhibitiwe kuuzwa na maduka ya dawa binafsi.
- Upatikanaji wa dawa hospitali uongezwe ili kuondoa uwezekano wa watu kununua dawa kwenye maduka binafsi ya dawa hivyo kuepusha kuuziwa dawa zisizotakiwa kwa wakati husika.
- Ufuatiliaji wa weledi kwa watumishi kwenye vituo vya utoaji wa huduma hasa hospitali za uma ili kuwabaini watumishi wa afya wasiokuwa na weledi na wachukuliwe hatua stahiki ili kukomesha tabia ya uuzaji wa dawa zisizo rasmi katika mifumo ya hospitali. Hii itasaidia kujenga Imani kwa wananchi juu ya utoaji wa huduma za afya nchini na watoa huduma pia. Vile vile itarahisisha utaratibu wa utoaji wa huduma hivyo kuondoa madhara ya utoaji wa huduma kiholela holela.
- HITIMISHO
- Holela holela ikidhibitiwa kwenye sekta za utoaji wa huduma za afya, itakuwa imethibitiwa katika jamii nzima na taifa litakuwa salama na watu wake watakuwa wenye afya imara.
Upvote
26