Kampeni ya "Komboa pointi za Kagera sugar" yazinduliwa,kuirudishia pointi za juma4 ijayo.

Wonderful

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2015
Posts
7,347
Reaction score
5,986
Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Mwesigwa Celestine ambaye sasa ni katibu mkuu wa TFF, ameitisha kikao cha kamati ya Kamati ya Sheria, Katiba na Hadhi za Waehezaji ambacho kinaelezwa kimepewa jina la “komboa pointi za Kagera”.




Taarifa za ndani kutoka TFF zinaeleza, kikao hicho kimepangwa kufanyika Jumanne na kuhakikisha kinarejesha “haki” ya Kagera baada ya Kamati ya Saa 72 kuipa Simba pointi tatu na mabao matatu baada ya Kagera Sugar, kubainika ilimchezesha beki Mohammed Fakhi akiwa na pointi tatu.




“Kweli hicho kikao kimeitishwa na wajumbe wameishatumiwa email, kazi itakuwa ni moja tu kuipa Kagera pointi. Hapa nafikiri wewe hujajua ndugu yangu, Yanga wameungana na kuhakikisha iwe isiwe pointi za Kagera zinarudi. “Baba mwenye nyumba anataka pointi za timu yake zirudi, si unajua ndiye mwenyekiti wa soka Kagera.





“Wakati haya yanatokea, baba mwenye nyumba hakuwepo, alikuwa Morocco. Sasa amerudi na anataka pointi zirudi. Hapa kuna Uyanga, kumbuka viongozi wote wa juu ni Yanga. Lakini usisahau wote wanatokea hukohuko, sasa hizi pointi hata kama Fakhi alikuwa ana kadi tatu, zitarudi,” kilieleza chanzo.




EMAIL YA MWESIGWA KWENDA KWA WAJUMBE:




Kikao cha Kamati ya Sheria,Katiba na Hadhi za Wachezaji

jm selestine <mjselestine@yahoo.co.uk>

To TPLB TPLB <tplb.tplb@yahoo.com>, Boniface Wambura <wambura70@gmail.com>

Cc Jamal Malinzi <jamalmalinzi@gmail.com>, Richard Sinamtwa <richardsinamtwa@gmail.com>

Friday, April 14, 2017 2:06 PM

Click to View Full HTML

Mtendaji Mkuu,

Bodi ya Ligi Kuu (TPLB).




Hii ni kukufahamisha kuwa kikao cha dharula cha Kamati ya Sheria,Katiba na Hadhi za Wachezaji ya TFF inategemewa kukaa siku ya Jumanne tarehe 18/04/2017 katika hoteli ya Protea Sea View saa 4 asubuhi.Unatakiwa kufika kwenye kikao na wafuatao:

1.Joel Balisidya

2.Rose Msamila

3.Michael Ngogo

3.Match officials wote wa mchezo wa ligi Kuu kati ya Kagera Sugar na African Lyon ie Match comm,centre ref,two assistants na mwamuzi wa nne.

4.Viongozi wa Kagera Sugar




Kila mmoja afike na nyaraka alizo nazo kuhusiana na mchezo huo.TFF itarudisha gharama za safari kwa wale wanaotokea nje ya Dar Es Salaam.




Wasalaam,
Mwesigwa Joas Selestine
General Secretary
Tanzania Football Federation
 
ikibainika kuna wahuni walimuingiza fakhi uwanjani wakijua watainufaisha simba wafungiwe kujishughulisha na mpira, na yule mchezaji wa zamani hajakoma tu kununua wachezaji wa timu ndogo ndogo, nae aitwe kasimu kake ka tigo pesa
 
Hadi tff wanatumiana email kwenye gmail hapana yaani wanashishwa kutumia email zenye domain zao. Kweli hatuko seeious
 
Figisu tu hzo simba chapa kaaaziiii
 
Wajumbe wa KAMATI ya masaa 72 si nao ni Simba hukuliona hilo eti!!??
 
Tz kwa matukio ni shida, tulianza na habari za front page za Bashite, tukaja za biashara za magari kuingizwa kama bidhaa za mitumba na ukwepaji kodi kisha habari za udaku za gwajima na bashite sasa tumefika page ya mwisho ya gazeti, michezo nako kuna la kuongea kuchangamsha vijiwe, duh!
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] umesahau ukurasa wa kat kulkua na habar za urusi na usa cjui n.korea
 
Hivi ile kamati ya masaa 72 wajumbe wengi ni wa upande upi vileeee kaswali kadogo tu.......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…