Brother, can you post that page please (SEMA USIKIKE)! Maana bila ya kuona hiyo siwezi kuchangia maada unless iondolewe kabisa hapa kwenye Forum
Wakulu msije mkanitoa roho . . . Mimi ni mjumbe tu wa kufikisha habari kama zilivyo na mjumbe hauwawi.
Kukata mzizi wa Fitina nimenunua gazeti na Ku-Scan. Here is a full Story:
MAFISADI WAPANGA KUMMALIZA MENGI
Source: Sema Usikike (Top Story), Jumatatu February 23, 2009 ISSN 0856 - 5414 No. 006 (Kama noma na iwe noma . . . !)
- Wafanya Vikao Usiku Kupanga Mikakati ya Kumchafua
- wapanga Kumhusisha na Mauaji ya Albino
- Wasambaza Vipeperushi Makanisani na Mashuleni
- Vitaandikwa kuwa Anafadhili Mtandao wa Madawa ya Kulevya Hapa Tanzania
- Kazi Hiyo Kuanza Hivi Karibuni
- Waandaa Vijana Watakaotoa Ushahidi wa Uongo
- Wadai Pia amemtoa Mwanawe Kafara Apate Utajiri
Mafisadi wapanga kummaliza Mengi
Katika ya kutaka kuzima kasi ya wenyekiti wa Makampuni ya IPP, Bw. Reginald Mengi ya kupiga vita ufisadi, baadhi ya mafisadi wamefanya kikao juzi usiku na kuamua kumchafua kwa kudai kuwa anahusika na mauaji ya Albino na kwamba amemuua mwanawe kwa - kumtoa kafara ili apate utajiri. -zilizopatikana katika kikao hicho, mafisadi hao wamepanga mikakati ya kuhakikisha wanammaliza Bw. Mengi na kumfanya anuke katika jamii.
Lazima tuhakikishe kuwa tunammaliza na ananuka katika jamii. Si anajifanya mpiganaji wa wanyonge? Safari hii haponi, akasema mwenyekiti wa kikao hicho ambaye jina lake linahifadhiwa.Kwa mujibu wa kikao hicho, mikakati inayoandaliwa ni kwamba mafisadi hao wamepanga kushirildana na baadhi ya waandishi wa habari kumuhusisha na mauaji ya albino hapa Tanzania iii kumchafua.
Taarifa zinasema kuwa mafisadi hao watasambaza vipeperushi mitaani hasa makanisani na mashuleni vildeleza jinsi Bw. Mengi anavyohusika na mauaji ya albino kwa sababu ya kutaka kupata utajiri zaidi.
Pia wamedai kuwa ili kummaliza Mengi vipeperushi hivyo pia vitaeleza jinsi alivyomuua mwanawe kama kutoa kafara ili utajiri wake uongezeke. Wamesema watafanya hivyo ili kuwaonyesha wananchi kuwa kama Mengi ameweza kumtoa mwanawe kafara, atashindwaje kuhusika na mauaji ya albino?
Uchunguzi Wa SEMA USIKIKE pia umepata taarifa za msiri wake aliyekuwa katika kikao hicho kuwa katika vipeperushi hivyo vitaandikwa jinsi Mengi anavyohusika na mtandao wa madawa ya kulevya na kwamba tayari mafisadi hao wamewarubuni vijana watakaotumika kutoa ushahidi wa nongo kumsingizia Bw. Mengi katika vyombo vya habari. Jnadaiwa kuwa vijana hao pia watatumika kumkandamiza Bw. Mengi kama suala hilo litapelekwa xnahakamani.
Kachero wa SEMA USIKIKE ambaye alikuwa katika kikao hicho amesema kuwa watu wote waliokuwa katika kikao hicho waliapishana kuwa atakayetoa ski ya mikakati inayoandaliwa atauawa kwa kupigwa risasi ama kusababishiwa ajali au kwa sumu.